Tanzania watu walionyooka hawatakiwi?

yvegenc prymacov

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
1,526
1,913
Habari,

Moja kwa moja kwenye mada, hivi Tanzania watu wachapa kazi wanyoofu, wasiopenda mizaha kazini kwanini huwa na maadui wengi? Au maadui wao ni yale magenge ya wahalifu wanayopambana nayo ndio huwajengea chuki?!

Kwa mfano najiuliza kwa kijana Paul Makonda, mkuu wa mkoa pekee aliyepambana kulijenga jiji la Dar, ndiye mkuu wa mkoa pekee aliyepambana na magenge ya wahalifu kama wauza madawa ya kulevya na watumiaji wake, kipindi cha Paul Makonda usingeweza kukutana na panya Road.

Lakini leo, Paul Makonda amefanikiwa kujitengenezea maadui wengi sana nje ya chama na ndani ya chama, kama ilivyo kwa Hayati Magufuli tu.

Ndiyo maana inafikia kipindi najiuliza, je Tanzania watu walionyooka hawatakiwi?
 
Kwa mfano najiuliza kwa kijana Paul Makonda, mkuu wa mkoa pekee aliyepambana kulijenga jiji la Dar, ndiye mkuu wa mkoa pekee aliyepambana na magenge ya wahalifu kama wauza madawa ya kulevya na watumiaji wake, kipindi cha Paul makonda usingeweza kukutana na panya Road.

Lakini leo, Paul Makonda amefanikiwa kujitengenezea maadui wengi sana nje ya chama na ndani ya chama, kama ilivyo kwa Hayati Magufuli tu.

Ndiyo maana inafikia kipindi najiuliza, je Tanzania watu walionyooka hawatakiwi?
Mkuu swali lako ni kama tayari umekwisha jijibu mwenyewe.

Tz ina jamii ya watu wanafiki na wazushi sana.

Fitina za Makonda zilianza kupikwa alipoivagaa vita ya madawa.

Chuki ya Magufuli ilianza baada ya kuwachuchumalisha kichura "mafisadi papa".

Lakini jamii kwa kuwa ni nyepesi kusadikishwa uongo, basi fitina za kupikwa ni rahisi sana kuvuruga sifa ya mtu kwsma kuwa uongo kugeuzwa kuwa ukweli na kuaminiwa na majority ni rahisi sana.

Kuna makala niliwahi kuuliza humu: " Makonda katika uongozi wake alifanya kosa gani kubwa la kijinai"?

Hakuna hata mmoja mpaka leo aliyenijibu swali hilo.

Uelewe kuwa mtu mwadilifu na mnyoofu nchi hii hana nafasi, isipokuwa kwa walamba viatu, wafitini na wanafiki ndiyo walioshika nyadhifa za juu kwa kuonekana ndiyo watu wema na wazalendo.
 
Fitina za Makonda zilianza kupikwa alipoivagaa vita ya madawa.
Kuna hata Muuza madawa mmoja alikutwa na hatia?

Nyie ni kundi la watu wenye chuki dhidi ya matajiri mnadhani wao ndio wamewatia umaskini.

Kila mtu anayeinuka na asiye unga mkono chama chako cha mafisadi mnambambikia kesi za madawa.

Hilo Mungu amezuia ndio maana akamfunga break.
Ktk watu zaidi ya 20 aliotuhumu madawa nitajie hata mmoja aliyekutwa na hatia.
 
Wewe unajua namna rushwa zilivyotamalaki kwenye vyombo vya sheria?

Chochote kinaweza kupindishwa kwa rushwa, hata kama mtu katenda ataonekana hakutenda na kesi akashinda ama kutokushitakiwa kabisa.

Nikuulize, biashara ya dawa za kulevya ipo au haipo nchini?

Kwanini mtuhumiwa hata mmoja asipatikane na hatia?

Mimi siyo msisiem, tafadhali usiniweke katika kundi hilo.

Kwa namna Makonda alivyokuwa akifanya kazi zake miye binafsi nilimfurahia.

Maana pamoja na mengi aliyoyafanya, aliingilia sana michongo ya kitapeli hasa ihusuyo viwanja na dhulma nyinginezo akasaidia wenye haki.

Nihitimishe kwa kusema kwamba, hadi leo sijadhihirishiwa na mtu yeyote kuhusu jinai aliyoifanya Makonda akiwa ofisini kama Rc.

Mawe anayotupiwa, mengi yanatokana na hayo niliyoeleza hapo juu, ni chuki za kuharibu michongo ya kihalifu aliyoifanya hakuna jengine!

Mimi na wewe tuendelee na misimamo yetu ya kumpenda ama kumchukia kwa sababu chochote afanyacho binadamu lazima kilete impact ya pande mbili za kufurahiwa ama kuchikiwa.
Na hakuna binadamu anayependwa ama kuchukiwa na watu wote.
Alamsiki.
 
Ni kama Yesu tu, aliwaumbua viongozi wa serikali na WA dini, matokeo yake wakamtundika msalabani.
 
Habari,

Moja kwa moja kwenye mada, hivi Tanzania watu wachapa kazi wanyoofu, wasiopenda mizaha kazini kwanini huwa na maadui wengi? Au maadui wao ni yale magenge ya wahalifu wanayopambana nayo ndio huwajengea chuki?!

Kwa mfano najiuliza kwa kijana Paul Makonda, mkuu wa mkoa pekee aliyepambana kulijenga jiji la Dar, ndiye mkuu wa mkoa pekee aliyepambana na magenge ya wahalifu kama wauza madawa ya kulevya na watumiaji wake, kipindi cha Paul Makonda usingeweza kukutana na panya Road.

Lakini leo, Paul Makonda amefanikiwa kujitengenezea maadui wengi sana nje ya chama na ndani ya chama, kama ilivyo kwa Hayati Magufuli tu.

Ndiyo maana inafikia kipindi najiuliza, je Tanzania watu walionyooka hawatakiwi?
Kwanini Marekani imemzuia Makonda kwenda nchini kwao? walitoa sababu, Je kuna ukweli wowote kwenye zile sababu? Au Marekani walijitungia tu bila utafiti wowote?, Makonda alikuwa mbunifu sn, mchapakazi, ila nyuma ya pazia pia pengine kulikuwa na mengi ambayo hatuyasikia kwenye vyombo vya habari ambayo yaliwafanya watu wamchukie, ile ishu yake na Bishop Gwajima mliiona. Hivyo kama binadamu anamapungufu yake, mabaya yake lakini pia ana mazuri yake. Rejea kwa Sabaya, tulimuona ni mchapakazi lakini baadae unaona alitenguliwa na kufunguliwa mashtaka kwa mambo ambayo tulikuwa hatuyasikii kwenye vyombo vya habari.
 
Kuna kizazi cha machawa siku hizi,kipo mpaka kwenye taasisi nyingi, wanapewa mpaka vyeo na wanasahau ufanisi wa mtu ktk kufanya kazi.

Na kinazidi kuongezeka.
 
Back
Top Bottom