Tanzania: Vyeti bandia, elimu za kununua na watumishi vihiyo

Mkuu Max,
Asante sana kwa juhudi zako naona utalikomalia hili swala hadi kieleweke.
Nashangaa hakuna wadau wa Arbor WAMEWEZA KU COMMENT na wako wengi sana.


Kufuatana na search ya Department of Corporation New Mexico, Arbour University haijasajiliwa hapo.

See: http://www.nmprc.state.nm.us/cii.htm

http://www.nmprc.state.nm.us/cgi-bin/prclist.pl?corpname=ARBON+EQUIPMENT+CORPORATION&direction=P

Ina weza kuwa ni foreign corporation. Ninafanya search ya US nzima.

Thanks
 
Wamemweka Dr Stella Bendera wa Wizara ya Elimu kama contact person wao hapa Tanzania!
Mwenye contacts za Dr Bendera awasiliane naye ili atueleze ni vipi anawakilisha Chuo ambacho hakipo.


Dr Bendera yupi? Yule ambaye nasikia yupo Menejimenti ya Utumishi kwa sasa?
 
nimesikia kwenye habari redioni kuna jamaa ametunga kitabu maalum juu ya mawaziri kumi wadnaganyifu na wenye vyeti feki na anaomba kipitishwe
 
kuweka mambo sawa tu ramadhani kihiyo aligombea jimbo la temeke 1995 akashinda kabla ya kung'olewa mahakamani chini uwakili wa dr. Masumbuko lamwai kwa kuforge vyeti vya dar tech hivi sasa dit, sijui lamwai naye sasa hivi yupo wapi maana toka arudi ccm kawa kama kafunikwa mtungini.


lamwai yupo kwenye acedmic zaidi kama dean of faculty, tumaini university dsm college, bado anaendelea na law firm yake japo inaonekana ajapata kesi kubwa ya kutikisa kwa muda mrefu.
 
lamwai yupo kwenye acedmic zaidi kama dean of faculty, tumaini university dsm college, bado anaendelea na law firm yake japo inaonekana ajapata kesi kubwa ya kutikisa kwa muda mrefu.

Huyu alishajifunga mikono baada ya kurudi CCM, sasa hivi ni kama buoyer tu, haumi tena. Count him out.
 
Ha! Ha! Ha ! Watanzania tuendelee kupokea mlio wa fedha badala ya fedha yenyee. kalakabaho
 
Hili suala la vyeti feki ni la kufutuatiliwa na Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi an Teknolojia. Sijui kama wazir na katibu mkuu wake hawana taarifa hizi. Kuhakiki kuwepo au kutokuwepo kwa taasisi ya elimu ya juu katika dunia ya sasa ni kitu rahisi sana hata kama chuo kingesemekana kuwa ndani ya jimbo hatari la Helmand.
 
Kwa haraka haraka kuna vitu viwili vya kuangalia katika vyuo vya elimu ya juu ya USA
1 Registration - registration ni rahisi na karibia kila chuo kina registration, hata mie nikianzisha chuo mda huu naweza pata hiyo registration.
2. Accreditation - Ngoma iko katika accreditation, hii lazima wataalamu waje wapitia degree na michepuo unayotoa, kuangalia level ya walimu na qualification zao, hii sio rahisi kupata kama unatoa vyeti feki na ha-umeet standard za elime, the most popular accreditation board is the Nortch central ya Illinoi - chicago, nafikiri hii information itasaidia. Bila acceditation hakuna kitu, na pia ukiona accreditation nenda ukaifanyie uchunguzi kidogo uone ni accreditation ya nini na masharti yao ni yapi, kila kitu kinawekwa wazi.
 
Mwanasiasa,


Jamani tunajaribu kutafuta kitu gani hapa?... Digri ya Tumaini haitambuliwi Marekani, Je hii ina maana digri hiyo ni fake? Naa hata kama ina address na majina ya maprofesa wa Tumaini hii itamsaidia nini msomi wa Marekani?

Hii si kweli kwamba Degree ya Tumaini haitambuliwi Marekani ... hebu tuzungumze hoja hapa - issue is whether these individuals are awarded degrees from not "unaccredited" institutions, but institutions that do not exist!
 
Naomba kutoa hoja kwa wanafamilia wa JF.

Mimi naona kuna ulazima kwa mamlaka husika kuunda tume itakayoshirikisha wakuu wa vyuo vyote vilivyopo hapa nchini na kuwasiliana na wale wa vyuo vya nje ili kufahamu au kujilizisha na vyeti vya baadhi ya waajiriwa serikalini.

Juzi tumesikia waheshimiwa wawili tena wenye vyeo vya juu wakituhumiwa kwa kuwa na vyeti bandia na hivyo elimu yao kutilia shaka, mimi naamini si hao tu wapo wengi wenye vyeti bandia au vya marehemu wakivitumia kujipatia ajira isiyowahusu.

Tanzania haiwezi kuendelea, mtu mwenye cheti bandia hata kazi zake nazo ni bandia tuuu...
 
Hapo ulipogusa ni penyewe hasa, lakini hao ni rafiki wa CCM. Nani kasahau Habari ya Bwana Kihiyo na Lamwai? Lakini cha ajabu naambiwa kwamba mheshimiwa kihiyo sijui yupo nje ya nji kama sehemu ya wafanyakazi wa ubalozi akila matunda ya tanzania huru na kodi zetu, shame on CCM!!
 
Back
Top Bottom