Ni vizuri
Tutafika ungefikiri vyema kabla ya kuandika.
Mimi ni Mtanzania mzalendo na hata vita nimepigana kwa ajili ya nchi yangu, ninalijua jeshi letu kuliko hata unavyofikiri wewe.
Huyo Kagame, Museveni na Kabila ni sisi Tanzania ndio tuliofanikisha mipango ya kuwaweka madarakani. Swali, je tumefaidika na nini kwa wao kuwa madarakani mpaka sasa?
Hivi unajua ni Tanzania ndio tuliopendekeza Rwanda chini ya Kagame wawe sehemu ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Lengo letu lilikuwa ni nini?
Ni kweli Rwanda inafaidika sana na mzozo wa DRC, Swali, je sisi Tanzania tunafaidika nini na waasi wa Kihutu dhidi ya Rais Kagame?
Embu tupe faida za moja kwa moja ambazo sisi watanzania tunafaidika nazo kwa kupigana vita visivyotuhusu katika nchi nyingine?
Tanzania tunapenda kujipendekeza sana kwenye mambo ya nchi zingine ili tusifiwe kimataifa but mwisho wa siku yanatugharimu sana.
Wema usizidi uwezo!!!