Tanzania Tunataka Demokrasia ya Kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Tunataka Demokrasia ya Kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Edwin Mtei, Jul 22, 2012.

 1. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Vituko vingi vya hivi karibuni vinadhihirisha kwamba Tanzania tunahitaji kujiuliza kama tunadhamiria kwa dhati kuwa na demokrasia ya kweli.

  Katiba yetu ya sasa, Ibara 18(a) inatoa haki na uhuru wa raia kutoa maoni na fikra zake (free speach), lakini uongozi, hususan polisi, wanaonekana hawajui au hawatambui hilo.

  Katiba yetu ya sasa inaruhusu vyama vingi vya siasa (na hata hii mpya tunayoandaa sasa haiondoi hilo). Lakini ukimsikiliza mmoja wa viongozi, hususan MwanaSheria Mkuu, utadhani hajui au hatambui uhuru wa mawazo nje ya chama kimoja cha kisiasa. Ukifuatilia misimamo na mawazo ya viongozi wengi wa serikali na chama tawala utadhani hawatambui wapinzani wanatoa mchango katika kutoa changamoto na kuimarisha utekelezaji wa sera.

  Hata ukifuatilia mienendo au vituko vinavyowakabili viongozi halali wa vyama vya upinzani, hata wale waliochaguliwa rasmi na wananchi kuwawakilisha katika Bunge au Halmashauri za wilaya utadhani Serikali yetu na Chama tawala vinawaona ni maadui au waasi waliwateuwa.

  Sasa tujiulize, tunataka na tunatambua uwepo wa vyama vya upinzani katika siasa zetu? Inaonekana kuna umuhimu wa kuwa na mafunzo ya uraiya mwema miongoni mwa vijana wetu na umma kwa jumla ili muundo wa siasa na utawala tuliojiwekea kwa maksudi ueleweke na utengemae.
   
 2. M

  Magesi JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera mzee Mtei umesema ambacho wengi wameshindwa kusema
   
 3. d

  dada jane JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli utu uzima dawa. Huwa namshangaa Jaji Werema. Kwa nini anashindwa kuwa dawa ya watanzania. Mungu akubariki Mzee Mtei uje ushuhudie demokrasia ya kweli Tanzania. Ili uje useme sasa "umruhusu mtumishi wako maana ameuona wokovu" kama alivyosema Simione wa kwenye biblia.
   
 4. N

  Njaare JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM hawawezim kuwa tayari kuona chama kingine kinaibuka. Ni lazima wahakikishe wanakidhoofisha kwani wanaamini kuwa wao ndo wenye hati miliki ya nchi hii. Wako tayari kutumia ubabe wowote kuhakikisha wao tu ndo wanatawala. Ila tuanalo tumaini kuwa hata Farao alitumia ubabe wa hali ya juu kuwazuia wana wa Israel kuondoka Misri. Hata hivyo ule ubabe ndo ulikuwa kichocheo na ari ya waisraeli kuondoka Misri. Na kwa watanzania kila uongozi wa CCM hasa upande wa bunge unapofanya ubabe, unawahamasisha watanzania kibao kujiunga na upinzani.
   
 5. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimefarijika kusoma reactions za wanaJF kuhusu hili suala linalonikera kila ninaposoma vituko vya kisiasa hapa nchini.

  Sina madhumuni ya kushambulia taasisi au viongozi fulani, lakini ili nitoe dukuduku zangu zaidi kufafanua ninavyoona kwamba tunaelekea njia mbaya, niseme tu kwamba hata baadhi ya wale tunaodhani wamejiunga na vyama vya upinzani, wanaonekana wanaanza kusita.

  Kwa mfano, kwa nini wakili ambaye najua ni mwanaCDM, asiwe na ujasiri wa kusema kortini kwamba Kova na polisi wanakiuka Katiba yetu ya sasa, kwa kuwatia mbaroni kina Mnyika na Lissu, eti kwa kuhutubia huko Ndago. Ni haki ya chama cha siasa kueneza sera bila bughudha. Saidi Mwema na Kova wapewe hiyo Katiba wasome.

  Kitila Mkumbo katiwa mbaroni eti kwa kumkashifu MwanaCCM Mwigulu Nchemba. Mbona hilo ni suala ambalo mwenye kukashifiwa angeenda kortini kudai fidia? Kama kweli Polisi watashirikiana na CCM kugeuza kashfa (slander) kuwa jinai, basi ni lazima tujiulize, tunao uhuru wa mawazo kama Katiba yetu inavyotamka? Tanzania tunadhamiria kukuza demokrasia ya kweli?
   
Loading...