Tanzania tunasimama wapi kiteknolojia?

Aizi Azma

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
553
Reaction score
1,151
Well,... Kenya wanatupiga gap (Kwa maoni yangu), wana-establish Konza City na wana initiatives mbalimbali za kuhakikisha wanaendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia. Rwanda ndo usiseme, wako vizuri... mpaka tunaambiwa wamepenyeza mpaka 'chumbani' kwetu. Huwa najiuliza ina maana sisi Tanzania hatuoni jinsi teknolojia inavyotuacha? Kwanini wenye mamlaka hawaoni umuhimu wa kufanya jitihada za makusudi kama nchi za kuhakikisha tunaendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia? Dunia ina-shift kiteknolojia kwa kasi ya ajabu... Sisi tunaji-position wapi?

Hapa naongelea kuanzia mitaala mashuleni mpaka mipango tunayojiwekea kama nchi. Tusijekuwa tunatumia mtazamo na teknolojia ya mwaka 2000 kupanga mipango ya mwaka 2025... tutaachwa kwenye vumbi wakati wenzetu wakipiga hatua kubwa hasa hasa kiteknolojia.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Africa.
 
teknolojia yetu ipo sumbawanga, bado kuzinduliwa tuuu
 


Mimi, wewe na yule tunaona, kadhalika tunajitahidi tuwezavyo ili tusonge mbele, lakini je huko mbele tunakostaka kusonga kunafunguliwa milango na waliojuu!? Imani imekwisha, kama waliojuu wana mashaka juu ya tekinolojia na hawataki kujua nguvu ya tekinolojia, kamwe usitegemee kupiga hatua kwasababu nguvu hiyo ni tishio kwao
 
Hii ni 'time bomb' ... Tik tok tik tok tik..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…