Tanzania Tuna Wasomi?

Bonesmen

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
929
991
Mfumo wa elimu ya nchi yangu umekuwa mbovu sana kiukweli wakati nasoma nilifundishwa kumeza yani kukariri ili nije nifaulu mtihani kwani huyo anaenifundisha nae anadai alikariri sana na kumeza bila kuelewa sana nae akiwa na nia hio hio ya kufaulu na kupata kazi tu.

Wasomi elimu haziwasaidia maana mambo walio yakariri kipindi wameshasahau.
Wakuu hivi tunazalisha wanafunzi wa aina gani dhana ya elimu imekuwa ni theory tu bila hata practical leo ukijaribu kukaa na wanafunzi wa form six wanaosoma science ukawadadisi utagundua hali inatisha sana kama hawa tunawategemea kuwa wahandishi au madokta ni kweli taifa litapiga hatua?

Mwanafunzi wa PGM hapati shauku kabisa ya kuangalia utendaji kazi wa dunia au Wa PCM hata kujiuliza deeply why ndege inapaaa au kwanini Nje ya atmosphere mwanga unasafiri kwa speed sana Yani hawana shauku kabisa na wajifunzalo pengine hawaelewi uhalisia zaidi ya kukariri na kuja kupaste kwenye mtihani
 
Mfumo wa elimu ya nchi yangu umekuwa mbovu sana kiukweli wakati nasoma nilifundishwa kumeza yani kukariri ili nije nifaulu mtihani kwani huyo anaenifundisha nae anadai alikariri sana na kumeza bila kuelewa sana nae akiwa na nia hio hio ya kufaulu na kupata kazi tu , Wasomi elimu haziwasaidia mana mambo walio ya kalili kipindi wameshasahau Wakuu hvi tunazalisha wanafunzi wa aina gani dhana ya elimu imekuwa ni theory tu bila hata practical leo ukijaribu kukaa na wanafunzi wa form six wanaosoma science ukawadadisi utagundua hali inatisha sana kama hawa tunawategemea kuwa wahandishi au madokta ni kweli taifa litapiga hatua?
mwanafunzi wa Pgm hapati shauku kabisa ya kuangalia utendaji kazi wa dunia au Wa pcm hata kujiuliza deeply why ndege inapaaa au kwanini Nje ya atmosphere mwanga unasafiri kwa speed sana Yani hawana shauku kabisa na wajifuzalo pengine hawaelewi uhalisia zaidi ya kukariri na kuja kupaste kwenye mtihani

CHANZO: Habari Leo

UTAFITI wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Uwezo, umebaini kuwa kati ya wanafunzi 10 wanaomaliza darasa la saba, wanafunzi watatu hawawezi kufanya hesabu za darasa la pili.

Katika matokeo ya utafiti huo yaliyotangazwa Dar es Salaam jana, taasisi hiyo pia ilibaini kuwa, nusu ya wanafunzi wanaomaliza elimu hiyo ya msingi sawa na asilimia 49.1, hawawezi kusoma hadithi kwa Kiingereza.

Mkurugenzi wa Uwezo, Grace Soko, alisema jana kwamba utafiti huo ulifanywa kwa wahitimu wa shule za msingi 42,033 waliokuwepo majumbani ambao walifanya majaribio ya darasa la pili katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hesabu.

Mbali na Kiingereza, somo ambalo utafiti huo umebaini kuwa ni gumu kuliko masomo mengine, pia ilibainika kuwa mhitimu mmoja wa elimu ya msingi kati ya wahitimu watano, hawawezi kusoma hata Kiswahili cha darasa la pili.

Katika somo la hesabu, Soko alisema, "ingawa stadi za kuzidisha zipo kwenye mtaala wa darasa la pili, hakuna mwanafunzi hata mmoja wa darasa la pili aliyeweza kuzidisha bila shida, huku asilimia 31 ya wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi wakishindwa kufanya hesabu hizo.

Alisema jambo hilo linadhihirisha kuwa mhitimu mmoja kati ya wahitimu 10 wanaomaliza elimu ya msingi bila kuwa na stadi ya hisabati hawataweza kufanya masomo ya sayansi na biashara akiwa katika elimu ya sekondari.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Twaweza, Rakesh Rajani ambaye alikaribishwa wakati wa kutangaza matokeo ya utafiti huo, aliipongeza serikali kwa kuinua kiwango cha elimu kwa kuwa kuna ongezeko kubwa la uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya msingi.

"Inasikitisha kuona watoto wanahitimu darasa la saba bila kujua kusoma Kiingereza hata kile alichotakiwa kusoma mtoto wa darasa la pili, watashindwa kumudu masomo ya sekondari ambayo yanafundishwa kwa lugha hiyo," alisema.

Kutokana na matokeo hayo, taasisi hiyo ya Uwezo imebuni mkakati wa miaka minne wa kuendeleza stadi za kusoma na ujuzi wa hesabu kwa watoto wa umri wa miaka mitano hadi 16 katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.
 
Back
Top Bottom