Tanzania tuna hali ngumu lakini wenzetu Kenya Wana hali ngumu zaidi Serikal yashindwa Kulipa Mishahara!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,137
Mwenzako akinyolewa wewe tia maji

Namshauri tu Waziri wa Fedha awe anafuatilia pia yanayotokea nchi jirani au zinazotuzunguka

Hapo Kenya kwa mfano wameishiwa Fedha za mishahara na 60% ya Mapato yao wanalazimika kulipia Deni la Taifa

Nawatakia nyote Pasaka Njema!
 
Watu wanaongea mno ...full kumpondea huyu mama...sawa ana mapungufu kama sisi lakini tumeshindwa kumpa hata maneno yenye faraja Kwamba apate nguvu ya kupambana lakini tumekazana....vitu vimepanda bei....sijui kile kimefanya vile.....ung'atuke!

Ni sawa na mwanaume anapambana kutafuta pesa atunze familia,badala apate faraja toka Kwa mke anaambulia maneno kilasiku na vichambo na kutafuta mwanaume mwingine .

Hali ni ngumu kote.....sisi ni taifa la chini na uwezo mdogo kiuchumi....Kuna vita Kwa wakubwa huko tuumiao ni nyasi.....
 
Watu wanaongea mno ...full kumpondea huyu mama...sawa ana mapungufu kama sisi lakini tumeshindwa kumpa hata maneno yenye faraja Kwamba apate nguvu ya kupambana lakini tumekazana....vitu vimepanda bei....sijui kile kimefanya vile...
Umeandika vizuri sana!
Rais SSH Mungu ampe Nguvu na Moyo wa Kuvumilia.

Nchi ya Tanzania tuko mahali pazuri sana ukilinganisha na wenzetu majirani!

Hapo kwenye Watumishi wasiowaaminifu iko Shida!

Njia ni Moja tu-Uwajibikaji.

Mama usitoke kwenye Reli-Nenda mbele na waliowengi wanaona Juhudi zako.

Nadhani kinachokosekana kwa sasa ni mzunguko wa pesa huku chini...

Ili kukabiliana na hali kama hii Serikali inaweza kubuni kitu kinaitwa-Consumption Economy.

Mfano Serikali inaweza kuanza program ya Miaka 3 mpk 5 ya kulisha wanafunzi wote Mayai huko Mashuleni na Vyuoni!

Masharti tu ni kuhakikisha kwamba Mayai yote yananunuliwa kutoka kwa Wafugaji wa Ndani.

Hata kama Serikali itatumia 500Bn kwa Mwaka lakini hiyo pesa itakuwa inazunguka kwa watu wa chini na itainua Uchumi wa watu wa kawaida!

Lakini pia unaimarisha Afya ya Watoto na Vijana!

Kama Taifa tutaongeza Per capita Consumption ya Mayai.

China wameendelea kwa hii model ya Consumption Economy.

Mayai.
Maziwa.

Pesa zinalipwa nyingi kwenye Miradi mikubwa lakini zote zinaondoka kwa Sababu hakuna mwananchi mwenye uwezo wa kutekeleza Miradi kama hiyo na kama wako ni wachache sana!

Viwanda.
Wazawa wenye Viwanda wafuatwe na wasaidiwe kwa hali na Mali ili waweze kuongeza uzalishaji na ikiwezekana waongeze Viwanda zaidi...

Wapate mikopo Mizuri inayovutia UWEKEZAJI wa Viwanda...(Hili ni la Muhimu na wasichelewe)

Pesa itazunguka huku Chini na Maisha yatakuwa Matamu sanaa!

So far
Mh Rais Samia is one of the Best President in Africa as of now!
 
Kwani Katiba Mpya haijawasaidia huko?

mwanzoni walidhani kuwa na katiba mpya ingewasaidia kupata kila kitu, sasa pamoja na kitiba mpya bado mambo magumu.

Pamoja na kuwa na katiba mpya lakini hadi Leo hii Raila hana imani na Tume ya uchaguzi (IEBC) Wala mahakama!!!!!

Nakubaliana na Prof. Shivji kuwa kweli;
" katiba mpya sio mwarobaini"
 
Umeandika vizuri sana!
Rais SSH Mungu ampe Nguvu na Moyo wa Kuvumilia.

Nchi ya Tanzania tuko mahali pazuri sana ukilinganisha na wenzetu majirani!

Hapo kwenye Watumishi wasiowaaminifu iko Shida!

Njia ni Moja tu-Uwajibikaji.

Mama usitoke kwenye Reli-Nenda mbele na waliowengi wanaona Juhudi zako.

Nadhani kinachokosekana kwa sasa ni mzunguko wa pesa huku chini...

Ili kukabiliana na hali kama hii Serikali inaweza kubuni kitu kinaitwa-Consumption Economy.

Mfano Serikali inaweza kuanza program ya Miaka 3 mpk 5 ya kulisha wanafunzi wote Mayai huko Mashuleni na Vyuoni!

Masharti tu ni kuhakikisha kwamba Mayai yote yananunuliwa kutoka kwa Wafugaji wa Ndani.

Hata kama Serikali itatumia 500Bn kwa Mwaka lakini hiyo pesa itakuwa inazunguka kwa watu wa chini na itainua Uchumi wa watu wa kawaida!

Lakini pia unaimarisha Afya ya Watoto na Vijana!

Kama Taifa tutaongeza Per capita Consumption ya Mayai.

China wameendelea kwa hii model ya Consumption Economic!

Mayai.
Maziwa.

Pesa zinipwa nyingi kwenye Miradi mikubwa lakini zote zinaondoka kwa Sababu hakuna mwananchi mwenye uwezo wa kutekeleza Miradi kama hiyo na kama wako ni wachache sana!

Viwanda.
Wazawa wenye Viwanda wafuatwe na wasaidiwe kwa hali na Mali ili waweze kuongeza uzalishaji na ikiwezekana waongeze Viwanda zaidi...

Wapate mikopo Mizuri inayovutia UWEKEZAJI wa Viwanda...

Pesa itazunguka huku Chini na Maisha yatakuwa Matamu sanaa!

So far
Mh Rais Samia is one of the Best President in Africa as of now!
Huyu huyu aliyedai vita ya Ukraine itapandisha bei ya kila kitu wakati bei zilianza kupanda karibia mwaka mmoja kabla hata ya vita yenyewe. Kashindwa kazi.
 
Watu wanaongea mno ...full kumpondea huyu mama...sawa ana mapungufu kama sisi lakini tumeshindwa kumpa hata maneno yenye faraja Kwamba apate nguvu ya kupambana lakini tumekazana....vitu vimepanda bei....sijui kile kimefanya vile...
Hatuna wasiwasi wowote kwamba mama ni mwadilifu. Tatizo lake wapigaji wamemuweka kwenye kichupa hana pa kupumulia, wenye miwani myeusi wameugana na wapigaji. Sasa tumsaidieje sisi walala hoi?
 
Hatuna wasiwasi wowote kwamba mama ni mwadilifu. Tatizo lake wapigaji wamemuweka kwenye kichupa hana pa kupumulia, wenye miwani myeusi wameugana na wapigaji. Sasa tumsaidieje sisi walala hoi?
Tusitoe maneno magumu ya kumdharaulisha.....tumwambie apambane inawezekana
 
Back
Top Bottom