Tanzania tumeanza siasa za misimamo mikali?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Kuna movement kubwa ya chinichini naiona Tanzania. Tofauti na mwaka 2016 kuna mabadiliko makubwa matatu

1. Wananchi hawaogopi tena vyombo vya usalama kama zamani wala kesi za kubambikizwa. Na badala yake Mahakama, polisi na hata Jeshi haviheshimiki kama zamani kwasababu ya kuingizwa kwenye siasa

2. Siasa za Tanzania zimekuwa za kimataifa kuanzia Lissu apigwe risasi. Lissu kitu ambacho wengi hawajui kila tukio kubwa ana rekodi na kutuma kwenye email list ya viongozi wote Duniani ambao anajua wanapenda demokrasia. Kwa sasa kuanzia EU mpaka US kuna wabunge wanajua siasa za Tanzania sana kuliko hata Watanzania wengine

3. Umri wa Watanzania. Watanzania wengi ni watoto chini ya miaka 25 ni 75% sasa mwa miaka minne hii kuna vijana ambao walikuwa watoto miaka minne lakini sasa sio watoto tena na ni wengi sana. Sasa hawa karibu wote wapo kwenye mitandao na kwenye mitandao upinzani unafanya vizuri kueleza sera kuliko serikali. Serikali inaonekana ni ya wazee. kibaya zaidi hakuna kazi kwa vijana na wanaona maendeleo ni kama ya watu wazima pekee. Hawa vijana hawana magari ya kuendesha kwenye madaraja mapya, hawana pesa ya kupanda ndege mpya, hawaoni mbwawa, hawajui na hawajawahi kufika kwenye Mbuga. Hawa vijana hawajui umeme vijijini na wala hawaumwi sana kujua kwamba tuna zahanati. Hawa vijana wanachoona ni kwenye mitandao hakuna Mkenya mpinzani yuko jela wanaona wapinzani Tanzania wako jela. Wanaona wanasiasa wanapigwa risasi auwako mahakamani kila siku. Hii taswira sio nzuri kwa vijana.

Kitu kimoja ambacho ni sehemu ya kukua ni kuwa mpingaji lakini vijana wetu hawana sehemu zaidi ya mitandao. Hivyo navyoona hata kwenye mitandao na WhatApp groups kuna uoga uliokuwepo ambao haupo tena hata pale watu wanapojua wana rekodiwa kinyume na sheria. Kibaya ambacho serikali inafanya ni kwamba serikali inafanya vitu ambavyo ni tofauti na mila zetu. Nyumbani na jamii za kitanzania zinaongea hakuna kufungana, kupigana risasi wala kunyanyasana kwa kutofautiana kwenye mawazo pekee. Kitu kimoja tu ambacho Watanzania wote waliungana kupinga na kutaka Watanzania wenzao wafungwe ni kwenye ufisadi tu. Lakini hakuna ushahidi wowote kwamba wapinzani ni mafisadi. Sasa kijana wa kawaida anasema kama hawa sio mafisadi na wanafugwa je wanapigania nini sasa. Wakina Msigwa, Lema , Mdee wanawajibu ni demokrasia tu na hilo wanaanza kulielewa sasa. Sudan walijifunza kwa waarabu wa Tunisia hivihivi kwenye mitandao. Lakini baya zaidi viongozi wa nchi za nje siku hizi wamemulika sana Tanzania na Kenya. Kenya kwa kukuza demokrasia na sisi kwa kubomoa.

Miradi mingi ni mizuri sana lakini itachukua muda sana kuleta matunda. Plant ya gas ni miaka 20-30, treni kufika Rwanda na Congo miaka sio chini ya 10, miradi ya umeme mpaka umeme ushuke bei ni miaka 10, bomba la gas la Uganda miaka 10. Pamoja na miradi mizuri hawa vijana hawawezi kuielewa au huwezi kuwaeleza wakuunge mkono kwa miradi ambayo kwasasa hawana hata uelewa wa faida zake. Hivyo wataanza kuwa na misimamo mikali hasa kama uchaguzi usipokuwa huru
 
Tatizo serikali yetu sidhani kama huwa inatathimini athari za maamuzi yake kabla ya kufanya.

Leo wamewakamata wa Dar, mwezi ujao watawakamata wa Mbeya, baadae Arusha hata musoma na mikoa mingineyo.

Serikali ijitathimini jinsi ya kukabiliana na siasa za upinzani, la sivyo itazidi kukomaza usugu kwenye mioyo ya watanzania wengi..

Leo mwanaichi anaumizwa lakini watu hawastuki wanazidi kusonga mbele, kesho mwananchi atauwawa lakini watazidi kusonga mbele.

Hapo ndio serikali itajua nini maana ya wananchi, maana siku zote wananchi wanavyozidi kuumizwa na kuuwawa ndivyo wanavyozidi kusonga mbele na kuwa sugu maradufu.

Hao mnaowaumiza ni Kaka, mama, baba, na Dada zetu.. sasa siku wakiumia wote Mimi nitakuwa na nini cha kujitetea zaidi kupigania damu za ndugu zangu.?
 
Kwani nyie vichwa maji huwa mnaelewa so mnakula na kushiba lakini sisi kina pangu pakavu mnatuzidishia hasira tu subilini tu kama gadafi aliwapa wa Libya kila kitu lakini kunyimwa tu Uhuru hata wa kutoa dukuduku tu unaona kolicho tokea IPO siku tutaamua bora kukosa wote tuwe pangu pakavu maana wananeeka wachache wanaumia wengi hivi hiyo midenge mi wa myovozi ntayapandia wapi kibuli zarau na majivuno yatawaponza Tanzania ni yetu sote tunaipenda ila kujiona nyie ni bora kuliko wengine tutakuja heshimiana tu
Mambo uliyoyaandika yameshaandikwa sana tu ila naona mleta mada umeanzia mwisho kwenda mwanzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
najibu namba moja....kama huogopi vyombo vya usalama itisha maandamano uone ni wangapi watatii, cc mange kimambe! watanzania hawajahi kuwa jasiri kiasi hicho, hebu thubutu kutuita tuandamane, kuna kipindi pia wslimwaacha TL kuandamana na watu 6 wakat akiwa Rais wa Chama cha mawakili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom