Tanzania tukihit 8% ya ukuaji wa uchumi; Kenya, UG & Co. bye bye!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Sasa tunakuwa mpaka 7% Kiuchumi, tumejipanga na kuna kila dalili kuanzia mwakani nchi yetu tutahit 8% economic growth hilo likitokea hiyo ni magic number naweza kusema rasmi sasa Kenya na AM yote bye bye, tuliwapenda sana lakini ni lazima sasa tuwaaache na kuendelea na safari!

Kwa maana 8% ni magic number na hapo ndipo wataalamu wa Kiuchumi wanaposema kwamba kutakuwa na trickle down effect yaani mtu wa chini ataanza kufaidika moja kwa moja na ongezeko la Uchumi lakini ni lazima tu hit 8%, sasa ikumbukwe kwamba Kenya mpaka sasa hivi wanashindwa hata kuhit 6% ingawaje bado wana Uchumi mkubwa kutushinda lkn ni swala la muda tu kwani kama kila kitu kikienda sawa na mwakani tuka hit 8%, aisee hiyo ni bye bye tutakuwa tunamtafuta Nigeria ambaye nae ni swala la muda tu kwani Nigeria anategemea mafuta na sasa yameshuka bei na haijulikani ni lini yatapanda, Saudi Arabia yenyewe karibia miguu wakati sisi ni all round kwanza nimesikia kwamba lengo letu 10% tukihit hapo next stop AK!!
 
kibaya ni sekta zinazosaidia huo ukuaji hazina impact Ya moja kwa moja kwa mtu wa kawaida alaf kufika 8% kwa sasa ni ndoto ....
 
Nabaki nachekaa tuuh!aya maajabu yanayotabiriwa kwa Tanzania..!
 
Mtoa mada haielekei kama kweli unaufahamu uchumi vinginevyo usingeandika ulichoandika!!

Uchumi wetu bado mdogo sana tena kwahiyo kutoka 7% hadi 8% bado tutakuwa tunazunguka hapa hapa!!

Kwa uchumi mdogo kama huu kufikia hapo unaposema, basi uchumi unatakiwa kukua kwa ANGALAU 10% kwa muda usiopungua miaka 10 mfululizo... yaani steady economic growth na ndipo tutakuwa tunaifukuza Nigeria!
 
Hivi umeshawahi hisi impact ya hiyo 7% kwenye mfuko wako au kwenye maisha yako kwa ujumla..??

Hakuna ubishi kwamba Maisha ya WatanZania yameboreka kwa kiasi kikubwa sana ingawaje bado ni wachache waliofaidika lkn kuna tofauti kubwa sana ukilinganisha na tunapotoka, mfano mdogo tu miaka 10 iliyopita ilikuwa ni nadra sana kuona nyuma ina air conditioning na hii ilikuwa ni Masaki na udosini tu leo hii ukienda hata Magomeni utakua kuna nyumba zina ac hiyo ni ishara tosha kwamba maisha yamebadilika bado haitoshi lkn mabadiliko yapo tena makubwa tu!
 
Mtoa mada haielekei kama kweli unaufahamu uchumi vinginevyo usingeandika ulichoandika!!

Uchumi wetu bado mdogo sana tena kwahiyo kutoka 7% hadi 8% bado tutakuwa tunazunguka hapa hapa!!

Kwa uchumi mdogo kama huu kufikia hapo unaposema, basi uchumi unatakiwa kukua kwa ANGALAU 10% kwa muda usiopungua miaka 10 mfululizo... yaani steady economic growth na ndipo tutakuwa tunaifukuza Nigeria!

Nigeria haina Uchumi mkubwa kihivyo kama unavyofikiri, kumbuka Uchumi wa Nigeria ni kama 400 bilioni US dollars lkn kuna wa Nigeria milioni +200 yaani zaidi mara 4 ya Watz wote, ungesema kwamba ni ngumu kuifikia AK hapo ni sawa ningekuelewa kwa maana AK wana matured economy yaani ni nchi iliyoendelea tayari na itachukuwa muda mrefu sana labda double digits ya economic growth kwa miaka hata 20 kuweza kuifikia na hapo kama wao hawakuwi tena lkn siyo Nigeria, kwa maana Nigeria ukiangalia wingi wa watu wao Uchumi wao siyo mkubwa hivyo ina maana uzalishaji wao ni mdogo sana, fikiria tu Nigeria nchi yenye watu milioni 200 hawawezi kuzalisha Umeme hata ya MW 5 000 wana mgao mpka leo hii lkn sisi miaka 5 tunafika huko na zaidi!
 
Kwanza uchumi wa Nigeria ni almost +$500 Billion against less than $50 Billion za Tanzania... angalia hiyo difference!

Hata tukiamua kutumia kigezo chako cha population bado ratio ya GDP to Population kwa Nigeria ni bora mara 2 zaidi kuliko kwa Tanzania na ndio maana hata per capita yao inakimbilia $3000 wakati Tanzania hata 1500 haijagusa!

Kwamba population ya Nigeria ni +200 million unatakiwa ku-cross check your data manake all statistics zinaonesha population ya Nigeria ipo btn 170 - 180 Million!

Lakini kwa upande mwingine, Nigeria ina potential kubwa kuliko Tanzania... big population ya Nigeria ni opportunity kuliko kuwa threat na ndio maana kampuni nyingi duniani zinawekeza Nigeria coz' big population means big market.

Population ilikuwa big threat back then wakati ambapo nchi nyingi zilikuwa na closed economy with lots of barriers to the flow of foreign investments. Kinyume chake, in this modern free economy, investments always zinaelekezwa kule kwenye soko kubwa... population means market!

Nigeria kutoweza kuzalisha 5000 MW sio kwamba hawawezi bali ni kv tu nchi yenyewe ni very corrupt like many other African countries. lakini unaweza kuifananisha Nigeria na Tanzania only if you don't know the power of population in a modern economy.

For the time being, the only possible immediate solution itakayokuza uchumi wetu ni gas ambayo hata hivyo itaingia sokoni si chini ya miaka 5 -7 toka sasa wakati Nigeria tayari wanazalisha still with a very larger gas reserve!

Kwamba eti bei ya mafuta imeshuka is just a matter of time. Siasa za Iran na Saudi ndizo zinawaumiza wenyewe lakini vile vile suala la Iran kuondolewa vikwazo kumemfanya aongeze idadi ya producera. But all in all, hayo yote ni mambo ya muda tu.

Lakini hata isipokuwa ni suala la muda still huwezi kulinganisha nchi inayouza mafuta kwa bei ya chini kabisa (assuming Nigeria) na ile ambayo hata hayo mafuta ya bei cha chini kabisa hayapo like Tanzania.
 
Haya mambo ya kukua kwa uchumi kama yatakuwa yanatokea ila huku chini bado tunasoma namba kamwe sitaelewa masuala ya ukuaji wa uchumi.
 
Hakuna ubishi kwamba Maisha ya WatanZania yameboreka kwa kiasi kikubwa sana ingawaje bado ni wachache waliofaidika lkn kuna tofauti kubwa sana ukilinganisha na tunapotoka, mfano mdogo tu miaka 10 iliyopita ilikuwa ni nadra sana kuona nyuma ina air conditioning na hii ilikuwa ni Masaki na udosini tu leo hii ukienda hata Magomeni utakua kuna nyumba zina ac hiyo ni ishara tosha kwamba maisha yamebadilika bado haitoshi lkn mabadiliko yapo tena makubwa tu!
Dah kweli bana.. mie nimetoka kwenye mbege sasa nakula serengeti yangu kiroho safi tu
 
Hakuna ubishi kwamba Maisha ya WatanZania yameboreka kwa kiasi kikubwa sana ingawaje bado ni wachache waliofaidika lkn kuna tofauti kubwa sana ukilinganisha na tunapotoka, mfano mdogo tu miaka 10 iliyopita ilikuwa ni nadra sana kuona nyuma ina air conditioning na hii ilikuwa ni Masaki na udosini tu leo hii ukienda hata Magomeni utakua kuna nyumba zina ac hiyo ni ishara tosha kwamba maisha yamebadilika bado haitoshi lkn mabadiliko yapo tena makubwa tu!
Umenikumbusha kwamba foleni ni ishara ya utajiri.... kumbe inaweza ikawa ni ishara ya uchache wa miundombinu, ubaya wa mipango miji, au wale wale wanaotuibia wameongeza magari...

Kwamba installation ya AC magomeni na kwingine kiwe kipimo cha maendeleo... Not 100% banaa
 
Sasa kwani wewe ulifikiri ni nini? Kama miaka 10 iliyopita Magomeni, Manzese, Temeke watu walikuwa hawana ac majumbani mwao leo hii wanazo sasa hiyo utaitafsiri vipi? Au wewe maendeleo unayapima vitu???
 
Back
Top Bottom