Tanzania Tujifunze kwa DANGOTE: Pale Viwanda, Kilimo na Ajira vinapokutana

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Dangote amejipanga Kufikia 2021 awe mzalishaji mkubwa wa kwanza wa mchele Duniani.
Kupitia mashamba Yake zaidi ya Hekari 100000, ameajiri zaidi ya wanigeria 16000.
Kama haitoshi wananchi wa eneo lake la uwekezaji/Outgrowers wanapata uhakika wa soko la Mipunga yao.

Hii haikutokea kwa bahati mbaya ila ni mpango unaoihusisha serikali ili ifike hatua nigeria isiagize mchele kutoka nje bali wao ndio wauze nje.
Haya ni matokeo ya makubalioano yaliyosainiwa na Dangote, Serikali ya Sokoto na wananchi wake.

Tuanze na Uwekezaji mkubwa ambao Sekta binafsi ipewe kipaumbele kusimamia Kilimo nchini. Tutatumia nguvu kidogo kuliko tunavyodhani sasa.

Mfano huu unatosha kutufikirisha juu ya Ardhi tunayojivunia.
Ukitaka kujua hali ya kilimo na Ufugaji nchini, Unaweza kuanzia Youtube ulinganishe wakenya,waganda na watanzani utagundua tunatambaa kwenye ardhi yenye rutuba na maji ya kutosha...
 
Hivi sasa serikali na sekta binafsi ni paka na panya

Mmoja akiona matajiri ngozi nyeusi anajua ni wezi na wapiga dili, ila wauza bombardier na yepi markez wanaojenga reli hao sio wapiga dili

Afrika ina safari ndefu sana
 
Mkuu, kwani Dangote aliyepiganiwa aanze uzalishaji wa simenti kule Mtwara ni mtu mwenye ngozi nyeupe?.

Huwezi ukakwepa kuwa na ndege kwenye dunia ya 2017, huwezi ukakwepa kuwa na reli inayofanya kazi katika karne ya leo hii.

Huwezi ukakwepa kushirikiana na makampuni makubwa ya ujenzi katika miaka ya sasa. Huwezi ukaishi kwa kutegemea akili za jana ndio zitatue matatizo ya leo hii!!.
 
Tatizo akili za Jana (ccm) ndio zinatatua matatizo ya leo,
 
Kuna mnaijeria nilikua naongea nae, akaniambia kuhusu umafia wa Dangote, kwahiyo tuwe nae makini, Dangote yupo makini sana katika ishu mikataba
 
Tatizo akili za Jana (ccm) ndio zinatatua matatizo ya leo,
Huoni kuwa hizo akili za leo na zenyewe zina ENL ambaye alipelekwa CDM na mpigaji ambaye jengo lake limebomolewa pale Mkwepu?.

Alipotakiwa mtu mwenye akili za leo, basi akili za kipigaji zikamtafuta kutoka huko huko CCM!!.

Nyinyi kaeni mtulie muwaachie watu wafanye kazi wanayoiweza. Mnapewa nafasi ya kuwaambia watanzania uwezo wenu upo vipi mnaishia kuongozwa na akili za kupenda fedha za matajiri.

Tulieni dawa iwaangie vyema, acheni kurukaruka ili sindano ifanye kazi iliyotengenezwa kufanya.
 
Uvivu ndio shida,kulima hakuna siasa,wala njaa haina siasa.Uwekezaji wa kawaida kwa kilimo cha kumwagilia kutumia tekinologia rahisi na ya kisasa,unaweza kuibadirisha Tanzania.
Kuna wakati wazungu wakulima wenye hadhi walipofukuzwa Zimbabwe wapo waliomba kuwekeza kilimo tukawatolea nje tena kwa mbwembwe.
Sera ya kilimo kwanza ilinufaisha wanasiasa badala ya wananchi walengwa.
Juzi eti mbunge machachali anadai serikali haiwekezi kiasi cha kutosha katika kilimo huku akijua kilimo kinapigwa vita na hao wabunge.Wanahodhi ardhi maelfu ya maeka hawaitumii bali wana mpango wa kuwalangua wakulima wenye utashi.
 
Kuna mnaijeria nilikua naongea nae, akaniambia kuhusu umafia wa Dangote, kwahiyo tuwe nae makini, Dangote yupo makini sana katika ishu mikataba
Ni sawa lkn hakuna mfanyabiashara asiekuwa mafia trump raisi wa usa na bado mfanyabiashara anataka tax reforms ili azidi kuweka baishara zake mazingira mazuri. Kwa hyo umafia ni nature ya ubepari
 
Back
Top Bottom