Tanzania,The home of doublestandard

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,858
Kama heading inavyojieleza.Kwakweli ukiwa na akili timamu huwezi kuunga mkono yanayoendelea katika awamu hii hata yale yalio mazuri kwasababu ya doublesstandard ya wazi kabisa.

Mifano:

Watumishi wanahakikikiwa huku wakuu wa mikoa na wilaya ambao na ni watumishi hawahakikiwi.

Watumishi wa umma wanafukuzwa kazi kwa kutumia vyeti feki huku Daudi Albert Bashite akituhumiwa kutumia cheti feki akiambiwa achape kazi.

Naibu Waziri wa zamani wa Fedha, Adam Malima anafikishwa mahakani kwa kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake wakati waziri wa zamani wa Habari,Utamaduni na Michezo,Nape Nnnauye anatishiwa bastola hadharani na anaemtishia bastola mpaka sasa anadunda urainani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar-es'salaam anatuhumiwa kuvamia kituo cha matangazo cha Clouds huku akiwa na askari lakini hata kuhojiwa hajahojiwa ila raia wengine wako mahabusu na wengine wako jela wanatumikia kifungo cha maisha/miaka 30 kwa kosa la uvamizi wa kutumia silaha.

Hiyo ni mifano michache tu miongoni mwa mingi.

Nikisema: Tanzania,the home of doublestandard nakosea?

Ukiwa mtu mwenye akili timamu na ambae ni objective,unaweza kweli kuunga mkono hata yale mema yanayofanyika kutokana na hii doublestandard?


I will never ever do that.
 
Huyu bwana mkubwa anatuumiza sana kihisia,kiufupi watanzania tunateseka kimawazo kwa mambo yanayoendelea nchi hii!
UNA VYETI FEKI ? HULIPI KODI? kama unazo sifa zote tajwa hapo lazima umuone Magufuli mbaya
 
UNA VYETI FEKI ? HULIPI KODI? kama unazo sifa zote tajwa hapo lazima umuone Magufuli mbaya
Akiwa mzuri kwako inatosha naomba usinishobokee
Nakushangaa sana unayeishi kwa vyeti alafu unajiona mjaanja
 
Niliamini makubwa sana kwa awamu hii ya 5 lkn matumaini yangu yameyeyuka yooote! mbele ni giza nene sioni kitu. Kila kukicha afadhali ya jana!
 
Niliamini makubwa sana kwa awamu hii ya 5 lkn matumaini yangu yameyeyuka yooote! mbele ni giza nene sioni kitu. Kila kukicha afadhali ya jana!
Kuna siku kigogo mwingine atafanya hiki alichokifanya Malima na hakuna hatua zitakazochukuliwa.

Hii nchi wengine ni bora tubaki watazamaji tu.
 
Back
Top Bottom