Tanzania sio mali ya Magufuli

Tanzania sio mali ya Magufuli

Nakuunga mkono mleta uzi. Ukijaribu kuangalia wale wote wanaotaja na kumsifia Magufuli kwa kiwango kikubwa ni wale aliowapa uteuzi, ama wale wote wanaotegemea kwa kujipendekeza kwao kwake atawapa nafasi ya kufanikiwa kimaisha. Wale wote wenye mapungufu katika sifa ya nafasi walizo nazo hivyo namna pekee ni kuliimba jina la kulinasibisha na kila jambo la nchi hii ili asiwazibie mlo. Mfano halisi wa huu ni rc Makonda, ukijaribu kumsikiliza anaweza kumtaja kila baada ya dk3 hata kama hana sababu ya msingi ya kufanya hivyo, kisa ni huo umiliki wa vyeti vyenye utata.

Pia rais mwenyewe ni mtu anayependa kusifiwa na kunyenyekewa, hivyo wanaomwambudu na kumtegemea kimasha wameshagundua udhaifu huu nao wanatumia udhaifu wake kama fursa. Hata hiki kilichotokea juzi kwa wanaccm kwa kushirikiana na jeshi la polisi kufanya rafu zote ni kutaka kuonyesha Magufuli anakubalika. Wapambe wake hawakuwa tayari kuuona ukweli ambao ungewaumiza. Hivyo waliamua bora heshima yao ishuke kuliko kukabiliana na ukweli ambao ungewaumiza nyoyo zao. Pia kitendo cha rais kuwa na kinga ya kutoshitakiwa kwa kiwango kikubwa imesababisha watu wadhaifu kujinyenyekeza na kujipendekeza kupita kiasi.
 
TANZANIA SIO MALI YA MAGUFULI.

Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

Kwanini wateule wengi wa rais wakitoa maagizo au kukemea jambo hasa rushwa wanasema "serikali ya Magufuli haitaki wizi" au " wizi sio wakati wake huu" au "pesa ya Magufuli hailiwi" au "pesa ya serikali ya awamu ya tano ni ya moto", na maneno mengine yanayofanana na hayo.

Wanakosea sana. Na wanamkosea rais pia. Kama kweli lengo ni pesa ya Magufuli hailiwi basi jitihada zote za kusimamia rasilimali ni za muda tu na hivyo hazina maana.

Tafsiri yake ni kuwa Magufuli akiondoka basi tunarejea tena kule . Wasaidizi wa rais lazima wajue kuwa rushwa sio ajenda ya Magufuli. Ni ajenda ya taifa Tanzania. Magufuli ni kiongozi wa hiyo ajenda tu.

Kumbe badala ya kuwaambia wananchi kuwa Magufuli hapendi rushwa, waambie Tanzania imebadili mwelekeo haipendi tena rushwa. Waambie pesa za Tanzania hazitaliwa tena, badala ya kuwaambia pesa ya Magufuli hailiwi.

China walipoamua kupambana na rushwa hawakusema Mao Tse Tung hapendi rushwa au hela yake hailiwi. Walisema taifa limebadili mwelekeo na sasa rushwa ni haramu kwa maana ya uharamu.

Maana yake hata baada ya Mao kuondoka sera ilibaki ileile kwakuwa haikuwa ya Mao bali ya taifa China. Tuwaambie watu sera ya rushwa sio ya Magufuli bali ya taifa Tanzania.

Sidhani kama rais alianza vita hii ili kujenga dira binafsi. Nadhani alilenga kujenga dira ya taifa itakayoishi miongo mingi baada ya kuondoka kwake. Huu ndio unatakiwa kuwa msimamo.

Pili, wateule wa rais hamfanyi kwa ajili ya rais. Mnafanya kazi kwa ajili ya Tanzania. Rais amekuteueni tu kwasababu anatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Kwanini basi mnapokataza mambo yanayokatazwa na sheria mnasema "Magufuli hapendi", mara "Magufuli amekataza" nk, nk. Mkuu wa mkoa au Wilaya anawaambia wananchi "Magufuli amepiga marufuku kulisha mifugo kwenye hifadhi" au " rais amekataza ujenzi kwenye hifadhi za barabara" nk, nk.

Kwanini usiwaambie sheria inakataza. Kwanini usihimize watu kufuata sheria badala ya kumuogopa Magufuli.

Tunahitaji kujenga watu ktk misingi ya kuelewa kuwa kinachofanyika sasa ktk rasilimali zetu na kwingineko si cha Magufuli. Ni cha taifa na kuwa hakitaisha hata Magufuli akiondoka bali kitaongezeka zaidi. Wajue kuwa Tanzania si mali ya Magufuli bali Magufuli ni kiongozi tu wa muda anayeonesha njia ya Tanzania ya leo na ya kesho. Na hii kazi ifanywe na wasaidizi wa rais.

Huna haja ya kumtaja taja Magufuli kila unapozuia uovu uliokatazwa na sheria. Litaje taifa na kuwa sasa limebadilika na muelekeo na muelekeo wenyewe ni huu. Wajenge watu waogope sheria badala ya Magufuli.

Wako wahalifu wamejaaliwa subira. Wameficha makucha wakisubir Magufuli aondoke. Wako tayari kusubr ht miaka 15. Wanasubira sana hawa. Na hawa ndio tunaotakiwa kukatisha tamaa kuwa vita sio ya Magufuli bali ya taifa. Na kuwa vita hii itaisha tu taifa litakapokuwa linafika mwisho wake(kiama).
Mkuu umenena vyema na ndiyo maana wasaidizi wake wamegundua vyema madhaifu ya bosi wao bosi anapenda sifa na anataka asifiwe hata kama hastahiri sifa hizi. Bashite kila baada ya dakika anamsifu bosi wake na sifa hulevya
 
..exactly...huku kumsujudia rais hivi ni ishara mbaya sana ya nchi kutawaliwa kidikteta...maana madikteta ndio wenye kupenda kusujudiwa....Na kama rais hapendi tungeshamsikia akikemea tabia hii ya watu walio chini yake...
..BTW.. Hata wanaposema hela ya magufuli wanakosea sana sana.. Maana hela si yake bali ya mlipa kodi wa tz anaepigika vilivyo kwenye utawala huu...
...inakera Na kuudhi sana pale unaposikia kiongozi akitafta sifa kwa rais kwa kutumia maneno ya kitumwa kabisa..eti tunafanya hivi maana rais nae hapendi!!....yani si sheria zinakataza bali rais hapendi......this is pure nonsense and stupidity....kwamba wao wanafanya kazi kumfurahisha rais na si kuwatumikia watanzania..... Inaudhi sana....basi tu....Na mtu aneongoza kwa kufanya hivi nchi hii ni bashite.... Yani yeye anasema kabisa kuwa anamfanyia kazi rais....hata kama anavunja sheria za nchi yeye maadamu rais atafurahi kwake sawa....ndio maana wanadiriki hata kuwadhuru wale wanaoonekana kumkera rais... Ili wamfurahishe.....

..kuna siku hii nchi itashikwa Na wenye akili na watenda haki....Na hakika aina za watu namna hii watajuta kuzaliwa...maana wataadhibiwa kwa matendo yao ya wakati huu....muda tu utasema.....
 
katiba bunge ndilo linaamua muwe na wabunge wengi kwanza
Utakuwaje na wabunge wengi kama kuna kikundi kinachoamua nani awe na nani asiwe??!! Kazi ya wananchi ni kupiga kura lakini wakurugenzi wanaamua nani asiwe!!
 
..exactly...huku kumsujudia rais hivi ni ishara mbaya sana ya nchi kutawaliwa kidikteta...maana madikteta ndio wenye kupenda kusujudiwa....Na kama rais hapendi tungeshamsikia akikemea tabia hii ya watu walio chini yake...
..BTW.. Hata wanaposema hela ya magufuli wanakosea sana sana.. Maana hela si yake bali ya mlipa kodi wa tz anaepigika vilivyo kwenye utawala huu...
...inakera Na kuudhi sana pale unaposikia kiongozi akitafta sifa kwa rais kwa kutumia maneno ya kitumwa kabisa..eti tunafanya hivi maana rais nae hapendi!!....yani si sheria zinakataza bali rais hapendi......this is pure nonsense and stupidity....kwamba wao wanafanya kazi kumfurahisha rais na si kuwatumikia watanzania..... Inaudhi sana....basi tu....Na mtu aneongoza kwa kufanya hivi nchi hii ni bashite.... Yani yeye anasema kabisa kuwa anamfanyia kazi rais....hata kama anavunja sheria za nchi yeye maadamu rais atafurahi kwake sawa....ndio maana wanadiriki hata kuwadhuru wale wanaoonekana kumkera rais... Ili wamfurahishe.....

..kuna siku hii nchi itashikwa Na wenye akili na watenda haki....Na hakika aina za watu namna hii watajuta kuzaliwa...maana wataadhibiwa kwa matendo yao ya wakati huu....muda tu utasema.....
Mkuu wa wilaya mmoja anatoa matamko hela ya Magufuli hailiwi as if Magufului ni God Father this is just a trash,Magufuli is much little than our mother Tanzania
 
Back
Top Bottom