TANZANIA SIO MALI YA MAGUFULI.
Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.
Kwanini wateule wengi wa rais wakitoa maagizo au kukemea jambo hasa rushwa wanasema "serikali ya Magufuli haitaki wizi" au " wizi sio wakati wake huu" au "pesa ya Magufuli hailiwi" au "pesa ya serikali ya awamu ya tano ni ya moto", na maneno mengine yanayofanana na hayo.
Wanakosea sana. Na wanamkosea rais pia. Kama kweli lengo ni pesa ya Magufuli hailiwi basi jitihada zote za kusimamia rasilimali ni za muda tu na hivyo hazina maana.
Tafsiri yake ni kuwa Magufuli akiondoka basi tunarejea tena kule . Wasaidizi wa rais lazima wajue kuwa rushwa sio ajenda ya Magufuli. Ni ajenda ya taifa Tanzania. Magufuli ni kiongozi wa hiyo ajenda tu.
Kumbe badala ya kuwaambia wananchi kuwa Magufuli hapendi rushwa, waambie Tanzania imebadili mwelekeo haipendi tena rushwa. Waambie pesa za Tanzania hazitaliwa tena, badala ya kuwaambia pesa ya Magufuli hailiwi.
China walipoamua kupambana na rushwa hawakusema Mao Tse Tung hapendi rushwa au hela yake hailiwi. Walisema taifa limebadili mwelekeo na sasa rushwa ni haramu kwa maana ya uharamu.
Maana yake hata baada ya Mao kuondoka sera ilibaki ileile kwakuwa haikuwa ya Mao bali ya taifa China. Tuwaambie watu sera ya rushwa sio ya Magufuli bali ya taifa Tanzania.
Sidhani kama rais alianza vita hii ili kujenga dira binafsi. Nadhani alilenga kujenga dira ya taifa itakayoishi miongo mingi baada ya kuondoka kwake. Huu ndio unatakiwa kuwa msimamo.
Pili, wateule wa rais hamfanyi kwa ajili ya rais. Mnafanya kazi kwa ajili ya Tanzania. Rais amekuteueni tu kwasababu anatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.
Kwanini basi mnapokataza mambo yanayokatazwa na sheria mnasema "Magufuli hapendi", mara "Magufuli amekataza" nk, nk. Mkuu wa mkoa au Wilaya anawaambia wananchi "Magufuli amepiga marufuku kulisha mifugo kwenye hifadhi" au " rais amekataza ujenzi kwenye hifadhi za barabara" nk, nk.
Kwanini usiwaambie sheria inakataza. Kwanini usihimize watu kufuata sheria badala ya kumuogopa Magufuli.
Tunahitaji kujenga watu ktk misingi ya kuelewa kuwa kinachofanyika sasa ktk rasilimali zetu na kwingineko si cha Magufuli. Ni cha taifa na kuwa hakitaisha hata Magufuli akiondoka bali kitaongezeka zaidi. Wajue kuwa Tanzania si mali ya Magufuli bali Magufuli ni kiongozi tu wa muda anayeonesha njia ya Tanzania ya leo na ya kesho. Na hii kazi ifanywe na wasaidizi wa rais.
Huna haja ya kumtaja taja Magufuli kila unapozuia uovu uliokatazwa na sheria. Litaje taifa na kuwa sasa limebadilika na muelekeo na muelekeo wenyewe ni huu. Wajenge watu waogope sheria badala ya Magufuli.
Wako wahalifu wamejaaliwa subira. Wameficha makucha wakisubir Magufuli aondoke. Wako tayari kusubr ht miaka 15. Wanasubira sana hawa. Na hawa ndio tunaotakiwa kukatisha tamaa kuwa vita sio ya Magufuli bali ya taifa. Na kuwa vita hii itaisha tu taifa litakapokuwa linafika mwisho wake(kiama).
Kwani huko ccm mna maamuzi zaidi ya raia wa taifa hili? Kwa maneno yako haya unathibitisha kuwa ccm ajenda ya siri na taifa hili kwani mliingia mikataba ya kishenzi ya kuuza nchi kwa hao mnaowalamba miguu leo! Tamati yenu haipo mbali kwani uzee na ukongwe wenu unawafanya msiweze kufikiri sawasawa! Na siku hao polisi wakichoka dhukuma mnazowafanyi baba na babu zao, hakuna rangi mtaacha kuiona!Katiba ya warioba utaisubiri sana tena sana hakuna kitu kama hicho uko kwenye safari ya lowasa ya matumaini hewa
katiba bunge ndilo linaamua muwe na wabunge wengi kwanzaKama mnapendwa na mnajiamini Kwanini hamkubali taasisi na vitu vinavyotoa haki kwa wote eg katiba, tume huru nk. ?!!!
Kwani Bashite anamheshimu Warioba?Tanzania sio Zimbabwe ndio maana ni nchi tofauti zenye majina tofauti. Grace Mugabe alichochemka ni kutoheshimu wapigania Uhuru wa Zimbabwe akina munangagwa wakati yeye familia yake wala wazazi wake hawakupigania Uhuru wa Zimbabwe ndio maana jeshi LA Zimbabwe likampiga mateke grace Mugabe na hawara yake Mugabe.Jeshi LA Zimbabwe limerudisha kuwakabidhi waliopigania Uhuru wa Zimbabwe akina munangagwa sio akina grace Mugabe ambaye hata vita ya kupigania Uhuru ya chimulenga hajui ni kitu gani.Grace Mugabe ni bull shit don't refer her here ni malaya tu wa Zimbabwe
Mfalme Binta.Kwani unadhani wao hawana akili? Wanajuw jamaa anzvyopenda sifa. Alafu kweny uchaguzi uliopita 2015 kama unakumbukumbu uliwahi kuona kofia au nguo imeandikwa chagua ccm!!! Yey anadhani asingekuw yey ccm isingepita. Ndo hayo unuyoyaona mkuu. Yey anajuw kuw kila kitu ni mwenyew. Hapangiwi.
Mafarisayo walikuwa wabishi kuliko wewe.Endelea kuota mchana wa saa saba wakati watu wapo lunch![]()
Shamba lisilo na mwenyewe mwenye jina binafsi hilo ni shamba la ngedere
mnaokototeza viji mafanikio hewa baada ya uchumi kusinyaaKwasababu anaamini kuwa yeye ni Mtumishi wa watu ndio maana hata hili la mfumo wa kukusanya kodi amelifanikisha
endelea...
Mfumo wa Rais wa Kukusanya Mapato Kielekroniki eRCS umepaisha mapato ya kodi ya makampuni ya simu kwa asilimia 102%
Mfumo wa Rais wa Kukusanya Mapato Kielekroniki eRCS umepaisha mapato ya kodi ya makampuni ya simu kwa 102%
Mfumo wa Kukusanya Mapato Kielekroniki (eRCS) umeonyesha mafanikio makubwa kwa miezi mitatu ya mwanzo ya Julai, Agosti na Septemba 2017, baada ya Makusanyo ya Kodi kwa Upande wa Zanzibar (ZRB) kupitia eRCS kufikia Shilingi Bilioni.7.2, ukilinganisha na Shilingi Bilioni 3.5, ZRB walizokusanya kipindi Kama hicho mwaka 2016 kabla ya mfumo wa eRCS.
Makusanyo hayo yakiwa ni Ongezeko la Shilingi Bilioni 3.6 sawasawa na asilimia102%. Ni zaidi ya Mara mbili ya makusanyo ya mwaka Jana kabla ya mfumo wa eRCS, yanayofikia shilingi Bilioni 7.2 ni majumuisho wa Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty) na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Baada ya kukata Marejesho.
Wakati huo huo Taarifa tulizonazo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni kwamba makusanyo ya kodi yanayotokana na kampuni za simu, kwa kutumia eRCS TRA wamefanikiwa kuongeza makusanyo kwa asilimia 21% kwa kukusanya Jumla ya shilingi Bilioni 128.9 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba 2017, ukilinganisha na makusanyo ya miezi ya Aprili, Mei na Juni 2017 kabla ya kuanza kutumia mfumo wa eRCS.
Aprili, Mei na Juni 2017 kabla ya eRCS, makampuni ya simu saba yalilipa jumla ya kodi ya Shilingi Bilioni 101.7.
Julai, Augusti na Septemba 2017, baada ya kuanza kutumika eRCS, Makampuni ya simu yale yale yameweza kulipa Shilingi Bilioni 128.9. Kukiwa na ongezeko la Shilingi Bilioni 27.2 sawa na 21% ambazo ni majumuisho yaliyotokana na kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) na Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty).
Ukijumuisha makusanyo yanayotokana na Kodi kutoka kampuni za simu saba kuanzia mwezi Aprili 2017 mapaka mwezi Septemba 2017 TRA imekusanya Jumla ya Shilingi Bilioni 230.7. kwa kipindi cha miezi sita tu, ambazo ni wastani wa shilingi Bilioni 38.5 kwa mwezi.
Taarifa tulizopata kutoka chanzo chetu ambao hawakutaka majina yao yatajwe wametueleza kwamba Serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu unaofanywa na kampuni za simu katika Taarifa zao walizozipeleka TRA za input kwa ajili ya “return” ambazo zinakosa uhalisia kwani zinajumuisha taarifa za miezi iliyopita kwa lengo la kuongeza kiwango cha input tax.
Mfumo eRCS ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamad Shein walipozindua Dirisha la kukusanya kodi Kielekroniki Elecrtronic Revenue Collection System (eRCS) tarehe 1 Juni 2017, ukiwa na lengo la kusaidia Mamlaka zote mbili za Mapato yaani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB) kuongeza mapato yanafanyika kupitia njia za kielektroniki.
Mpaka Mwezi Novemba 2017, ni kampuni saba za simu ndizo zilizounganishwa katika mfumo wa eRCS, Kampuni hizo ni Vodacom, TTCL, Airtel, tiGO, Halotel, Zantel na Smart.
Taarifa hii imeandikwa kutokana na taarifa zinazopatikana
IDC, TRA na ZRB
Novemba 2017.
Acha kuweweseka. Tulia wewe. 43-1 imekuchanganyaTANZANIA SIO MALI YA MAGUFULI.