Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 97
- 1,751
TANZANIA SIO MALI YA MAGUFULI.
Kwanini wateule wengi wa rais wakitoa maagizo au kukemea jambo hasa rushwa wanasema "serikali ya Magufuli haitaki wizi" au " wizi sio wakati wake huu" au "pesa ya Magufuli hailiwi" au "pesa ya serikali ya awamu ya tano ni ya moto", na maneno mengine yanayofanana na hayo.
Wanakosea sana. Na wanamkosea rais pia. Kama kweli lengo ni pesa ya Magufuli hailiwi basi jitihada zote za kusimamia rasilimali ni za muda tu na hivyo hazina maana.
Tafsiri yake ni kuwa Magufuli akiondoka basi tunarejea tena kule . Wasaidizi wa rais lazima wajue kuwa rushwa sio ajenda ya Magufuli. Ni ajenda ya taifa Tanzania. Magufuli ni kiongozi wa hiyo ajenda tu.
Kumbe badala ya kuwaambia wananchi kuwa Magufuli hapendi rushwa, waambie Tanzania imebadili mwelekeo haipendi tena rushwa. Waambie pesa za Tanzania hazitaliwa tena, badala ya kuwaambia pesa ya Magufuli hailiwi.
China walipoamua kupambana na rushwa hawakusema Mao Tse Tung hapendi rushwa au hela yake hailiwi. Walisema taifa limebadili mwelekeo na sasa rushwa ni haramu kwa maana ya uharamu.
Maana yake hata baada ya Mao kuondoka sera ilibaki ileile kwakuwa haikuwa ya Mao bali ya taifa China. Tuwaambie watu sera ya rushwa sio ya Magufuli bali ya taifa Tanzania.
Sidhani kama rais alianza vita hii ili kujenga dira binafsi. Nadhani alilenga kujenga dira ya taifa itakayoishi miongo mingi baada ya kuondoka kwake. Huu ndio unatakiwa kuwa msimamo.
Pili, wateule wa rais hamfanyi kwa ajili ya rais. Mnafanya kazi kwa ajili ya Tanzania. Rais amekuteueni tu kwasababu anatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.
Kwanini basi mnapokataza mambo yanayokatazwa na sheria mnasema "Magufuli hapendi", mara "Magufuli amekataza" nk, nk. Mkuu wa mkoa au Wilaya anawaambia wananchi "Magufuli amepiga marufuku kulisha mifugo kwenye hifadhi" au " rais amekataza ujenzi kwenye hifadhi za barabara" nk, nk.
Kwanini usiwaambie sheria inakataza. Kwanini usihimize watu kufuata sheria badala ya kumuogopa Magufuli.
Tunahitaji kujenga watu ktk misingi ya kuelewa kuwa kinachofanyika sasa ktk rasilimali zetu na kwingineko si cha Magufuli. Ni cha taifa na kuwa hakitaisha hata Magufuli akiondoka bali kitaongezeka zaidi. Wajue kuwa Tanzania si mali ya Magufuli bali Magufuli ni kiongozi tu wa muda anayeonesha njia ya Tanzania ya leo na ya kesho. Na hii kazi ifanywe na wasaidizi wa rais.
Huna haja ya kumtaja taja Magufuli kila unapozuia uovu uliokatazwa na sheria. Litaje taifa na kuwa sasa limebadilika na muelekeo na muelekeo wenyewe ni huu. Wajenge watu waogope sheria badala ya Magufuli.
Wako wahalifu wamejaaliwa subira. Wameficha makucha wakisubir Magufuli aondoke. Wako tayari kusubr ht miaka 15. Wanasubira sana hawa. Na hawa ndio tunaotakiwa kukatisha tamaa kuwa vita sio ya Magufuli bali ya taifa. Na kuwa vita hii itaisha tu taifa litakapokuwa linafika mwisho wake(kiama).
Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.