Tanzania Premier League: Simba SC 0 - 0 Lipuli FC zatoshana nguvu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika la mtifuano wa ligi kuu ya Tanzania bara TPL, linatarajia kutimua vumbi leo Ijumaa Novemba 23, 2018 na kesho kutwa ambapo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mabingwa wa nchi wana Lunyasi, Pasi mia, Simba SC watawakaribisha wana Paluhengo Lipuli FC.

Kwa mchezo wa leo Simba inahitaji ushindi ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu TPL, kabla ya kuwakabili Mbabane Swallows ya Swaziland katika ligi ya Klabu bingwa Afrika utakaovurumishwa Novemba 27/28 kwenye uwanja wa Taifa. Kumbuka mchezo huu utashuhudia mubashara kupitia Azam Sports 2 kuanzia saa 10:00 jioni.

Vikosi vya timu kwa pande zote mbili kwenye mchezo wa leo hadharani
IMG_20181123_140139_105.jpeg
IMG_20181123_140115_052.jpeg
IMG_20181123_140157_031.jpeg


Uwanja wa Taifa..Mpira umeanza ni mchezo wa TPL

Simba SC 0-0 Lipuli FC

Timu zimeanza kwa mashambulizi kwa pande zote kwa zamu.

04' John Bocco anakosa bao baada ya shuti lake kupanguliwa na golikipa wa Lipuli FC...ilikuwa hatari sana

07' Simba wanapoteza nafasi nzuri ya kuandika bao..Shuti kali John Bocco kudakwa na golikipa wa Lipuli

10' Matokeo bado bila bila uwanja wa Taifa

Timu zishambuliana kwa zamu..Lipuli wanakwenda kwenye lango la Simba

20' Simba SC 0-0 Lipuli FC

28' Lipuli FC wanakosa nafasi ya wazi kuandika bao baada ya Beki Bukaba kupokonywa mpira na mchezaji wa Lipuli na kupiga shuti lililookolewa na Aishi Manula.

Wawa na Bukaba wanashindwa kukaa sawa huenda Kocha wa Simba akafanya mabadilko kidogo.

30' Kwa mara nyingine tena Lipuli wanakosa bao..Ni kazi nzuri ya golikipa Aishi Manula kupangua shuti na kumkuta mchezaji wa Lipuli na kupiga nje nakuwa goal kick

35' Simba SC 0-0 Lipuli FC

Anakwenda kwenye Benchi Paul Bukaba anaingia James Kotei upande wa Simba SC

40' Faulo kuelekea lango la Lipuli baada ya golikipa kuucheza mpira nje ya 18 wakati Bocco akienda kumsalimia..

Inapigwa faulo lakini haikuzaa matunda

Lipuli wanajaribu kupanga mashambulizi lakini mabeki wa Simba akiongozwa Wawa wanaokoa hatari zote..!

45+3' Ni Mapumziko uwanja wa Taifa mchezo wa Simba na Lipuli ambapo wanatoka bila kwa bila

Simba SC 0-0 Lipuli FC

Kipindi cha pili kimeanza kwa mchezo wa TPL

Lipuli wanatengezea nafasi kwa kujaribu kulifikia lango la Simba..Lakini Simba nao wanazidi kuliandama lango la Lipuli kuona kama wanaweza kupata bao

60' Simba SC 0-0 Lipuli FC

72' John Bocco leo anazidiki kukosa bahati ya kuiandikia timu yake bao..nafasi nyingine tena anapoteza

74' Kichuya anatoka nafasi yake anaingia Haruna Niyonzima upande wa Simba SC

Lipuli wakwenda kumjaribu Manula..lakini Wawa anahakikisha kuwa hakuna kumfikia

77' Goo la la, Ilikuwa hatari lango la Lipuli ni Kapteni John Bocco anapoteza nafasi kwa mara nyingine tena..Leo si yeye tena

80' Simba 0-0 Lipuli FC uwanja wa Taifa.

Rashid anakwenda na kupiga shuti lakini golikipa wa Lipuli anakaa sawa..ilikuwa nafasi murua kwa Simba

90+5 kuelekea kumalizika mchezo huu wa TPL

Naaaaaaaam Mpira umekwisha ambapo timu zinatoka suluhu ya bila kufungana, pamoja na kuwa na mashambulizi makali kwa pande zote lakini Simba walionekana kuwa bora zaidi kutafuta mabao lakini bahati haikiwa yao.

Simba SC 0-0 Lipuli FC

Pamoja na wote hapa JF walioshiriki kuleta mchezo huu shukrani kwenu

Asanteni...Ghazwat
 
Patashika la mtifuano wa ligi kuu ya Tanzania bara TPL, linatarajia kutimua vumbi leo Ijumaa Novemba 23, 2018 na kesho kutwa ambapo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mabingwa wa nchi wana Lunyasi, Pasi mia, Simba SC watawakaribisha wana Paluhengo Lipuli FC.

Kwa mchezo wa leo Simba inahitaji ushindi ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu. Kumbuka mchezo huu utashuhudia mubashara kupitia Azam Sports 2 kuanzia saa 10:00 jioni.

Vikosi vya timu kwa mchezo wa leo hadharaniView attachment 943891View attachment 943892View attachment 943893
Ligi yenyewe hii . Timu zetu za taifa zinafungwa na Burundi , Cape Verde, Lesotho n.k.
Hata sijui furaha yako ni nini ?! Ligi ya Kiswahili na wanafki

Tubaki kutambiana humu humu. Haina maana yoyote.
 
Back
Top Bottom