Tanzania niipendayo kweli ndiyo hii?

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Nilipokuwa kijana wa miaka takriban kuanzia 6 au 7 hivi nilizoea kwenda shambani na mama,mimi nikiwa nyuma yeye akiwa ametangulia.Mama yangu Mungu amrehemu sana,sasa ni mzee wa miaka 77, lakini bado ana nguvu,kwa vile hali 'matakataka' kama sisi.Kule shamba sikuwa hasa nafanya kazi,kwa kweli ilikuwa ni kumpa tu mama company.Nilichokiona wakati ule na sasa ni tofauti kabisa.Aina mbalimbali za maboga,miwa,majani ya kondeni,miti nakadhalika ambayo ilikuwepo wakati ule leo haipo kabisa.Kinachoendelea hasa ni ni nini mpaka bayoanuai ipotee kiasi hiki?Mungu anajua.Mama aliponiambia twende shamba nilikubali hata bila kusita,kwa vile niliamini kwa dhati kwamba alichoniambia mama kilikuwa sahihi kabisa.Leo hii ukimrudi mtoto hata pale ambapo amekosa utakumbana na matusi,kebehi na kejeli kiasi kisichoweza kutamkika,kinachoendelea hasa ni nini? Jamii imekumbwa na magonjwa katika kiwango cha kutisha,mengi yakiwa mapya.Sambamba na magonjwa vifo navyo vimeongezeka katika kiwango cha kutisha.Mazingira yanaendelea kuharibika, mvua nazo zinazidi kutupa mkono na njaa inazidi kuongezeka.Cha kushangaza ni kwamba wala hatustuki sana na tunaendelea na maisha 'as if there is no problem.'Mtu makini ataona kwamba hakuna tena maadili katika jamii yetu,kila mtu anafanya analoona linamfaa yeye,wala jamii inayomzunguuka haina maana tena.Wazazi-watu sikuhizi hakuna tena,siku hizi kuna wazazi-TV.Mtoto analoona kwenye TV ndilo la kutekeleza, la mzazi halina maana tena.Niambieni mwenzenu,kweli hii ndiyo Tanzania tuipendayo?Lakini hasa kinachoendelea ni nini?Katika siku hizi za karibuni,ufisadi,ujambazi,mauaji ya maalbino,ajali barabarani zimejitokeza katika hali yakushangaza sana.Wachunguzi wa mambo watakubaliana na mimi kwamba ushirikina nao umeongezeka kwa kiasi cha kutisha sana.Lakini hasa kuna nini?Jamani mbona hatustuki?

Wale wazee kama mimi watakumbuka kitu kimoja, kwamba katika miaka ya mapema themani,kuna gazeti moja lilikuwa linaitwa Watu.Mwandishi mmoja wa gazeti hili aliripoti taarifa ya kikao ambapo Freemasons walikaa Dar-Es Salam kwa nia ya kupanga mikakati ya kuipotosha Tanzania.Mwandishi yule aliandika mambo mengi sana,lakini matokeo yake ni haya mambo tunayoyaona leo.Hatujui kwa uhakika Freemasons wana wanachama wangapi Tanzania.Lakini kwa vile nchi imeharibika sana, ninaamini wanachama wao wapo kila sehemu.Watu hawa wanamuabudu shetani,ingawa wao wenyewe wanalikataa hilo.Wanatoa makafara ya watu,na takwimu zinaonyesha kwamba pale ambapo Freemasons wapo, hata ajali nazo zinakuwa nyingi sana,na hakika hili tunaliona Tanzania leo.Nimalize kwa kusema kwamba, kama Freemasons wataruhusiwa kuendelea kuwepo Tanzania kama ilivyo sasa,matatizo yetu hayatakwisha.Naiomba serikali ichukue hatua za makusudi kabisa kukipiga marufuku kikundi hiki kiovu nchini.Najua kazi hii ni ngumu kwa vile wanachama wa kikundi hiki ndio matajiri wakubwa nchini na wafadhili wa mambo mbalimbali.Mashirika ya dini hayana ubavu tena kabisa kwani nayo yameingizwa mkenge kabisaa.Mengi yanafadhiliwa na Freemasons "au kwa kujua au bila kujua."Hapa nina wa-quote wenyewe Freemasons.
 
You are all over the place man, mara bioanuwai, mara Freemasons huwajui, mara ndiyo wanaosababisha yote haya.Stick to what you know.

Wewe unajiita "agricultural scientist" lakini your presentation is most unscientific.
 
na takwimu zinaonyesha kwamba pale ambapo Freemasons wapo, hata ajali nazo zinakuwa nyingi sana,na hakika hili tunaliona Tanzania leo.

Takwimu zipi hizo? Labda ushare na sisi kidogo unaweza ukaeleweka.
 
Umeandika ya msingi ... kweli tuanze kustuka na kufungua macho, kabla haya matata...

Kwanza, tumeruhusu 'utamaduni na tabia zetu za msingi' kukandamizwa na "maendeleo" yaingizwayo na waUlaya. Tunaruhusu, tukijua ama bila kujua, kujifunza ama kufundishwa, haya "maendeleo" kiujinga na kiupuuzi. Wengi tunakuwa 'brainwashed' badala ya kuongeza 'brain-power'. Kweli tunahitaji kuamka and kustukia hizi elimu za 'maendeleo' zinavoingizwa. Kipofu ataona vile hii 'elimu' inavofundisha tamaa, uchoyo, afu ugaidi...

Pili, 'freemasons' wana nia moja tu - kutawala dunia. Mkisikiaga maraisi wazungu wa Marekani, wakitamka 'NEW WORLD ORDER' - hawaongelei amani duniani ama izo demokrasia wanazoropoka-ropoka kirahisi. Mbinu za kutawala dunia, wameamua, zitapatikana kwa kuanzisha fujo, ama kutilia chumvi fujoni - kupanda mbegu za fujo, ama kumwagia mbolea nyingi 'mbeguni'. Jihadharini, tujihadharini... kilichoandikwa na 'tikkera' hapa ni cha muhimu sana.

PAMOJAH.
 
Back
Top Bottom