Tanzania ni nchi ya ajabu sana!!! Dah

Tanzania ni nchi ya ajabu sana!!! Dah

belak

Senior Member
Joined
Jul 23, 2016
Posts
179
Reaction score
377
Habari wandugu!
Mwezi uliopita nilikuwa na safari yangu kutoka Johannesburg hadi Nairobi kwa gari kibiashara zaidi! Kutoka South,Botswana,hadi Zambia kila traffic alienisimamisha alipojua ninaenda wapi hakuruhusu nichelewe hata dk moja karibu wote walinitakia sfr njema na kunikumbusha kuzingatia usalama wangu na wa wengine barabarani! Wengine walidiriki hata kuegesha malori yanayokaguliwa pembeni ili tunaoenda mbali tupewe kipaombele!

KITUKO SASA
Sijui ilikuwa bahati nasibu kupita mbeya usiku? Nilipoingia tu Tanzania nchi yangu ya amani nikiwa mafinga asbh sehemu inaitwa kinyanambo nilibambikiziwa kosa eti nimeover speed wakati namonitor speed yangu ni 40 mahali palipotaka 50 kijana huyu askari anatoka povu kutaka hela kwanguvu kwa kosa lisilolangu huku wengine wakinishambulia balaa kama mwizi! Mbaya zaidi walipojua natoka safari ndio usiombee! Nilipoteza saa zima hapo kwa ajenda ya kishetani sana! Mwisho nikalipa faini nikaondoka!
Friends! Kutoka mafinga hadi Dodoma nilisimamishwa njiani Mara 12 kila anaesimamisha anataka hela na anatafuta kosa kama mungu vile!

Nimejiuliza maswali mengi sana kwenye Taifa kama hili! Tabu niliyoipata baada ya kuingia nchini kwangu huwezi amini!

MY TAKE
Kuna tafsiri nyingi sn za amani but ukipewa mamlaka kubwa kama wewe si mwadilifu kama walivyo hawa ndg zetu wengi ni afadhali ukutane na shetani! Nashindwa kuelewa kama traffic mbinguni wapo nitamuuliza Mungu maswali mengi sana! Barabara za kwetu na tunazilipia kodi but tunaendesha magari kama wageni au ndege tunaowindwa what is thissssss!! Nchi hii inatamkiwa laana nyingi sana na watu wake ambazo ni halal ni ngumu sana kufurahia maisha bongo labda uwe askari, mchawi na mtu mwenye roho mbaya sana

Mwisho! Kwakuwa najua serikali haiwezi fanya mabadiliko yoyote ktk hili nimeamua tu kuliweka hili kundi la hawa watesaji kama kundi duni saana na la mwisho kwa umuhimu in my list of group of people in the society.Hii ni kwasababu nimejihakikishia kuwa dhamiri ya traffic wa Tanzania sio usalama na utu bali ni fedha na mapato ya udhalimu yanayokusanywa eti yakalete maendeleo!!!!!
 
Kwani huyu GARI ndo ng'ombe wa mjini,bado tuna mawazo kumiliki GARI ni utajiri kumbe ni hobi tu.
 
Hebu shirikisha kaubongo kdg kufikiri! Gari ni facility au kitendea kazi sio starehe! Unaweza kutoka mbeya hadi dar kwa mguu zama hizi?
 
Kuna member mwingine kaleta mada kama hii, tuendelee tu kugugumia maumivu ya dhuluma. Mungu ni mwema wakati wote.
 
Zambia wapo vizuri unasimamishwa Trafiki akikagua huna kosa anakwambia tuu Safari njema Mzee au tipepampako ya soda chabe uli chee mushi...akimaanisha tupe ya soda tuu gari haina matatizo ukiwa unayo unawapa hauna unatembea tuu bila shida kabisa...Botswana ndio kabisa watakuvizia kwenye speed tuu na reflector kama umebandika sawa na unaambiwa ubandike kabla haujaingia Nchini mwao hakuna kuviziana...Nilichogundua Elimu yetu ni ya hovyo inawafanya wafanyakazi wengi kuwa wajinga bila kutumia akili katika maamuzi yao au shule hawakwenda kabisa...
 
Hebu shirikisha kaubongo kdg kufikiri! Gari ni facility au kitendea kazi sio starehe! Unaweza kutoka mbeya hadi dar kwa mguu zama hizi?
Tuliza ubongo kama ya kusoma, nachomaanisha,kuna baadhi ya wasimamia Sheria wamegeuza gari kwao kama ni chanzo cha mapato,wakiona gari wanafosi hadi makosa ambayo mengine ni onyo tu wao wanataka hela tu.
 
Kuweni wabunifu, nunua kofia ya ccm na scuf ya bendera ya tanzania, hakikisha kwenye collection yako ya music usikose nyimbo za ccm.

hutaombwa ombwa hela kamwe, hii mbinu imenisaidia sana kwa kuwa mimi ni msafiri wa safari ndefu mara kwa mara hapa bongo.
 
Source of income au pesa ya kiwi waliambiwa pia kila kosa la 30000 traffic anakula 5000.
 
Habari wandugu!
Mwezi uliopita nilikuwa na safari yangu kutoka Johannesburg hadi Nairobi kwa gari kibiashara zaidi! Kutoka South,Botswana,hadi Zambia kila traffic alienisimamisha alipojua ninaenda wapi hakuruhusu nichelewe hata dk moja karibu wote walinitakia sfr njema na kunikumbusha kuzingatia usalama wangu na wa wengine barabarani! Wengine walidiriki hata kuegesha malori yanayokaguliwa pembeni ili tunaoenda mbali tupewe kipaombele!
KITUKO SASA
Sijui ilikuwa bahati nasibu kupita mbeya usiku? Nilipoingia tu Tanzania nchi yangu ya amani nikiwa mafinga asbh sehemu inaitwa kinyanambo nilibambikiziwa kosa eti nimeover speed wakati namonitor speed yangu ni 40 mahali palipotaka 50 kijana huyu askari anatoka povu kutaka hela kwanguvu kwa kosa lisilolangu huku wengine wakinishambulia balaa kama mwizi! Mbaya zaidi walipojua natoka safari ndio usiombee! Nilipoteza saa zima hapo kwa ajenda ya kishetani sana! Mwisho nikalipa faini nikaondoka!
Friends! Kutoka mafinga hadi Dodoma nilisimamishwa njiani Mara 12 kila anaesimamisha anataka hela na anatafuta kosa kama mungu vile!
Nimejiuliza maswali mengi sana kwenye Taifa kama hili! Tabu niliyoipata baada ya kuingia nchini kwangu huwezi amini!
MY TAKE
Kuna tafsiri nyingi sn za amani but ukipewa mamlaka kubwa kama wewe si mwadilifu kama walivyo hawa ndg zetu wengi ni afadhali ukutane na shetani! Nashindwa kuelewa kama traffic mbinguni wapo nitamuuliza Mungu maswali mengi sana! Barabara za kwetu na tunazilipia kodi but tunaendesha magari kama wageni au ndege tunaowindwa what is thissssss!! Nchi hii inatamkiwa laana nyingi sana na watu wake ambazo ni halal ni ngumu sana kufurahia maisha bongo labda uwe askari, mchawi na mtu mwenye roho mbaya sana
Mwisho! Kwakuwa najua serikali haiwezi fanya mabadiliko yoyote ktk hili nimeamua tu kuliweka hili kundi la hawa watesaji kama kundi duni saana na la mwisho kwa umuhimu in my list of group of people in the society.Hii ni kwasababu nimejihakikishia kuwa dhamiri ya traffic wa Tanzania sio usalama na utu bali ni fedha na mapato ya udhalimu yanayokusanywa eti yakalete maendeleo!!!!!
Ukija tena joz tutaftane
 
Ki ukweli kama hutaki kero za trafik kwa tanzania, pita usiku ukiona pamekucha paki pembeni lala maana watakugeuza mtaji wajinga hawa.
 
Back
Top Bottom