Tanzania ni nchi pekee inayojali ukarimu na kumuamini mgeni usiefahamiana

ema-ze-boy

Member
Feb 13, 2017
47
47
Asubuhi ya Leo tarehe 16 Feb 2017 Jumatano nilikuwa na shida na ofisi ya serikali ya mtaa wa kwa bwawani kata ya Mwananyamala nikiwa natokea main road ya Bagamoyo nikaanza kupita mitaani kuisaka jengo zilipo serikali za mtaa mtu wa kwanza alikuwa mama wa makomo age ya mamaangu.

Nilipomsalimu nikamuomba anielekeze zilipo ofisi ya serikali ya mtaa alikuwa anafagia akaacha kufagia akasogea barabara ya vumbi kunionyesha njia.

Nikiwa naelekea mbele nikafika cafe flani Mara mvua ikaanza kunyesha nikajikinga mvua pale baadae nikamuuliza mhudumu alikuwa bize anakaanga chapati pale akaacha akaanza kunielekeza kufika serikali ya mtaa nikamshukuru na kuondoka.

Mbele kidogo nikakutana na duka kuna mdada binti hivi nikamuuliza
Kutoka pale lilipo duka aikuwa mbali na zilipo serikali za mtaa yule binti akatoka ndani ya duka kwa mlango wa nyuma hadi niliposimama ng'ambo ya Barabara akanionyesha jengo lenyewe nikamshukuru na kwenda.

TAFAKARI
Kwa wote hawakuwa wananifahamu lakini wamenitendea kwa upendo na heshima kubwa.
Hii haitoshi kusema Tanzania tuu watu wapekee sana kulinganisha na wenzetu.
 
kuna siku nilikua naenda posta nikajikuta nasahu walet kazini yenye nauli kwenye mkoba nilikua na 400 tu na nisingeweza kurudi kazini nikalipa nikamfuata bodabida nkamuomba aniazime elf2 ntamrudishia kesho yake nilimuambia ukweli nkampa na namba ya simu yangu
kweli aliniazima kesho yake nkamrudishia...
 
Tunaweza kulinganisha na kinachotokea msumbiji sasa kwa kuwa treats watanzania ivyo tunavyosikia kupitia media na kipindi cha nyuma yaliyojiri afrika ya kusini kuhusu foreigners
Licha ya msahada was kuwapambania nchi zao ili wajitawale kwa Uhuru
Je wanatulipa sahihi au diplomatic body yetu wawakumbushe kuiheshim na kuwaheshim watanzania wakiwa kwao ???
 
Watanganyika ni watu wakarimu sana ni ngumu hata yule unaemdai kumwambia maneno magumu na makali huku unamwangalia usoni sasa inapotokea mtu anaongea maneno makali tena maneno watakoma,kweli kweli,ngoja,hakuna yanakuwa mengi ktk maongezi yake unajiliuza huyu ni Mtanganyika kweli au ni mwenyeji wa Tanganyika maaana kuna Mtanganyika pure na Mtanganyika mwenye Asili ya Asia,Uarabuni,Ulaya mpaka kuna Watanganyika wenye Asili ya China
 
Huo ndio ukweli.
Watanzania wengi ni wakarimu sana na wanapenda wageni sana na ndio maana hata wakimbizi wanakimbilia sana.
Lakini wale wenye roho mbaya Mungu anawaona
 
Mi nilikodi bodaboda saa 7 usiku kwenda klabu kuwa nitamtolea tgpesa. Mtandao uligoma alinirudisha kwa makubaliano ya kumlipa kesho yake jspokuwa tulikuwa hatujuani. Nilimlipa,. Ujumbe tuheshimu ahadi vingimevyo titapoteza
 
Ukalimu wa Watanzania, umechanganyikana na Uzuzu! Matokeo yake tunapata shida tunapotoka nje, kwa kudhani kila nchi wanaishi Kama Watanzania!
 
Kuna jamaa sikumbuki jina lake aliomba msaada wa kulipiwa kodi kutokana na matatizo, alichangiwa hela hapa Jamiiforums akajenga nyumba
 
Kuna ambao huwa hawapendi kulisikia hili ila inabidi tu walielewe...“umoja huu na ukarimu huu umejengwa imara na muasisi wa taifa letu hayati Mwl Julius Nyerere ”,kama umewahi kutembea tena sio mbali hapo jirani tu Kenya utajua ninachomaanisha,jamaa hawana muda wakumsikiliza mtu hata kama umegongwa na gari upo chini unakata roho wanakuacha wanasema sio kazi yao ni kazi ya polisi sio hapa mtu humjui hujui kama huko unakoenda utaambiwa wewe ndiye uliyemgonga unampakia kwenye gari yako anachafua seat na damu huu ni ubinadamu wa ajabu ambao wenzetu wanajaribu kuuiga wanashindwa.
 
Wageni wengine wanauchukulia ukarimu huo kama ujinga flani.
Nathubutu kuuita ukarimu uliopitiliza kuwa ni uzuzu, hayo ndio yaliotufikisha hapa tulipo kwa kuichelewesha nchi yetu kupiga hatua za kimaendeleo kwa kujitoa kusaidia mataifa mengine yajikomboe, km vile msumbiji na afrika ya kusini, baada ya hapo raia wa tanzania wanatanga na kunyanyasika na mataifa hayo hayo, na yote waliyo tendewa katika harakati za kuwakomboa hakuna hata anayo yakumbuka, hata viongozi wao hawajali utu wa watanzania katika mataifa yao, inauma sana wanyo fanyiwa watanzania nchini msumbiji.
 
Ni sahii kabisa, mfano mzuri nauona hapa kazini kwangu, nina co-workers wengi kutoka nchi jirani ya Kenya, lakini kila anaekuja lazima atasifia sana especially ukarimu wanaoupata, mitaani wanavyopendwa. Mpaka sasa kamekuwa ka utamaduni akina kijana single lazima aoe huku!!!! Wengi wanasema wanataka kukaa Tz coz kumetulia..!!!
 
Mi nilikodi bodaboda saa 7 usiku kwenda klabu kuwa nitamtolea tgpesa. Mtandao uligoma alinirudisha kwa makubaliano ya kumlipa kesho yake jspokuwa tulikuwa hatujuani. Nilimlipa,. Ujumbe tuheshimu ahadi vingimevyo titapoteza
Hakuna kitu kizuri kama uaminifu!!!!
 
Back
Top Bottom