Tanzania ni Mali ya nani?

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
Katika moja ya miswada iliyopelekwa Bungeni na Wabunge kwa umoja wao kutoipitisha ni ule unaohusu "KUPUNGUZA USHURU BIDHAA YA MAJI"

Wabunge waliipinga kwani haina manufaa kwa mlaji badala yake inamnufaisha mwekezaji.

Baada ya kitendo cha Bunge kuukataa muswada huu; Sasa maji ya kunywa ya chupa yamepanda bei kwa Sh. 300/= hadi 500/= hii imefanywa makusudi baada ya Bunge kukataa kupitishwa muswada wao.

Mfumuko wa bei ni ugonjwa unaoinyemelea nchi yetu pasipo kuchukuliwa hatua muhimu za kupambana nao. Kila siku hali inakuwa heri ya Jana. Tumeshuhudia katika kipindi cha miaka 7 iliyopita hali inazidi kubadilika siku kwa siku.

Bidhaa muhimu hasa Chakula na nguo vinapanda bei kila siku, bidhaa ya mafuta (Nishati) ndiyo haipimimiki.

Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Mwananchi katika baadhi ya masoko hasa DSm umegundua yafuatayo:-

"Ili kupata mchicha wa kula watu wanne sasa zinahitajika Sh5,000 badala ya Sh2,000 za Juni mwaka jana", anasema Hussein Juma anayemiliki genge eneo la Manzese.

Anasema uhalisia huo unafuatia bei halali za sasa ambapo fungu la mashina matano ya mchicha, au matembele ni Sh200, mashina matatu ya Spinachi sasa ni Sh200 badala yakuwa Sh100 ya kila fungu.

Kwa hali hiyo ili kununua mchicha wa kutosha watu wanne lazima awe na Sh5,000 ili aweze kununua vitunguu, nyanya na mafuta mbali ya mkaa ambao sasa fungu moja ni Sh1,200.

Bei ya kilo moja ya mchele mzuri hapa ni kati ya Sh2,300 -1,900 mchele kawaida unauzwa kwa bei ya Sh1,800-Sh1,700'' anasema mfanyabiashara wa eneo la Segerea.

Kauli hiyo inaungwa mkono na Bakari Chongera anayemiliki duka la la vyakula kwa bei ya jumla na rejareja.

Chongera anasema bei ya mchele haishikiki katika masoko yote tofauti na bei ya maharage ambayo alisema imeanza kuporomoka baada ya wakulima wa mkoa wa Kagera kuingiza sokoni mazao hayo.

Maharage sasa yanauzwa Sh1,800 kwa kilo badala ya Sh2,000 ingawa ni machafu.

Hata hivyo, bei ya sembe inaonekana kubaki ile ile ya mwaka jana ya Sh800 kwa kilo, jambo lililotajwa kuwa ni faraja na kwamba sababu kubwa ni hatua ya Serikali kuruhusu mahindi kutoka Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa yauzwe kwa bei ndogo.

Uchunguzi wa bei ya nyama uligundua kuuzwa kwa Sh6,000 wakati maini ni Sh8,000 kwa kilo. Bei ya kuku wa kienyeji ni kati ya Sh12,000 na Sh20,000.

Bei ya dagaa wa Kigoma wenye uzito wa gramu 50 ni Sh1,000 badala ya Sh500 za mwaka jana.

Mfanyabiashara wa vyakula kwenye magenge ya Segerea, Moses Severino anasema bei ya vyakula imekuwa kubwa kutokana na ukimya wa Serikali.

Je, nini hatma ya Mtanzania Mlalahoi?

Je; kiwango cha kipato kinaendana na matumizi ya Mtanzania?

Je, nini kifanyike kudhitibi mfumko wa bei?

Je, ni nani mmiliki wa Serikali ya Tanzania?

Natoa hoja:

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Katika moja ya miswada iliyopelekwa Bungeni na Wabunge kwa umoja wao kutoipitisha ni ule unaohusu "KUPUNGUZA USHURU BIDHAA YA MAJI"

Wabunge waliipinga kwani haina manufaa kwa mlaji badala yake inamnufaisha mwekezaji.

Baada ya kitendo cha Bunge kuukataa muswada huu; Sasa maji ya kunywa ya chupa yamepanda bei kwa Sh. 300/= hadi 500/= hii imefanywa makusudi baada ya Bunge kukataa kupitishwa muswada wao.

Mimi binafsi nimepatwa na kigugumizi katika hili KILA NIKITAFAKARI NASHINDWA KUPATA JIBU NDIO MAANA NIKAONA NILETE HAPA mnisaidie kwani hili soko huria sasa linawanufaisha wachache na kutuweka pabaya walalahoi.
Sasa hivi kila kitu bei juu, na Serikali bado ipo kimya kama kawaida haijatoa tamko lolote. Mfano kuongezeka kwa bei ya maji ni katika kuishinikiza Serikali ipunguze kodi jinsi wanavyotaka wao.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Wakuu,
Tunapoendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mambo ya kitaifa yaliyoko mbele yetu, hususan mchakato wa kuandikwa kwa katika mpya, naomba kuuliza swali. Nahisi pamoja na mambo mengine, katiba mpya itatakiwa kuwa na ibara inayolitaja taifa letu Tanzania. Katika kufikiria hayo nimepata swali ambalo pengine laweza kuonekana jepesi lakini kumbe gumu. Hivi; Tanzania ni mali ya nani? Naomba mtazamo wenu kisha tujadiliane
 
ni nchi ya mafisadi na familia zao!!!!
 
Kama ni mali ya waTZ, imekuwaje sio wanufaika wakuu wa maliasili ya tanzania yenyewe; au inakuwaje njia kuu za uchumi wa nchi hii zinamilikiwa na watu wasio waTZ; na je, katiba mpya itaweza kubadili chochote hapo?
Aidha, kama ni mali ya waTZ wameipata wapi?
 
Kama ni mali ya waTZ, imekuwaje sio wanufaika wakuu wa maliasili ya tanzania yenyewe; au inakuwaje njia kuu za uchumi wa nchi hii zinamilikiwa na watu wasio waTZ; na je, katiba mpya itaweza kubadili chochote hapo?

Kwa hiyo mkuu unataka kusema kwamba Tanzania ilikuwa mali ya Watanzania kati ya mwaka 1967 hadi mwaka 1992. Yaani wakati wa utekelezaji wa Azimio la Arusha ambapo njia kuu za uchjmi zilikuwa zinamilikiwa na Watanzania wenyewe.
 
Watanzania hawajawahi kumiliki njia kuu za uchumi, enzi unazozisema njia hizo zilimilikiwa na dola, kwa kisingizio cha kwamba ni mali ya umma. Ndio maana uliibuka msemo kwamba 'mali ya umma haiumi'. yaani kwa kuwa watanzania walikuwa si wamiliki wa uchumi, hawakuwa na uchungu na hicho kilichoitwa mali ya umma.
 
Back
Top Bottom