James Hungury
JF-Expert Member
- Jun 8, 2013
- 825
- 612
Nawasalimu,
Shame on us!
Hakuna lolote,
Kila mahali ni ovyo ovyo tu, tangu tumepata uhuru kila siku tunadanganywa nchi imepiga hatua, hatua gani? Za kobe au? Nchi yenye resource zote, lakini hakuna maendeleo ya maana yaliyopo, hadaa za kupewa pipi tamu za mda,
Eti barabara, eti mwendo kasi, wapi nyie, mmetufanya watoto wadogo kila siku,
Mmeshindwa kufanya lolote la maana.
Nchi inakila kitu hakuna lolote mlichokifanya nyie CCM, nasema uwazi hakuna lolote, nchi hii inamapungufu mengi sana, tena bora hata wakoloni walivyokuwepo, leo matatizo yamezidi zaidi, wachache wanafaidi kwa kodi za wengi, ukoo wa serikali ndo unakula matunda.
Kwako wewe kapuku utatafuta kwa jasho lako,uza mitumba,pipi,karanga,upate ajira vyote ni shida tupu kwakuwa mazingira yatakuwa yaleyale,utakatwa kodi za kutosha za kulisha ukoo wa serikali.
Wale wajinga wajinga ambao nao wamedumazwa na limbwata la chama CCM, basi utawasikia wakusema CCM amefanya mambo makubwa, ukimuuliza mambo gani anakwambia, huoni amani, huoni barabara, huoni mwendo kasi,! Ha ha ha ha limbwata baya sana.
Hivi unajua tangu uhuru, je wajua kama tunajivunia maendeleo ya awamu mmoja? Hiyo miaka mingine walikuwa wanafanya nini? Hebu waangalie wale wenye ukoo wa serikal, matumbo hayo.
Kila mmoja anachota resources zetu kama alizitengeneza yeye, wako kwenye mgao wa uji. Nchi hii imelogwa na nani?Watanzania tumepewa limbwata baya sana,penye ubaya sisi twapaona safi.
Nchi ina masikini wengi hatari, maisha yakusononesha, ajira za shida, vijana hawana ramani, unasema wafanye kazi, kazi gani? Waje uwaajiri nyumbani kwako au? Shame on you.
Tunapitwa hata na nchi jirani ndogo tu,! Aibu hii tuipeleke wapi?
Leo ukitaka ufanikiwe uwe mtoto wa kigogo, au uwe kwenye ukoo wa serikali, vinginevyo sahau kupata hata ukatibu, lakini walio kwenye system utasikia, ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani, mara ameteuliwa kuwa mbunge viti maalumu, fuatilia historia utakuta yuko kwenye kale kaukoo ka serikali. Shame on you!
Nb: Tusidanganyane lolote, mwongo mmoja wa rais hauwezi badilisha wala maliza matatizo ya miongo yote.
Mh. Majipu, majipu! Lol, juhudi njema lakini nakusalimu.
Nawasilisha