Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,387
- 38,663
Kuna zama hadi kwenye hati za kusafiria (Passport) za Tanzania kuna baadhi ya nchi "adui" ziliwekwa kwamba mtanzania haruhusiwi kwenda huko. Ukiangalia nchi nyingi tu duniani marafiki na maadui wa nchi hizo wanafahamika. Kama nchi lazima kuwe na muongozo wa kinchi ni nani ni rafiki na ni nani ni adui.
Mwalimu na wenzake walipoanzisha (Non Alignment Movoment-NAM) hoja ya kutofungamana na upande wowote ilijengwa katika msingi ya kutochaguliwa nani awe rafiki au nani awe adui, si katika misingi ya kufungamana na nchi yoyote ile bila ya nchi hiyo tunayofungamana nayo kukidhi vigezo vinavyotakiwa ili kuwa na urafiki na Tanzania.
Wakati wa vita vya "Biafra" Tanzania iliwaunga mkono watu wa kabila la Igbo waliotaka kujitenga na Nigeria bila ya kujali "marafiki" wengine wa Tanzania walikuwa wanaunga mkono upande upi katika vita ile. Ndivyo baadaye yalipokuja masuala ya Ukombozi wa Southern Rhodesia (Zimbabwe) na hata Afrika ya kusini, msimamo wa Tanzania inamuunga nani mkono ulijulikana na kila mtu.
Hivi nchi yetu kwa sasa kwenye sera za siasa za nje rafiki wa Tanzania ni yupi na adui ni yupi? Jee kwa sasa Tanzania nchi zote za dunia hii ni marafiki zetu ama ni maadui zetu? Urafiki si ujirani wa kijografia Maana hata Kenya waliwahi kuitwa "manyang'au" zama zile baada ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuvunjika.
Rafiki yetu ni nani na adui yetu ni nani?