RingaRinga
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,043
- 513
Tanzania ni kati ya nchi nne ambazo Serikali ya China imeahidi kufanya ‘kufuru’ ya uwekezaji wa viwanda.
=======
Dar es Salaam. Tanzania ni kati ya nchi nne ambazo Serikali ya China imeahidi kufanya ‘kufuru’ ya uwekezaji wa viwanda.
Hayo yamebainika kwenye kongamano la wachumi na wadau wa biashara kati ya China na Tanzania, Kenya na Afrika Kusini ambalo lilijadili fursa na changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ambaye alikuwa anafungua kongamano hilo, amesema uamuzi wa kuiteua Tanzania ulifanywa kwenye mkutano uliofanyika mapema mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Amesema katika mkutano huo ambao Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, China iliamua kushirikiana na nchi za Afrika Kusini, Kenya na Tanzania kujenga uchumi wa viwanda.
Chanzo: Mwananchi