mazaga one
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 2,463
- 3,932
- Thread starter
- #21
Mkuu umekosa hoja ya msingi mimi hujanijibu majibu yangu kwa usahihi,hii ni ishara ya kuwa kuna HAPANA kubwa kwa unachokifiria kichwani mwako.Jipangeee Mkuu
- Toka mfumo wa vyama vingi tume hii haijawahi kuwa huru. Na madai ya tume huru hayajaanza jana. Chaguzi zote hizo hazijawahi kuwa huru. Watu kushiriki sio kwamba wanakubaliana na kinachoendelea.
- Machafuko yamewahi kutokea zaidi ya mara moja, huenda hujui kuwa nchi hii iliwahi kupata wakimbizi. Nadhani haya yalipokuwa yakitokea ulikuwa bado unasoma. Sio mara moja au mbili wapinzani wamekuwa wakitangazwa kwa kutumia nguvu baada ya tume kutaka kuchakachua matokeo halali.
- Bunge letu lina wabunge wa upinzani, na hawa walitangazwa wakati wa JK, demokrasia ikiwa na unafuu kwa mbali. Toka ameingia Magufuli madarakani, kile kilio cha tume kutokuwa huru na ushahidi wa wazi kuwa tume haiko huru umedhihirika. Magufuli anasema kuwa uchaguzi utakuwa huru, yeye ndio anayeongoza kwa kunajisi chaguzi za nchi hii, na hakuna mtu anayemuamini, labda wanaccm na vyama mapandikizi kwani ndio wanaofaidika na mfumo huu mbovu wa tume na uchaguzi wenyewe.