Tanzania nchi yangu, mazuri na mabaya ni yetu, Serikali ya awamu ya tano ni yetu!

mazaga one

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
2,463
3,932
Serikali yetu pendwa ya chama cha Mapinduzi ni serikali sikivu na inayojali watanzania kwa kufanya mambo mengi mazuri na ikiwa sikivu pia kwa wananchi wake.Hivi mliopo humu Jf ni watanzania kama nilivyo mimi au ninyi wenzangu baadhi yenu mnaishi ulaya?

Nianze na haya yafuatayo!

1.Kuna mtu alileta maada ya watu kulalamika gharama za kuwekwa karantini kuwa kubwa watu wakashauri zichaguliwe hostel na serikali yetu ilivyo sikivu imelifanyia kazi lakini bado unakuta comments za watu humu nalo wanalipinga hivi ni kwanini? Ilhali mjadala wa mwanzo watu walionekana kuwatetea hao wa karantini na gharama kuwa kubwa.Sasa serikali imefanya lakini bado midomo humu inaendelea shida ni nini?

2.Kila nchi ina namna take ya kupigana na kuchukua tahadhali za majanga,sasa inakuaje humu ndani hasa wanasiasa uchwara wanalazimisha mawazo yao ya usingizi et serikali iyafwate.Hivi kweli ninyi kwa kuwa familia zenu zinasoma shule nzuri,chakula bora cha uhakika mnataka watoto wa mkulima kama mimi nipate shida baadae muanze kusema serikali hamna kitu? Nasema Noo Kubwa.Big up Mh.Makonda kwa kuhamasisha Watanzania wanawaotishwa na wanasiasa uchwara piga kazi Mh.

Mimi kama kijana wa Chama navutika na wewe unavyofanya i wish siku nije Dsm nikupongeze Mh.Makonda Jembe letu.

3.Ni kwa nini vyama vya upinzani yani tatizo la Corona hili yani badala ya kutanguliza maslahi mapana ya taifa letu mbele ninyi mmekuwa watu wa kupotosha na kutafuta kiki ya kisiasa,hii ni ishara ya ninyi kuwa watu wa kupenda madaraka au kuwasaidia watanzania?

4.Hivi ni kinashindikana nini kama Watanzania wenzangu mliopo humu mkawa watu wa kushauri kuliko kuandika vitu vya Kongo na uzushi humu au kwenye mitandao mingine kwa ajili ya kuishauri serikali yetu na kujivunia maendeleo yetu tuliyopiga kupitia serikali ya awamu ya tano.

5.Corona ipo ndugu zangu naombeni tusimame kidete sote kwa pamoja na tuendelee kuchukua tahadhari muda wa uchaguzi bado wapinzani msitafute kiki wakati wa matatizo,muda bado wa kampeni,acheni upotoshaji kwa jamii jamani.Mh Rais ashasema uchaguzi upo kama kawaida.

mazagaone@gmail.com
 
Uwe uzushi au ukweli vipo vya kujifunza.Jiulize wenzetu walioendelea kwann wameruhusu Uhuru wa habari ikiwemo ukosoaji sababu ni matured na civilized viongozi wao uwaza makubwa na sio madogo mfano kupambana na upinzani au Wakosoaji wao uwatumia Wakosoaji positively kama source ya jinsi gani ya kuboresha zaidi maslai ya wananchi thus wao awafail sababu kupitia maoni ya watu upata kitu.Huwatumia Wakosoaji kama kioo cha kujitazama wasianguke maana kioo cha MTU ni watu.

Ili ujishape itazame jamii yasema nn kuhusu wwe,ili uwe mchezaji bora wasikilize watazamaji wao wako nje wanayaona makosa yako usiyoweza yaona hadi ukiwa nje ukawekewa replay.

Jiulize kwann watawala wa kiafrica huwa na akili wakishatoka nje ya madaraka ni kwa sababu huwa wanayaona Yale Yale makosa yao waliyokuwa wakiambiwa wakiwa madarakani.

Si ajabu Leo kusikia viongozi wastaafu wakitamani katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.Hata ukisikikiza speech zote za Mwalimu zinaponda madhaifu yake aliyofanya akiwa madarakani.
 
Uwe uzushi au ukweli vipo vya kujifunza.Jiulize wenzetu walioendelea kwann wameruhusu Uhuru wa habari ikiwemo ukosoaji sababu ni matured na civilized viongozi wao uwaza makubwa na sio madogo mfano kupambana na upinzani au Wakosoaji wao uwatumia Wakosoaji positively kama source ya jinsi gani ya kuboresha zaidi maslai ya wananchi thus wao awafail sababu kupitia maoni ya watu upata kitu.Huwatumia Wakosoaji kama kioo cha kujitazama wasianguke maana kioo cha MTU ni watu.Ili ujishape itazame jamii yasema nn kuhusu wwe,ili uwe mchezaji bora wasikilize watazamaji wao wako nje wanayaona makosa yako usiyoweza yaona hadi ukiwa nje ukawekewa replay.Jiulize kwann watawala wa kiafrica huwa na akili wakishatoka nje ya madaraka ni kwa sababu huwa wanayaona Yale Yale makosa yao waliyokuwa wakiambiwa wakiwa madarakani. Si ajabu Leo kusikia viongozi wastaafu wakitamani katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.Hata ukisikikiza speech zote za Mwalimu zinaponda madhaifu yake aliyofanya akiwa madarakani.
Unataka kushauri nini? Maana mbona viongozi wetu wote ni wasikivu.
 
Nijenge hoja gani, nimekuambia wangekuwa wasikivu tungekuwa na tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, unasema naropoka maana sijui ninaloongea. Ulitaka nijenge hoja gani we mwendawazimu?
Mimi nadhani unaropoka vitu usivyovijua,tume huru si ilishasemwa uchaguzi utakuwa huru na haki,pia swala la katiba si liko wazi kwa sasa wananchi wanahitaji maendeleo hilo litakuja tu
 
Narudia tena, tume hii haiko huru, na hao wanaosema itakuwa huru hatuwaamini. Tunataka muundo wa kuifanya tume iwe huru, na sio kutuambia iko huru wakati tunaona fika haiko huru. Katiba mpya iko pending kwa hatua ya kura, hakuna popote panapoonyesha tukipata katiba mpya hakutakuwa na maendeleo, labda unithibitishie katiba mpya inazuia vipi maendeleo. Unaposema katiba itakuja tu unaamaanisha nini, na ni kipi kinachofanya isiwepo sasa? Halafu kwa Utetezi huu wa kijinga ndio unasema naropoka? Pumbavu kabisa.
 
Wangekuwa wasikivu hivi leo tungekuwa na tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, tena ile ya maoni ya wananchi na sio hiyo version ya ccm iliyochakachuliwa.
Kwani katiba mpya na tume huru inaletwa na viongozi?
 
Narudia tena, tume hii haiko huru, na hao wanaosema itakuwa huru hatuwaamini. Tunataka muundo wa kuifanya tume iwe huru, na sio kutuambia iko huru wakati tunaona fika haiko huru. Katiba mpya iko pending kwa hatua ya kura, hakuna popote panapoonyesha tukipata katiba mpya hakutakuwa na maendeleo, labda unithibitishie katiba mpya inazuia vipi maendeleo. Unaposema katiba itakuja tu unaamaanisha nini, na ni kipi kinachofanya isiwepo sasa? Halafu kwa Utetezi huu wa kijinga ndio unasema naropoka? Pumbavu kabisa.
Asante naona CDM washakupa bando na simu basi unajifanya kutetea unachokiamini,Naomba unijibu maswali haya
1.Ni lini uchaguzi wetu haujawahi kuwa huru?
2.Ni lini nchi yetu ilishawahi kutokea fujo baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa?
3.Bunge letu lina wabunge wa upinzani pia na walipata viti vingi sana mwaka 2015,Je hao walipitia kupitia tume IPI?????
 
Serikali yetu pendwa ya chama cha Mapinduzi ni serikali sikivu na inayojali watanzania kwa kufanya mambo mengi mazuri na ikiwa sikivu pia kwa wananchi wake.Hivi mliopo humu Jf ni watanzania kama nilivyo mimi au ninyi wenzangu baadhi yenu mnaishi ulaya?

Nianze na haya yafuatayo!

1.Kuna mtu alileta maada ya watu kulalamika gharama za kuwekwa karantini kuwa kubwa watu wakashauri zichaguliwe hostel na serikali yetu ilivyo sikivu imelifanyia kazi lakini bado unakuta comments za watu humu nalo wanalipinga hivi ni kwanini? Ilhali mjadala wa mwanzo watu walionekana kuwatetea hao wa karantini na gharama kuwa kubwa.Sasa serikali imefanya lakini bado midomo humu inaendelea shida ni nini?

2.Kila nchi ina namna take ya kupigana na kuchukua tahadhali za majanga,sasa inakuaje humu ndani hasa wanasiasa uchwara wanalazimisha mawazo yao ya usingizi et serikali iyafwate.Hivi kweli ninyi kwa kuwa familia zenu zinasoma shule nzuri,chakula bora cha uhakika mnataka watoto wa mkulima kama mimi nipate shida baadae muanze kusema serikali hamna kitu? Nasema Noo Kubwa.Big up Mh.Makonda kwa kuhamasisha Watanzania wanawaotishwa na wanasiasa uchwara piga kazi Mh.

Mimi kama kijana wa Chama navutika na wewe unavyofanya i wish siku nije Dsm nikupongeze Mh.Makonda Jembe letu.

3.Ni kwa nini vyama vya upinzani yani tatizo la Corona hili yani badala ya kutanguliza maslahi mapana ya taifa letu mbele ninyi mmekuwa watu wa kupotosha na kutafuta kiki ya kisiasa,hii ni ishara ya ninyi kuwa watu wa kupenda madaraka au kuwasaidia watanzania?

4.Hivi ni kinashindikana nini kama Watanzania wenzangu mliopo humu mkawa watu wa kushauri kuliko kuandika vitu vya Kongo na uzushi humu au kwenye mitandao mingine kwa ajili ya kuishauri serikali yetu na kujivunia maendeleo yetu tuliyopiga kupitia serikali ya awamu ya tano.

5.Corona ipo ndugu zangu naombeni tusimame kidete sote kwa pamoja na tuendelee kuchukua tahadhari muda wa uchaguzi bado wapinzani msitafute kiki wakati wa matatizo,muda bado wa kampeni,acheni upotoshaji kwa jamii jamani.Mh Rais ashasema uchaguzi upo kama kawaida.

mazagaone@gmail.com
Jibu hatuna umoja wa kitaifa. Swali fikirishi ninani chanzo cha kutokuwa na umoja wa kitaifa
 
Asante naona CDM washakupa bando na simu basi unajifanya kutetea unachokiamini,Naomba unijibu maswali haya
1.Ni lini uchaguzi wetu haujawahi kuwa huru?
2.Ni lini nchi yetu ilishawahi kutokea fujo baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa?
3.Bunge letu lina wabunge wa upinzani pia na walipata viti vingi sana mwaka 2015,Je hao walipitia kupitia tume IPI?????

  1. Toka mfumo wa vyama vingi tume hii haijawahi kuwa huru. Na madai ya tume huru hayajaanza jana. Chaguzi zote hizo hazijawahi kuwa huru. Watu kushiriki sio kwamba wanakubaliana na kinachoendelea.
  2. Machafuko yamewahi kutokea zaidi ya mara moja, huenda hujui kuwa nchi hii iliwahi kupata wakimbizi. Nadhani haya yalipokuwa yakitokea ulikuwa bado unasoma. Sio mara moja au mbili wapinzani wamekuwa wakitangazwa kwa kutumia nguvu baada ya tume kutaka kuchakachua matokeo halali.
  3. Bunge letu lina wabunge wa upinzani, na hawa walitangazwa wakati wa JK, demokrasia ikiwa na unafuu kwa mbali. Toka ameingia Magufuli madarakani, kile kilio cha tume kutokuwa huru na ushahidi wa wazi kuwa tume haiko huru umedhihirika. Magufuli anasema kuwa uchaguzi utakuwa huru, yeye ndio anayeongoza kwa kunajisi chaguzi za nchi hii, na hakuna mtu anayemuamini, labda wanaccm na vyama mapandikizi kwani ndio wanaofaidika na mfumo huu mbovu wa tume na uchaguzi wenyewe.
 
Back
Top Bottom