Tanzania nchi ya ulabu, sio vitabu

Tanzania nchi ya ulabu, sio vitabu

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,031
Reaction score
168,654
HATIMA YA VITABU VYA Prof. Joseph Mbele
Anaandika....
Vitabu vyangu vimeanza kuniumiza kichwa. Hapa naleta picha za baadhi, ambavyo vimo ofisini mwangu. Vingine viko nyumbani. Jumla ni kama vitabu elfu tatu. Ninawazia hatima ya vitabu hivi nitakapostaafu na kurejea Tanzania, kwani nilikuwa hapa kwa majukumu fulani, lakini si kuishi moja kwa moja.
Tangu baada ya kuja hapa ughaibuni, wakati orodha ya vitabu hivi ikiwa inaongezeka, nilikuwa nawazia kuvisafirisha Tanzania, ambako ninavyo vingine vingi. Nilikuwa nawazia kuanzisha maktaba. Lakini ninajiuliza itakuwa na faida gani katika nchi ambayo utamaduni wa kusoma vitabu ni haba kama maji jangwani.
Ninapofikiria hivyo, ninashawishika kuviuza hapa hapa Marekani. Kuuza vitabu binafsi ni utamaduni wa kawaida hapa Marekani. Nimepiga hesabu nikaona kuwa hata kwa punguzo kubwa la bei, sitakosa kupata dola 10,000, ambazo ni zaidi ya milioni ishirini za madafu. Hela hizo nikienda nazo Tanzania nitaweza kufungua baa ya nguvu, kwani Tanzania ni nchi ya ulabu, si vitabu.
Uzuri wa Tanzania ni kuwa siku ya kufungua baa, unaweza kumpata hata waziri kuwa mgeni rasmi, na shughuli ikafana sana. Lakini ufungue maktaba, utakuwa mtu wa bahati sana ukimpata katibu kata kuwa mgeni rasmi. Kwa hivyo, kwa sasa, naegemea zaidi upande wa kwenda kufungua baa
...swali langu.
Tufanyaje kurudisha utamaduni WA kusoma?
27331741_10155616185114051_49711546884344964_n.jpg
 
hahaaa nimecheka
daahhh kwamba ukifungua bar waweza kumpa invitation hata waziri kisha akaja ...daahh
kuna wale waarabu wlikwenda ikulu kupeleka msaada wa vyerehani 50 na waziri mkuu akavipokea hhaaahaaa na pictr zikapigwa. ..eti walikuwa wana saport kauli mbiu ya Tanzania ya viwounder ..daahhh


TANZANIA EEEHHH NCHI YANGU WEEEE..
MUNGU TUNU SURU KAMA TAIFA WALLAH
 
hahaaa nimecheka
daahhh kwamba ukifungua bar waweza kumpa invitation hata waziri kisha akaja ...daahh
kuna wale waarabu wlikwenda ikulu kupeleka msaada wa vyerehani 50 na waziri mkuu akavipokea hhaaahaaa na pictr zikapigwa. ..eti walikuwa wana saport kauli mbiu ya Tanzania ya viwounder ..daahhh


TANZANIA EEEHHH NCHI YANGU WEEEE..
MUNGU TUNU SURU KAMA TAIFA WALLAH
Jiulize ni watanzania wangapi wanaweza kukaa na kitabu masaa mawili wanasoma!!
 
Back
Top Bottom