Tanzania na Upinzani Kanjanja

Tanzania na Upinzani Kanjanja

CHADEMA IMEKWAMA INAHITAJI AKILI KUBWA KUWANASUA. ACHENI MAANDIKO YATIMIE.

Na Thadei Ole Mushi.

Kwa wale wakristo wenzangu watakuwa wanamfahamu sana Mtume Paulo na barua zake ambazo zinaitwa WARAKA alizowaandikia Waefeso na Wafilipi.

Ulishawahi kujiuliza kwa nini Pulo alitumia njia hiyo kuwasiliana na Waefeso au Wafilipi? Kwa nn aliwaandikia barua? Kwa nn yale aliyoyataka kuwaeleza hakuwaeleza moja kwa moja bila kutumia barua??? Jibu ni moja tu kuwa Mazingira aliyokuwepo hakuwa na fursa ya kufanya hivyo. Ikumbukwe kuwa wakati Paulo anaandika barua hizi kwa wapendwa wake Wafilipi na Waefeso alikuwa akisubiri hukumu ya Kaisari mfalme wa ROMA kipindi hicho yaani alikuwa amefungwa.

Paulo alifanikiwa kupenyeza ujumbe wake kwa wapendwa wake kupitia kwa rafiki yake Timoteo ambaye yeye alikuwa amefungwa ila baadaye aliaachiliwa na kuwa huru. Kitendo cha Timoteo kwenda mara kwa mara kumtembelea rafiki yake Paulo gerezani kilimpa fursa Paulo kuwaandikia ujumbe wa wokovu wapendwa wake hawa.

Ninaposoma maandiko haya na hadithi hizi za kina Paulo zinanifanya niwakumbuke watu watatu waliokuwa chadema Mwigamba, Kitila na Zitto. Nakumbuka ule waraka walioundika wakiwa kifungoni kifungo cha uminyaji wa Demokrasia na kutumia media kuusambaza kama Paulo alivyomtumia Timoteo. Leo wanachadema wamegeuka wayahudi hawasikii la kuambiwa yale yote yaliyotabiriwa na manabii hawa yanatokea kwa sasa.

Kama waraka ule ulivyosema kuwa CHADEMA imekosa hoja za msingi za kusimamia na sasa wanasubiria tu CCM iwatengenezee matukio ili wapate cha kuongea nanukuu kutoka kwenye waraka wenyewe :-

“Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.”

Kauli ya kinabii kwa kina mwigamba na kitila inaanza kujidhihirisha hapa kwani leo hii chadema uhai wake unategemea Hotuba za Magufuli. Magufuli asipohutubia taifa kwa mwezi mzima na Ukawa nao watakosa cha kuzungumza mwezi mzima.

Kama mtakumbuka Kipindi cha kampeni chadema ilisema CCM wamekosea kumteua Magufuli kwa kuwa si mwanasiasa na hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa ccm wa Tawi.

Kwangu hii ilikuwa ni projection nzuri kabisa walifanya ila hawakuandaa miundombinu ya ku deal naye kama akishinda. Wao wanataka mtu ambaye si mwanasiasa afanye siasa hii mbinu wakiendelea kuitumia kwa style Hii ya Mh Magufuli Ukawa watapotea kabisa.

Huwezi kufukuza kina slaa, zitto, kitila na Mwigamba halafu utegemee akili za kina Sugu na Lema wa Arusha. Chadema inapaswa ijifanyie tathmini yenyewe wajaribu kuweka opinion poll waangalie wamepoteza wapenzi wangapi. Na hili ni gap kwa watu wa research kutuambia kama uchaguzi ungefanyika leo nani angeshinda.

[HASHTAG]#KINACHOTOKEA[/HASHTAG] KWA SASA AMBACHO HAKIONEKANI.

1. Vyombo vya habari ikiwa ni magazeti, television na radio zimepunguza kwa asilimia 70 kuripoti habari zinazohudu Chadema ikilinganishwa na kipindi cha January 2014 -October 2015.

2. Mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na social media zote na vijiweni vijana wa Chadema kwa aslimia 90 wamekosa hoja na wanatukana matusi makubwa sana. Kama Malisa au Yericko hataandika kitu kupinga yanayofanywa na CCM basi watabaki kutukana hata kwa mambo ya msingi. Unapokosa vijana ambao wanaweza kujenga hoja kwenye hizi social media ni umeruhusu watu kupenyeza propaganda.

3. Uungwaji mkono toka makundi mengine nao umepungua. Makundi haya ni yale ya taasisi za kidini kama wachungaji, Mashekhe, na taasisi za elimu ya juu.

Makundi haya kila moja yameonekana kuunga mkono juhudi za serikali ya CCM kuliko maigizo ya Chadema.

4. Wanaoondoka Chadema ni wale wenye akili tu wanawaacha hawa vijana wanaotukana, vijana ambao hawana uwezo wa kutoa hata mkakati mmoja wa kukisaidia chama hii ni hatari kubwa sana kwa uhai wa Chama.

5. Kitendo cha Chadema kuanza kujiondoa kwenye chaguzi ni kiashiria tosha kuwa kinaanza kupoteza Uhai.

Kwa akili hizi za Kina Lema za kuota ndoto na kufanya mazishi ya mbwa kitaifa kazi mnayo sana.

Ole Mushi
 
Niliwahi kuwakubali sana hao wapinzani huko nyuma. Ila kwa sasa nimekata tamaa kabisa. Hawaeleweki kabisa hojazao zinataka nini. Wakishauliwa wanatoa matusi. Sijui wamepatwa na nini hawa jamaa.
 
Wale mnaoona upinzani uchwara kama ninyi ni watanzania kwa nini msianzishe huo upinzani imara?Kama ninyi mnaogopa tu hata kuanzisha vyama "imara" vya upinzani mnapataje nguvu ya kukosoa hawa wenzetu waliojitahidi hadi kuilazimisha CCM kucheza muziki isioupenda?
Kama ninyi mnaoukosoa upinzani mpo huko huko upinzani mf.akina Cheyo na Lipumba,ni wazi mmekuwepo huko miaka mingi,ni kwa nini hadi leo mmeshindwa kutekeleza mbachokifikiria hadi mkakubalika?
Kama mnaokosoa hivi mko CCM,kwa nini msipendekeze vyama hivi vifutwe au muwe wakweli tu kuwa mlivianzisha ili kudanganyia wakubwa wa dunia ili kila mtu ajue aweze kuwa kama Mzee Cheyo na Mrema?Si muwaambie ukweli akina Lissu ili wasikomae kupita kiasi hadi kuwa target ya wauaji wasiojulikana?
Mnaosema hivi,je mnaamini kwamba kuna watu wamezaliwa kuwa wapinzani tu na wengine watawala tu?Kama mnadhani hivyo basi hiyo ni imani potofu na inashiria tatizo kubwa zaidi zaidi la kifikra kuliko kuwepo upinzani uchwara wenyewe
Kutokujua mpira haimaanishi kwamba yanga ikicheza vibaya ndo usiseme. Watu tumepewa karama tofauti, wengine wanasiasa, wengine wakulima, wengine wafanyabiashara nk. Wanasiasa wa upinzani kama hawafanyi inavyotegemewa tutawakosoa tu. Waache kujiuza wafanye wajibu wao.
 
Kwa nini msiwe tu wakweli mkasema vyama vya upinzani vinakufa kwa sababu vimedhibitiwa kufanya siasa? Kwa nini mnashiriki dhambi ya uongo bila sababu za msingi?
 
Ina maana hata hukuona suggestion ya upinzani ya bajeti kupunguzwa ukubwa ili itekelezeke 100%?? Hyo hukuiona

Hukuona suggestion kuhusu vyanzo vipya vitatu kma source of income kufund bajeti as proposed na halima mdee kwenye bajeti kivuli???

Je unazungumziaje hayo mapendekezo mawili ya upinzani je yalikuwa hayana tija..... Tuanzie hapo kwanza
Kwanza kiongozi hoja ya kupunguza bajeti itekelezeke ni hoja dhaifu sana. Maana ya bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi. Serikali hufanya analysis na kutambua tunaweza kupata mapato katika vyanzo vya ndani, mikopo iliyonafuu na wahisani then wanatengeneza bajeti. Ukisoma sheria ya bajeti, inatoa flexibility za kibajeti. Mfano serikali inaweza kufanya uhamisho wa fedha za bajeti kwa asilimia 10 ya bajeti yote na kwa kupeleka ela katika matumizi ambayo yanahitaji fedha zaidi kuliko ilivyokadiriwa. Pili; watanzania tutambue kulipa kodi ni jukumu la kila mtu ila wajanjoa wengi hatulipi kodi hivyo kuathiri mapato. Pia; wahisani wanaweza kutoa commitment kipindi cha kuandaa bajeti na badae wakashindwa kutoa ama wakatoa zaidi. Kwa hiyo hoja ya kupunguza bajeti haina mshiko; cha msingi ni hela zilizopatikana zinatumika vyema.
Kuhusu vyanzo vipya walivyoproposed baadhi vilifanyiwa kazi vingine vikaonekana havina tija. Suala ya kodi ya rasilimali za taifa hili; hili lilikuwa katika mikakati ya serikali. Mi nilizani masuala ya kifedha; kama wapinzani wangetoa direction yao kwa misingi ya imani yao ili tuone mbadala ni upi. Ila still kuna haja ya vyama vya upinzani kuwa na sera madhubuti kuaminisha jamii.
 
Sasa mkuu kma ni hoja dhaifu kivp msichukue kwani wana nini cha kupoteza?? Yaani miaka 50 sasa bajet ya serikali ya CCM ya maendeleo haijawahi kutekelezeka hta kwa 50% alafu mkiambiwa mpunguze yasiyo na tija mnasema HOJA DHAIFU??? Sasa ukisema usinunue pangaboi alafu hyo hela iende kwenye wizara ya maji ili wilaya zote ziwe na maji safi na salama mnashindwa nni??? Mkishauriwa wabishi eti hoja dhaifu nakumbuka hta elimu bure mlisema haitekelezeki ila leo hii mnaitekeleza!!!

Kuhusu mapendekezo ya vyanzo vipya vya mapato niweke rekodi sawa hakuna hata moja ambayo serikali ya CCM ilipledge kuadopt zaidi walikosoa ili wasiwape credit upinzani yaani taabu kwelikweli hii nchi alafu bajeti ikifeli tena mnasema wananchi hawalipi kodi hivi miaka 50 mnategemea kodi za wananchi tu kwanni msiboost uwekezaji kwenye kilimo tuuze nje tupate mafedha ya kigeni mnakalia kusubiri VAT na payee miaka 50 are we serious????

Nakumbuka hata magufuli alisema wamepunguza allocation ya pesa kwenye wizara ya maji ili itekelezeke kwa 100% yaani kuliko kuweka lets say billion 500 mnaweka billion 100 sababu mko sure itapatikana hivyo itatakelezeka kwa 100% ila nashangaa wwe unatofautiana na mwenyekiti wa chama chako aliyekiri bajeti ikiwa na figures kubwa inakuwa chanzo cha kutokutekelezeka sababu haipo realistic!!!! Sasa nikuamini ww au mwenyekiti wako aliyekubali hoja ya mdee???

Ni hayo tu
 
Kma upinzani hauna hoja ya maana je umeshawahi kupitia hata hotuba ya KUB kwa wizara mbali mbali pale bungeni???

Je umewahi pitia ilani ya uchaguzi chadema 2015-2020

JE umesoma bajeti kivuli yoyote toka umeanza kufuatilia siasa

Tuanzie hapo kwanza

Kuandika hujui, kujibu hoja hujui pia.
 
Kama ni kanjanja waachie wafanye mikutano, msisaidiwe na polisi wakati wa uchaguzi muone
 
Nani awaachie? Na wasipoachiwa ndo kusema watakaa tu kama maboya milele?

Hili nalo ni swali zuri, Nadhani matumizi ya nguvu hayaepukiki kudai demokrasia. Nadhani kimya kingi kina mshindo mkubwa, it is amatter of time
 
Tangia uongozi wa awamu ya tano uingine madarakani; mengi yameanza kuonekana kuhusu uhalisia wa upinzani wa taifa hili. Upinzani katika inch hii umekosa muelekeo ya nini wanakitaka na kukisimamia. Hoja za msingi wananchi walizozitarajia kutoka kwao zimeyeyuka.

Hususani hoja ya kupiga vita rushwa na ufisadi, kutowajibika na uzembe kwa serikali na mengineyo. Wananchi wanataka kuona upinzani uliosimama kwa kupigania haki zao na kujenga hoja za maendeleo ya taifa hili.

Wananchi wanataka rasilimali za taifa hili zisaidie kunufaisha taifa hili sio kuibiwa na wageni. Wapinzani wamekuwa na utamaduni wa kukosoa kauli za rais na watendaji wake bila kuja na hoja mbadala. Kiufupi upinzani katika taifa hili umekuwa hauna dira wala muelekeo wa nini hasa wanaona mbadala katika kuleta maendeleo ya taifa hili.

Kuna hoja wanasimamia kusema ccm imeongoza miaka 50 lakini hakuna maendeleo. Hivi hawa jamaaa wanaelewa tumetoka wapi. Mi niwakumbushe kidogo tu; miaka ya 1970's usafiri ulikuwaje Tanzania. Ulikuwa unasafiri siku ngapi kutoka Dar hadi Songea ama Arusha.

Pili; idadi ya wasomi walikuwa wangapi na sasa wako wangapi; vipi kuhusu maendeleo ya miji na mikoa ilikuwaje kulinganisha na sasa (najua kuna watu humu wanapicha ya Dar es Salaam miaka ya 1970's, maybe wakiwawekea mtaweza kuelewa tuliko toka). Vipi kuhusu upatikanaji wa nishati ya maji na umeme ilikuwaje ukilinganisha na sasa.

Kama hoja ni hii, swali ni kwamba upinzani unaleta hoja ipi mbadala ya kupaisha taifa hili katika maendeleo ya haraka kiasi wanachoota wao? Ili upinzani wa Tanzania usionekane kanjaja naomba wadau mtuambie tu; ni vitu gani mtakavyoleta kwa muda mfupi tufikie hayo maendeleo mnayosema ccm imeyashindwa kwa muda wa miaka hamsini?

Naomba kuwasilisha.

Wananchi wa tanzania wanahoji haya:
Nyumba za serikali zilizouzwa kwa vimada kwa bei ya kutupwa! Waliouza madini yetu ikiwemo mafuta na gase, walioweka GPA kwenye elimu za watoto wao, walionunua vivuko vibovu na kuvipeleka jeshini, walioiba pesa za escrow hususan wale wa stanbic na sio hawa wa mkombozi, epa, kagoda nk. Wananchi wanataka kujua nani mmiliko wa vichwa vya train mlivyotangaza pale bandarini kuwa mmeokota , wanahoji zilipo ml 50 kila kijiji. Kule chuo wanahoji mikopo kwa wanafunzi.

Wanahoji ukanda na udini
Kama una amini upinzani sio lolote mwambieni huyo Mungu mtu wenu aruhusu japo wiki moj mikutano na awambie polisi na usalama wasishiriki uchaguzi tuone itakuwaje vinginevyo makelele y bure.

Hakuna kiwanda wala noah uongo mtupu wa kuwadanganya wakubwa wenzio kwamba Rose muhando karudi Ccm wakati 2015 alikuwa mburudishaji na kiburudisho
 
Kuingilia mada za watu !! Nayemuuliza keshajibu sasa ww sijui unaongea pumba gani au ndio wale fuata upepo wa kuambiwa upinzani hauna sera ila nkikuuliza hata kma katiba ya chadema ulishawahi kusoma unakodoa macho tu !!

Sory nadhani nilikosea kujibu, Nilikua namjibu mtoa mada, sorry sana
 
Wananchi wa tanzania wanahoji haya:
Nyumba za serikali zilizouzwa kwa vimada kwa bei ya kutupwa! Waliouza madini yetu ikiwemo mafuta na gase, walioweka GPA kwenye elimu za watoto wao, walionunua vivuko vibovu na kuvipeleka jeshini, walioiba pesa za escrow hususan wale wa stanbic na sio hawa wa mkombozi, epa, kagoda nk. Wananchi wanataka kujua nani mmiliko wa vichwa vya train mlivyotangaza pale bandarini kuwa mmeokota , wanahoji zilipo ml 50 kila kijiji. Kule chuo wanahoji mikopo kwa wanafunzi. Wanahoji ukanda na udini
Kama una amini upinzani sio lolote mwambieni huyo Mungu mtu wenu aruhusu japo wiki moj mikutano na awambie polisi na usalama wasishiriki uchaguzi tuone itakuwaje vinginevyo.makelele y bure. Hakuna kiwanda wala noah uongo mtupu wa kuwadanganya wakubwa wenzio kwamba Rose muhando karudi Ccm wakati 2015 alikuwa mburudishaji na kiburudisho
Mr. Tairi bovu kwa maelezo yako ndio maana ninasema upinzani wetu ni kanjanja kabisa. Kama hizo hoja ndio upinzani wanataka kujua basi hawahitaji kupayuka kupitia hivyo unavyosem mikutano ama nini. Kwanza ujue wananjia mbalimbali ya kuibana serikali kupata majibu ya hizo hoja. Cha kwanza wanaweza kuitumia bunge vizuri na kuuliza hizo hoja ili kupata majibu sahihi. Pili kama hizo hoja zinatakiwa kutolewa katika mikutano ya hadhara; Mhe. Mbowe na wabunge wengine wahoji kupitia mikutano yao ya hadhara.
 
I

Kwenye mkutano wa hadhara?? Je wananchi wa mpanda watajuaje?? Je jimbo la nyanghhwale ambako hakuna hta diwani wa chadema wataskiaje??? Na sheria gani inalimit mikutano ya siasa kwa wabunge tu

Tuwekane sawa hapo
 
Sasa mkuu kma ni hoja dhaifu kivp msichukue kwani wana nini cha kupoteza?? Yaani miaka 50 sasa bajet ya serikali ya CCM ya maendeleo haijawahi kutekelezeka hta kwa 50% alafu mkiambiwa mpunguze yasiyo na tija mnasema HOJA DHAIFU??? Sasa ukisema usinunue pangaboi alafu hyo hela iende kwenye wizara ya maji ili wilaya zote ziwe na maji safi na salama mnashindwa nni??? Mkishauriwa wabishi eti hoja dhaifu nakumbuka hta elimu bure mlisema haitekelezeki ila leo hii mnaitekeleza!!!

Kuhusu mapendekezo ya vyanzo vipya vya mapato niweke rekodi sawa hakuna hata moja ambayo serikali ya CCM ilipledge kuadopt zaidi walikosoa ili wasiwape credit upinzani yaani taabu kwelikweli hii nchi alafu bajeti ikifeli tena mnasema wananchi hawalipi kodi hivi miaka 50 mnategemea kodi za wananchi tu kwanni msiboost uwekezaji kwenye kilimo tuuze nje tupate mafedha ya kigeni mnakalia kusubiri VAT na payee miaka 50 are we serious????

Nakumbuka hata magufuli alisema wamepunguza allocation ya pesa kwenye wizara ya maji ili itekelezeke kwa 100% yaani kuliko kuweka lets say billion 500 mnaweka billion 100 sababu mko sure itapatikana hivyo itatakelezeka kwa 100% ila nashangaa wwe unatofautiana na mwenyekiti wa chama chako aliyekiri bajeti ikiwa na figures kubwa inakuwa chanzo cha kutokutekelezeka sababu haipo realistic!!!! Sasa nikuamini ww au mwenyekiti wako aliyekubali hoja ya mdee???

Ni hayo tu
Mbona hujibu hii mkuu Zee la kitaa
 
I

Kwenye mkutano wa hadhara?? Je wananchi wa mpanda watajuaje?? Je jimbo la nyanghhwale ambako hakuna hta diwani wa chadema wataskiaje??? Na sheria gani inalimit mikutano ya siasa kwa wabunge tu

Tuwekane sawa hapo
Kiongozi hiyo hoja unayosema ungenielewa tu. Namaanisha kuna njia mbalumbali za kuwasilisha hoja moja ni hiyo; mbili ni bunge; kama haitoshi itisheni vikao vya ndani vya chama na wekeni live kupitia tv mbalimbali ujumbe utafika tu.
 
Back
Top Bottom