SoC03 Tanzania na maadui wapya

Stories of Change - 2023 Competition

File Suleiman

Member
Jun 5, 2023
9
7
Mwishoni mwa miaka ya 1970, Tanzania tuliweza kuingia katika vita nzito dhidi ya adui wetu kutoka Uganda Nduli Iddi Amini ambapo Uganda iliivamia Tanzania na kwetu akawa kikwazo na adui ambaye ilibidi tupambane nae/nao, na njia ya kupambana na adui wetu tulitumia jeshi na zana za kijeshi tukaingia vitani kupambana na adui yetu ambae alivamia Tanzania yetu, tulishinda vita na tukampiga Amini japo na sie tulipata madhara makubwa, tukayumba kiuchumi na tukapoteza maisha ya watanzania na mali zetu juu ya vita, hatukua na jinsi sababu ilibidi tupigane ili tumtokomeze adui yetu.

Katika maswala ya kiusalama na ulinzi aina hii tunaiita usalama wa kitamaduni ambapo njia ya kupambana na adui anaeivamia nchi yetu hua ni njia ya kijeshi na zana za kijeshi, pia nchi ndio muhusika pekee katika maswala ya Nchi na mahusiano ya kimataifa hii kitalamu ni nadharia ya KIrealism, mambo yamebadilka sana katika dunia ya leo hata kwetu Tanzania ni zaidi ya miaka 40 sasa Tanzania hatujavamiwa na nchi nyengine au madui waingie na dhana za kivita kutuvamiwa japo kuna changamoto za hapa na pale ila sio vita kama ya 1979.

Tanzania Kama ilivyo nchi zengine tunapitia changamoto ya madui wapya ambao hatuwezi tena kutegemea jeshi au silaha na zana za kijeshi kupigana na kutokomeza madui hao, madui wetu wapya ni kikwazo na tishio kwa usalama wetu, wanachi wetu, vizazi vyetu na pia madui wetu wapya wameweza kuleta madhara kuliko hata madhara ya mwaka 1997 dhidi ya vita vya Kagera, Hatuna budi kuwa waelewa na kumakinika na madaui hawa ambao tusipokua makini wataimalia Tanzania yetu:

Uslama wa Kimazingira na adui mpya wa mabidiliko ya tabia ya nchi, Jeshi letu pendwa laweza linda mipaka yetu ili madui wasituvamie au wasije leta madhara kwa nchi yetu lakini mazingira yamekua tishio kubwa sanana hatari mnoo katika nchi yetu, shughuli za kibinadamu zisizo na ueledi zimechangia kumkuza adui uyu na sasa ni adui sugu, Tanzania tupo katika tishio la ukame na njaa sababu ya mvua kutokunyesha kwa msimu fikirika tuliozoea, mito kukaukaa na kutishia changamoto ya umeme na maji nchi nzima je hali ikiendelea kua ivi Tanzania itakuaje??, Jeshi linapambana kulinda ardhi yetu isivamiwe ila ongezeko la joto linavyozidi linafanya kina cha bahari kuongezeka ipo siku uko miaka ya usoni Zanzibar yetu itabaki historia kwa kutoweka kama leo hii hofu inavyotawla katika nchi ya kisiwa cha Tuvulu na visiwa vingine vya bahari ya Pasific kuwa vipo hatiani kutoweka, tunaweza pambana kupambania eneo letu la ziwa Nyasa ila tukapoteza maeneo yetu kwa matokeo ya athari ya tabia ya nchi, leo hii maeneo ya jiji la dar es salaam yalippo karibu na mito kama mto Msimbazi, Ng'ombe, Mbezi yanakaribiwa na atahari kuba ya kumezwa na nyumba nyingi zimemezwa na maji, baridi na joto kali limekua tatizo na karaha kwa mikoa ya pwani na nyanda za juu mwa Tanzania kama hali ikiongezeka itakuaje kwa badae itakua kama Ulaya na Asia wanavyokufa kwa joto kali, ivyo usalama wa kimazingira upo mashakani na adui mpya mabidiliko ya tabia ya nchi.
download.jpg

(Pichani ni waziri wa mmbo ya nje wa Tuvulu, Simon Kofe akiwawasilisha Mjadala wa madiliko ya tabia nchi kwa njia ya Video katik mkutano wa kimataifa wa madiliko wa tabia ya nchi wa COP26 , November 5, 2021 nchini Tuvalu akionyesha madhara na athari ya tabia ya nchi ilivyotishio kwa nchi iyo kumezwa na maji. chanzo na ha habari na picha ni REUTERS)
download (1).jpg

(Picha kwa hisani ya Tovuti ya JamiiForums, ikieleza mgao wa umeme kwa baadhi ya mikoa ambapo hii yote ni atahari za mito kukaukaa inayochangia uzalishaji wa maji kua hafifu na Tanzania inaingia katika hatari ya kukosa nishati kama umeme

Usalama wa Kitamaduni na tishio la Tamaduni zakigeni, Tamaduni ni maisha na alama za mwanadamu, jamii au jambo fulani kwa miaka mingi Tamaduni za Kiafrika zimekua zikitokomea polepole na vizazi vijavyo vya Tanzania ni ngumu kuja kujua asili yao na mwenendo wao halisi, Utandawazi umeleta tamaduni mpya za kimagaribi na kiasia ambazo zinaondoa na kufuta kabisa Utanzania wetu, kwa sasa sekta ya burudani kama mziki, filamu, maonyesho na mitindo vimeathiriwa na tamaduni za kimagharibi, ni nadra sana katka tasnia iyo kuona Utanzania wetu zaidi umemezwa na kuchakachuliwa na tamaduni za nchi nyengine kuanzia midundo, uvaaji, uchezaji na ufasilishaji, sio tuu sekata ya burudani hata kwenye maisha yetu ya kawaida tamaduni za nje zimechukua nafasi, leo hii serikali ipo njia panda katika mambo ya mapenzi ya jinsia moja ila kiuhalisia mapenzi ya jinsia moja yashakita mizizi na siku serikali ikitangaza au ruhusu hatutumshangaa Musa bali tutastajibishwa na ya firauni, leo hii mTanzania aliefika chuo awezi ongea maneno kumi bila kutia neno la kizungu, atahri ni kubwa na ni nzito kwa vizazi vyetu mana tamaduni za wenzetu tunazitukuza na kuziona bora mnoo na wao wenzetu tamaduni zao wanazikuza na kuzipaisha mwisho wa siku tunaanza tawaliwa kifikra kwa kuona vyetu havina mana na ngumu kujisifu mbaya zaidi vikifutika kwa jamii kushindwa vifanya kwa aibu leo hii Mzaramu yupo tayali kushiriki Haloweni na kuisfia lakini ataoana aibu kuzunguzmia unyago na kuchzezwa ndio mana tunatawaliwa mana hata elimu yetu imetawaliwa na tamaduni za kimagaharibi.

Usalama wa Chakula na tishio la usalama wa chakula, kwa miaka hii ya sasa vijana wengi wanatumia dawa za kuongeza nguvu za kiume na misuli, uku dada zetu wengi wakijifungua kwa oparesheni, haya mambo zamani ni ilikua adimu kuyasikia wala kuyaona ila kwa jamii yetu ya sasa ni kawaida mnoo na hii yote ni aina ya vyakula tunavyokula vimefanya tufikie uku, pia tishio la chakula sio kwa afya bali kuna siku nchi itakosa chakula kutokana na aina ya pembejeo tunazozitegemea shambani amazo mbegu nyingi kwa sasa ni ukitumia zinakua hazina tena matumizi yake mana ake mkulima akatafute tena mbegu, aina ya mbolea na madawa yanamadhara hata kwa aina ya kilomo kwa miaka ya badae hali ni tete, nguvu kazi inapotea vijana wengi ni lege na hatujui tunazaa viumbe vya aina gani, tunaweza siku moja nchi yetu tukawa tumezaa watoto matahira au wenye kasoro mbalimbali na tukawa nchi isio na rasilimali watu wajenzi.

Ushauri wangu ni wizara ya ulinzi na na usalama ijikite zaidi katika hawa maadui na kushirikiana zaidi na wizara zenye majukumu mama kama wizara ya mzingira, wizara ya tamaduni na wizara kilimo na mifugo pia na wizara kama wizara ya mambo ya ndani na wizara zenginezo kikamilifu kupambana na hawa madui wapya mana usalama na ulinzi sasa sio kulinda mipaka tuu bali kuna madaui ambao wanatuvamia na hatuwezi tumia bunduki au mabomu, bali elimu na mikakati endelevu pia elimu kwa jamii ambapo jeshi lipewe jukumu la ubalozi wa mzingira kwa jamii iweze jichanganya katika kutoa elimu ya kimazingira kwa vitendo kama wanaenda vitani mana vita halisi sasa ni hao madui wapya, mana mchango wa wabunge juu ya masuala yaulizi na kiusalama katika bajeti ya 2023/2024 wengi walikua na mawazo ya uslama katika mitazamo ya kitamaduni walishindwa kutafakari kama kuna atahri mpya ambazo ni changamoto kubwa sana au waeze kuoanisha mataizo mengine yawe sehemu ya miakakati katika wizara ya ulinzi na usalama kikamilifu kwa kushirikiana na wizara zengine.
 
Back
Top Bottom