Tanzania na kizazi cha wasomi wezi na wavivu!

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,616
12,277
Nina andika hii mada nikijuwa kabisa itaenda kugusa watu wengi na hasa ukizingatia jamiiforum inawasomi wengi. Ila ni bora tukalitumbuwa hili jibu ili vijana tukakumbuka tulipotoka na kule tutalipeleka hili taifa. Siku za hivi karibuni baada ya bwana mkubwa kuchukua nchi yameibuka mambo mengi ambayo yanatia mashaka makubwa ya nguvu kazi ambayo ndio gurudumu la maendeleo.

Vijana wa Tanzania kwakweli tunatia aibu nakuzuwa maswali magumu yasio kuwa na majibu ikiwa tunadhamira ya dhati kulipeleka taifa hili mahali fulani au tunawaza matumbo yetu tu.

Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanao ajiriwa ktk serikal na secta binafsi lakini pasipokujali thamani ya kazi na muda wa wao vijana wengi tumekuwa kero kwa waajiri even if utamlipa vizuri kias gani.

Vijana wamekuwa wezi na walio kosa uwaminifu kwa waajiri wao jambo limefanya makampuni mengi kuajiri watu toka nje ilikupunguza hasara wanapata.

Wakati serikal inapambana na waajiri wasilete watu wao kufanya kaz ndani ya taifa letu, waajiri wanapeleka ushaidi wa upotevu wa mamilion uliosababishwa na watu wao. Hili swala linatishia ajira za maelfu ya wazawa na mwisho wa siku wa tz tutakuwa makarani mwanzo mwisho, just b'coz tupo majizi.

Uvivu na uzembe hili ndio balaa tupu mtu anakuja muda anataka kazin, maudhuru yakutosha, kaz hafanyi mambo kibao yamelundikana alimradi siku iende. Mbaya zaid haya mavivu ndio malalamish mshahara hautosh na mbwembwe kibao, sim wasapp from asubuh jion.

Jamani vijana tubadilike au tusubirie kuwa makarani wakati wakenya na waganda wakija kuchukua nafasi zetu. Taifa hili linatutegemea ila sio kwakuwa wavivu na wategevu wakazi. Tafakarini 2016 itakuwa chungu kwa mijitu mizembe na mivivu.
 
Huu ni ukweli kabisa kwa hiki kizazi pumbavu, yaani kumuajiri kijana wa kitanzania ni sawa na kuotesha jipu sehemu za siri,, yaani kazi kwao ni leasure tu au msaada umewapa,, wengi wao wanareflect ule usemi wa donald trumph " african they are good for Sex,theft nk..

Kijana ameajiriwa ana miezi miwili anataka aishi kama 50cent au diamond... Kiukweli bila kubadirika mind Set kwa vijana wa kitanzania basi hali ni mbaya sana wakuu.

niukweli usiopingika vijana wakitanzania waliopata bahati ya kuajiriwa kwenye makampuni makubwa wametia sana watu na waajiri wao hasara,,, mfano mabenki, makampuni ya migodi,baadhi ya taasisi za serikali mfano tra,bandari na halmashauri.. ni hatari sana na inatia kinyaa!!!!
 
Tumainel. I real apriciate you bro. saiv mtu kamaliza chuo kikuu anataka mil.20 . Ha ha ha ata ukimuuliza alichosomea hewez ata kupambanua mamabo ila anawaza kuwa C.O wa kampuni.
 
Tz nchi ya kitu kidogo na watu wadogo...hii ni hakika...JPM inabidi awatandike vema mithili ya punda....vinginevyo maliasili na utajiri wote wa TZ bado vitabaki kuwa nyimbo na blah blah tu....sana sana wataendelea kufaidi wajanja wachache waliokwishawekeana ma dili na watawala wenu walafi walioondoka...
 
TumainiEl

Asante kwa kulisema hilo sina cha kuongeza zaidi ya kukupongeza kwa ujasiri wa kusema yale ambayo vijana wa Kitanzania hawapendi kuyasikia,naamini siku zote msema ukweli ndie anakutakia mema,nadhani watakao taka kusikia na wasikie,wale watakao weka nta masikioni na waendelee hivyo hivyo dunia imebadirika ,vijana wetu tusiwe kama vijana wa Afrika Kusini.Hata kwenye vitabu vya kidini imeandikwa na '' asiyefanya kazi asile''
 
Last edited by a moderator:
Umeongea sana, mungu akubariki, kubadilika huku sijui kutaletwa na nini aisee mungu atusaidie watanganyika
 
Hili suala limeanzia kwenye mfumo wa serikali yetu especially kipindi cha Mkapa. Viongozi walijaa kiburi na waliiba fedha hadharani kitu kilichosababisha kila kijan a aliyetafuta kazi shughuli ilikuwa ni kuiba tu.

Alivyokuja mzee wa Msoga ndiyo mambo yakawa tambarare kabisaaa, so Ndani ya miaka 20-25 ilikuwa ni wizi wa kutisha
 
Mtu ukimiliki kampuni ndio utayaona haya.

Huitaji kuambiwa na wakiambiwa wanakuwa wakali.

Ila ukweli ni kwamba vijana wa Tanzania sasa hivi competency ni ziro.

Muda wote wapo whatsap, kuwaza kuchat, ngono na ujinga.

Ukiwapa kazi wanawaza kuiba tu.

Kila siku excuses, mara nimefiwa yani ujinga mtupu.
 
Huu ni ukweli kabisa kwa hiki kizazi pumbavu, yaani kumuajiri kijana wa kitanzania ni sawa na kuotesha jibu sehemu za siri,, yaani kazi kwao ni leasure tu au msaada umewapa,, wengi wao wanareflect ule usemi wa donald trumph " african they are good for Sex,theft nk.. kijana ameajiriwa ana miezi miwili anataka aishi kama 50cent au diamond... Kiukweli bila kubadirika mind Set kwa vijana wa kitanzania basi hali ni mbaya sana wakuu..
niukweli usiopingika vijana wakitanzania waliopata bahati ya kuajiriwa kwenye makampuni makubwa wametia sana watu na waajiri wao hasara,,, mfano mabenki, makampuni ya migodi,baadhi ya taasisi za serikali mfano tra,bandari na halmashauri.. ni hatari sana na inatia kinyaa!!!!

Ni kweli naunga mkono Kwa 100%vijana wengi wakiwa kazini huwa wanawaza 10% kupiga na madili ya kila aina , utamkuta kijana anatumia mda mwingi kubuni jinsi ya kuiibia kampuni badala ya kuisaidia kampuni ikue zaidi tena wengi wakipata pesa huwa ni kushinda Bar , Disco na Guest House na kukimbilia kununua Alteza, crown nk , Magufuli apige marufuku vijiwe vijiwe na bar kufunguliwa mda wa kazi maana imewafanya Vijana wengi kukimbilia huko kupoteza mda mwingi huku kazi zikisimama.
 
Mtu ukimiliki kampuni ndio utayaona haya.

Huitaji kuambiwa na wakiambiwa wanakuwa wakali.

Ila ukweli ni kwamba vijana wa Tanzania sasa hivi competency ni ziro.

Muda wote wapo whatsap, kuwaza kuchat, ngono na ujinga.

Ukiwapa kazi wanawaza kuiba tu.

Kila siku excuses, mara nimefiwa yani ujinga mtupu.

Utendaji kazi wa Vijana wengi ni wa hovyo sana hasa wale wapenda starehe walevi wasiolala Usiku wanakesha kuzurula kwenye bar na kwenye kumbi za dansi nk, wengi wakikaa vikundi story zikiisha wanabakia kujadili watu wenye pesa kuwasifia wezi na watu wajanja wajanja , mda mwingi hutumika kupiga majungu , visingizio kibao yaani ndani ya wiki siku saba kazini huenda siku 2 au 3 tu zingine zote ni visingizio vya misiba, kuuguliwa, kuumwa nk, wapo busy kubuni wizi kuliko maendeleo ya kampuni.
 
Hili suala limeanzia kwenye mfumo wa serikali yetu especially kipindi cha Mkapa. Viongozi walijaa kiburi na waliiba fedha hadharani kitu kilichosababisha kila kijan a aliyetafuta kazi shughuli ilikuwa ni kuiba tu.

Alivyokuja mzee wa Msoga ndiyo mambo yakawa tambarare kabisaaa, so Ndani ya miaka 20-25 ilikuwa ni wizi wa kutisha

Mfumo wa ccm ni kulea Vijana wapenda kata K(mlegezo) vimini na vinguo vya hovyo hovyo pasipo kukumbuka kuwa Taifa Lina wajibu wa kusisitiza Malezi bora kuanzia chini Kama wafanyavyo Uganda ambapo Mseveni alimtambua kuwa maadili ya Vijana yameathirika sana kutokana na utandawazi hivyo wasipokuwa makini watazalisha viongozi wa hovyo huko mbeleni ndipo akaja na suluhisho mapema ( samaki mkunje angali mbichi) . Tanzania hakuna kiongozi tokea awamu ya pili hadi hii ya tano amewahi kukumbuka kuwa Maadili ya Vijana wa Taifa hili ni mabovu sana na ndiyo chimbuko la kuwa na viongozi wezi Mafisadi nk , ebu fikiria kuwa Mvaa mlegezo wa leo ndiyo kiongozi wa kesho unategemea nini zaidi ya kuwa na kiongozi wa hovyo mpenda dili na starehe, Nape Kama kweli anajua wajibu wake ni Kipindi cha yeye kupiga marufuku Uvaaji wa hovyo hovyo na kuwasisitiza Vijana wachape kazi waache kukaa vijiweni , bar na kupiga story kujadili watu na Ujinga Ujinga mwingi hakika Nchi itazalisha Vijana bora na kupanua Ajila sehemu zingine Duniani kinyume na hapo kampuni za kigeni zitaendelea kuleta wafanyakazi toka nje ,
 
Zamani tulizoe Wanawake ndiyo wambea na wapenda majungu, lakini siku hizi Vijana wamekuwa wambea balaa wengi wakiwa bar hawana story za maendeleo kazi ni moja tu kujadili watu na kuwaza michepuko nk, Rais Magufuli asipolitatua hili JIPU kubwa mapema asitegemee mapya huko Mbele kwani Hawa Hawa wanaoshinda bar wakiwa wamevaa milegezo ndiyo viongozi wa kesho . Tanzania bado sana maendeleo tutaendelea kuyahadithia tu humo humo vijiweni na kwenye bar .
 
Wizi na utapeli. ..kusifia watu sababu ya hela hata kama ni haramu

Hasa hasa wale wapenda kukaa vijiweni na bar mda mwingi huwa ni story za majungu na kujadili watu huwakuti kujadili maendeleo hata siku moja.
 
Utendaji kazi wa Vijana wengi ni wa hovyo sana hasa wale wapenda starehe walevi wasiolala Usiku wanakesha kuzurula kwenye bar na kwenye kumbi za dansi nk, wengi wakikaa vikundi story zikiisha wanabakia kujadili watu wenye pesa kuwasifia wezi na watu wajanja wajanja , mda mwingi hutumika kupiga majungu , visingizio kibao yaani ndani ya wiki siku saba kazini huenda siku 2 au 3 tu zingine zote ni visingizio vya misiba, kuuguliwa, kuumwa nk, wapo busy kubuni wizi kuliko maendeleo ya kampuni.

Humu ndani kumbe kuna wazee!! Au hayo ninayoyaona humu ni mawazo ya vijana ambao akili imedumaa kama Mchucha ambao umepandwa jangwani kwenye mwamba? Post zimekaa kiwivu wivu tu
 
Back
Top Bottom