Tanzania: Mkutano wa kitaifa kuzungumzia hali ya uchumi hivi sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Mkutano wa kitaifa kuzungumzia hali ya uchumi hivi sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sammy Sr., Oct 23, 2008.

 1. S

  Sammy Sr. Member

  #1
  Oct 23, 2008
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UKIACHILIA MBALI wale wanaotaka kuchukulia hali ya kiuchumi hivi leo kama mtaji wa kisiasa bado ninaamini kwamba ni muhimu kwa Mheshimiwa kuitisha kikao cha kitaifa kuzungumzia hali hii ili tujiulize maswali na tuatafute namna ya kujipanga ili tugeuze hasara kuwa faida kwa upande wetu.

  TUSIKUBALI kabisa kutekwa na mawazo eti kwa sababu Marekani na Uingereza wana hali mbaya basi na sisi (labda kwa wale waliowekeza kwenye nchi hizo badala ya kuwekeza hapa nyumbani) basi na sisi ni lazima tu athari za 'American and European generated recession zitukumbe na sisi!'

  Kuna vitu viwili vinatokea hapa. Wamarekani na wazungu wengine wamekula hasara kutokana na mismanagement ya benki zao. Lakini wakati huo huo bei ya mafuta ambayo ndiyo kitu crucial kwetu imeanza kushuka tena kwa kasi kubwa.

  Ukichukulia kwamba huko majuu watu sasa watataka vitu vya bei nafuu, je, sisi tumejipanga kiasi gani ili tuwe na bidhaa za kuuza huko kwa bei nzuri kwa upnade wetu lakini rahisi kwao?

  Je, tunaweza kuanzisha AKIBA AU HIFADHI KUBWA YA MAFUTA YA PETEROLI NA DIZELI ili bei ikianza kupanda tena sisi isituathiri hadi baada ya muda mrefu kuliko ilivyokuwa awali.

  Linaloendana na hili ni kuwa huko juu hamna nafaka kabisa. Je, tunawezaje kuwahamasisha Watanzania ili ifikapo Februari mwaka huu nchi nzima ijizatitii katika kupanda nafaka mbalimbali na hasa mahindi ili tuwe na zao kubwa la kutosha kuuza na kuingiza fedha za kigeni lakini wakati huo huo kutuwezesha kuanza majarabirio ya bio-fuel.

  Ufaransa imetengeneza gari linalotumia UPEPO, je, tunaweza kumtafuta yule mzee Athumani Mtengeni aende na kundi la wahandisi toka jeshini ufaransa kujifunza mradi huu? Na ufaransa kwa kuwa ndoa yao na Rwanda imevunjika wana njaa kweli ya mchumba hapa Afrika Mashariki.

  Je, tunaweza kuandaa MKAKATI WA UTALII WA KIUCHUMI ili kukaribisha WACHINA, WAHINDI, WAJAPANI, WAKOREA, WAARABU NA WAZUNGU kuja kutalii na wakati huo kuanza mazungumzo ya kuwekeza nchini katika vitu wanvyoamini vitaingiza faida haraka katika soko jipya la watu nusu bilioni la Afrika Mashariki, Kati na Kusini.


  Tunaweza kuboresha haraka haraka shule na vyuo vetu vikuu tukapata wanafunzi toka nchi za nje. aidha kuimarisha hospitali mbalimbali hadi kiwango cha kimataifa na kuanza kuvuta wagonjwa ambao la kama sio hivyo wangelipaswa kwenda kutibiwa Ulaya.

  Je, tunaweza kuanzisha chapuchapu maeneo maalum ya kuingiza bidhaa toka nje na kisha kuziuza haraka haraka tena nchi jirani na za mbali kama vile zimezalishwa hapa kwetu? [IMPORT-REEXPORT BUSINESS AREAS].


  Ninaamini tukondokana na ile 'mindest' ya kizamani kwamba ni viwanda na kilimo ndio vitatutajirisha na kukubali kwamba ni BIASHARA na HUDUMA ndizo kwa kweli zinazoweza kutupatia MITAJI tunayohitaji kuwekeza kwenye shughuli mbalimbali za uzalishaji tutakuwa tumefanya mapinduzi makubwa ya kimawazo na kimtazamo yatakayotusaidia kututoa kwenye nafasi ya 226 kati ya nchi 231 duniani kwa wepesi na kasi ya ajabu!

  Hatuhitaji hata kwenda mbali kuona ukweli kuwa ni HUDUMA na BIASHARA ndizo zinazomnyanyua Mtanzania haraka zaidi kuliko kilimo na uzalishaji mkubwa au mdogo ambao una matatizo kebekebe!

  JE, wanatusikia IKULU? Mkutano wa kitaifa upo au haupo?

  Je, tunaweza kujipanga na kusafirisha kwa wingi zaidi matunda, maua, ndizi, viazi, mihogo, nyama, samaki, maziwa-kwa kuwa na magari makubwa ya kisasa kwa ajili hiyo; ndege kubwa za mizigo; meli na vyombo vingine vya majini? Na nchi za kuvipeleka ikiwemo South Afrika, Zimbabwe, Swaziland, Lesotho, Botswana, Zambia, Malawi, Namibia, Angola na kadhalika. Katika hili natoa ushauri nilioupata kwa mzee kwamba ni vizuri Wizara ya Viwanda na Biashara itenganishwe. Mojawapoya wizara mpya iwe ni WIZARA YA BIASHARA YA KIMATAIFA ili kutoa msukumo zaidi kwa Tanzania kufanya biasha na nchi za nje.

  TATIZO kubwa la Watanzania ni kwamba tunashindwa kuuza tulicho nacho kwa wingi na kwa bei nzuri na tunashindwa kujiuza wenyewe lakni wepesi wa kuiuza nchi yetu kwa wageni. Nchi nzima lazima ipelekwa darasani ikajifunze MARKETING mwaka huu baada ya kikao hicho cha kitaifa.

  Maana MARKETING AU COMMERCE ni kama vile viwanda au kilimo ukiichangamkia ipasavyo. Mbona madalali hawazalishi kitu jamani lakini wapo mjini na wana maisha mazuri kuliko wengi wetu. Hatujifunzi tu!

  sammy sr.
  dar es salaam
   
 2. I

  Iga Senior Member

  #2
  Oct 23, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NAONA hili limekuwa likizungumzwa kwa namna au njia mbalimbali. Nimewasikia Tanzania Daima wakisema hivyo. Profesa Lipumba jana kwenye sauti ya Ujerumani na BBC katangaza hivyo, na nyie wana JF mko mstari wa mbele pia. Sasa Mwanakijiiji kwanini usichukue dhamana hiyo na kuoganaizi mkutano wa Kitaifa kuzungumzia Hali ya Uchumi ya Tanzania 2008 and beyond na mikakati ya kuhakikisha hatuzami zaidi ya hapa tulipofikia? Au tuchangishane wana JF wote ili tulifanye hili? Tusiulize Tanzania imetufanyia nini au itatufanyia nini bali tuulize SISI JF Tutaifanyia nini Tanzania?
   
 3. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naomba nipingane nawe licha ya uchambuzi wako mzuri.Tatizo hapa sio kutekwa na mawazo au ulazima wa kukumbwa na athari zinazozikabili most developed countries like US na UK.Laiti uchumi wa dunia (global economy) ungekuwa unatoa nafasi kwa developing countries like Tanzania kujipangia mambo yake basi wala tusingesumbuka na kuyumba kwa uchumi wa wafadhili wetu.By the way,huhitaji EC 101 kufahamu kuwa taifa lolote linalotegemea misaada lazima litaathiriwa na kuyumba kwa uchumi wa mfadhili/wafadhili wake.Hata uchumi wa mtaani unatueleza hivyo.Mtu unayemtegemea kwa kumpiga mizinga akichacha na wewe si unakuwa katika hali mbaya?
  Kaka,hii ishu haiko isolated kwa Wamarekani na WAZUNGU tu.Wajapani,Wakorea ya Kusini,na nchi kadhaa za Asia si Wamarekani wala WAZUNGU.Na kama mismanagement ya Benki,basi sie tumwombe Mungu tu yasitukumbe yanayowakumba wenzetu maana kama majambazi wa EPA wanahifadhiwa ilhali wenzetu wanawakalia kooni wanaodhaniwa kuhusika na financial crises kwenye nchi zao,basi tukae tukijua huko mbele ni hatari (kama BENKI KUU haiaminiki what to expect kwa benki "za kawaida"?)
   
Loading...