Tanzania Miaka Hamsini Ijayo: Fursa kwa Magufuli

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Wakati wa Nyerere Tanzania ilikuwa ikifuata, au tuseme ilitangaza rasmi kufuata, Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Mafanikio au kushindwa kufanikiwa kwa siasa hiyo ni jambo la mjadala. Lakini je, kwa sasa Tanzania inafuata siasa ipi? Bayana hakuna falsafa fulani inayoliongoza taifa. Ujamaa na kujitegemea? Huo unaonekana kupitwa na wakati. Hata Redio Tanzania Dar es Salaam kwa majina iliyonayo sasa imeacha kuweka ngonjera na mashairi ya kusifia ujamaa na kuwananga mabepari. Ubepari ni Unyama! ndio iliyokuwa kibwagizo cha miaka ile. Sasa hivi lakini hakuna pia vibwagizo vya kuusifia ubepari. Lipo ombwe la falsafa ya kitaifa.

Ilhali zipo falsafa nyingi ambazo taifa linaweza kuzichagua kuzifuata, siasa za uhurukweli, liberty, ndizo ambazo zinaweza kufanya nchi hii ipige hatua kubwa za maendeleo.

Kimsingi, uhurukweli unataka yafuatayo:

  1. Haki ya mtu binafsi kujiamulia mambo yake mwenyewe.
  2. Serikali iliyoachia nguvu ya soko kutoa ufumbuzi kwa mambo anuai.
  3. Kuwepo kwa mfumo imara wa sarafu isiyoweza kubadilishwa thamani na kitu chochote.

Kama Mheshimiwa Rais Magufuli akiichukua falsafa hii, atakuwa amejenga msingi muhimu ambao utalifanya taifa hili liwe na nguvu kubwa, lenye wananchi wanaoneemeka na taifa lao, na yeye kukumbukwa kama Founder of Modern Tanzania hata miaka hamsini ijayo. Isije kuandikwa kwenye vitabu vya historia namna hii:

1964-1985 JK Nyerere
1995-2005 BM Mkapa
2005-2015 JK Kikwete
2015-2025 JP Magufuli
2025-2035 Rais Fulani
2035-2045 Rais Mwingine
2045-2055 Rais Mwinginewe
2055-2065 Rais Mwinginewe Tena

Falsafa hii pia itamsaidia kupunguza changamoto nyingi ambazo zinatokea sasa hivi shauri ya ombwe la siasa inayofuatwa.
 
Napenda watu intellectual. Ukweli ni kuwa hakuna falsafa moja itakayoweza kuwa ni panacea kwa nchi za Afrika. Ni debate ndefu sana lakini kwa ufupi tatizo ni kuwa falsafa nyingi za maendeleo hazikuchukua mazingira ya Afrika kwa vile watungaji wake si Waafrika.
Mi naona turudie siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Hasa kwa vile mtunzi ni Mwfrika,na kwa kiasi fulani haitakuwa kuanza kitu kipya. Ila tuondoe mapungufu yaliyoamo ndani na kuendeleza mazuri, ambayo ni zaidi ya 80%. Hakuna mtu atayekuja Tanzania akawa na wakati wa kufikiria matatizo ya TZ kama Nyerere. Zama hizo hazipo kutokana na ushawishi wa TV,media,NGOs etc.
Hata Nyerere mwenyewe alishangaa kuwa kweli Ujamaa na Kujitegemea una makosa yake lakini ni busara kutupilia kabisa hata mazuri yake? Nini zuri katika kunafsisha mashirika ya umma ambayo yalikuwa yakijiendesha bila hasara?
 
Hii ni thread nzuri sana na nashangaa kwa nini 'Wabongo' hawachangii. Ah, lakini Wabongo wengi ni watu wa ngonjera na mipasho!
Kwa kweli nilikuwa nikifikiria kama tungeendelea kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ( baada ya kutoa mapungufu yake) viongozi kama Kikwete asingetokea. Na kama angepenya asingeweza kufanya excesses alizozifanya, kwa vile falsafa ya nchi ingembana. Asingeweza kwenda ' kuhemea' Ulaya mara 460 katika miaka kumi, kwa mfano!
 
Kitu kimoja ambacho kinatugharimu sana ni kutowekeza kwenye tafiti, tumezoea kutumia walivyogundua wenzetu bila kulinganisha mazingira yetu na yao.
China inapigwa sana vita lakini inaendelea kwasababu inajilinda na 'influence' za nje zisizo na maslahi kwao.
Tufanye tafiti ili tutumie vya kwetu kwa ajili yetu, tunaweza kuja na falsafa mpya ambayo ni mchanganyiko wa zilizopo, wasomi wachukue mawazo ya viongozi wetu waliopita na kuyapima yanaweza tumika vipi kwa kizazi hiki na kijacho
 
hapa kazi tu, ina tofauti gani na kila mtu ataishi kwa nguvu zake mwenyewe?

Ujamaa ulipigwa vita na mabepari ili wafikie malengo yao waliyoyapanga kipindi kirefu sema waliona haiwezi kufanikiwa bila ya kuleta kitu kingine cha kupambana na ujamaa. Wakati ujamaa ulikuwa ni kwa ajiri ya Afrika Ubepari ulikuwa kwa ajiri ya wazungu. Na ndo wakaweza kufight ujamaa na kilichofata ni kuweka kabisa viangalizi ama mizizi ya kuotesha ubepari kwa kuanzisha SAPs na vidudu vyake kama IMF. Madhara yake ndo tunayaona leo mfano viwanda vimekufa, ajira hamna na wahitimu hakuna anayejua hata kushika jembe wala koleo na bado unawaambia tunatatua tatizo, kazi za ofisini ziko ngapi ziwatoshe wote? kutoka 90% watu waliojua kusoma na kuandika mpaka 60% miaka hii ndo matokeo yao hayo. Mtu anaweza akasema viwanda tuliua wenyewe ama fulani lakini hiyo ni sababu tu, uharisia wenyewe upo kwenye de - industrialization policy yao sema hapa hawatafanya wao na badala yake watatengeneza mazingira ili ionekane mmeharibu wenyewe wakati mipango yote imeandaliwa na wao, ni kama kuandaa mechi wakati unajua matokeo tayari hata kabla ya dakika 90. Ujamaa ulisaidia katika mengi sana lakini kikubwa ni watu kupenda kufanya kazi na kujitegemea, inakusaidia kuwa na ziada hata pale hari inapokuwa ngumu hamtapoteza pesa yenu nyingi kununua huduma badala yake mtakuwa na nafasi nzuri ya kuuzia wengine na kupata faida. Hiki kitu wazungu hawataki kitokee Afrika katu.
 
Kitu kimoja ambacho kinatugharimu sana ni kutowekeza kwenye tafiti, tumezoea kutumia walivyogundua wenzetu bila kulinganisha mazingira yetu na yao.
China inapigwa sana vita lakini inaendelea kwasababu inajilinda na 'influence' za nje zisizo na maslahi kwao.
Tufanye tafiti ili tutumie vya kwetu kwa ajili yetu, tunaweza kuja na falsafa mpya ambayo ni mchanganyiko wa zilizopo, wasomi wachukue mawazo ya viongozi wetu waliopita na kuyapima yanaweza tumika vipi kwa kizazi hiki na kijacho

Tafiti zenyewe hata tukifanya sisi bado hazisaidii kwasababu bado njia zinazotumiwa ni za kimagharibi zaidi wakati tunatafuta majibu ya matatizo ya Afrika. Literature nyingi sana utakayoitumiwa imeandikwa ama na wazungu ama kwasababu ya wazungu kwasababu wao ndo wafadhiri wa tafiti zetu. Ni waafrika wangapi wanatoa pesa yao kufanya tafiti zao kwa ajiri ya nchi zao? wengi wao wanasubiri wazungu walete ili wakapige hela wakati mnatafiti tatizo lenu wenyewe. Mwalimu Nyerere alisema ni lazima mifumo na aina ya elimu ya Afrika itengenezwe zaidi katika kujibu matatizo ya waafrika wenyewe, lakini leo mitaala yoote ni ya kuletewa, pesa za uendeshaji ni misaada ya marekani, watoa semina ni wajerumani, mpaka tathimini ya elimu yenu wanafanya waingeleza na wahindi, hapo nyinyi mna nini? hilo ndo kumuenzi Nyerere? kwa namna hii Afrika tunajitegemea kweli? lakini ni kwanini? ni kwasababu sisi tumefanywa wategemezi, kaeni sisi wazungu tutawafanyia waafrika. Kwanini mkubali kukaa alafu muwaache wenzenu wawafanyie? Waafrika sisi ni viwete?
 
Nadhani kunautofauti mkubwa sana kati ya falsafa na kauli mbiu. Mtazamo wangu, kauli mbiu hupelekea falsafa kufanya kazi iliyokusudiwa. Taifa hili huendeshwa na kauli mbiu tu tangu Mkapa hadi leo. Natamani kuiona dira ya taifa
 
Mkuu Rweye ndio maana nikaongelea uwekezaji katika tafiti, inatakiwa tuwe na maabara zetu kwa gharama zetu tuweze kutumia hiyo elimu ya mweupe kwa manufaa yetu. Tuna wasomi wengi tu ambao wanaweza kutoa mawazo mapya na si ya kukariri.
Lazima tukubali kuumia leo kwaajili ya kesho misaada inatutia ulemavu
 
Last edited by a moderator:
Na....tutazunguka hapa hapa tu.... hadi tuwe na dira. Nchi ni kama meli inayoelea kwenda bandari fulani. Kama huna dira ya kuelekea huko utafikaje? Sisi hatuna dira wala bandari. Tutabaki kutatua vitatizo vidogo vidogo tu ajapo mtu kama JPM.
 
Michango yenu ni muhimu katika dhana hii ya kuwa na siasa ambayo ni dira inayoliongoza taifa.

Kama nyongeza, pana umuhimu wa kuasili sera ya uhurukweli kuwa ndiyo sera ya taifa: katika historia ya binadamu katika dunia hii, mara chache falme au mataifa yaliyoamua kutumia uhurukweli kwa wananchi wao, mataifa hayo yalipiga hatua kubwa sana za maendeleo. Kwa kuchagua siasa hiyo pia kutamwezesha Rais Magufuli kuepuka 'kubambikiziwa inshu' na warasimu wanaomsaidia kazi katika ngazi mbalimbali.

Road to hell is paved with good intentions
. Rais ana nia nzuri sana na sisi wananchi wake, ni kweli. Lakini warasimu wachache wanaweza kutumia nia yake hiyohiyo kujionyesha kwamba 'wanaenda na kasi ya Magufuli' lakini kumbe ni kwa maslahi yao binafsi. Mfano, Nyerere pia alikuwa na nia njema sana, lakini kadiri amri, sera na maelekezo yalivyokuwa yakishuka chini kwa wananchi, ndivyo yalivyozidi kutoholewa na warasimu tofauti na makusudio ya Nyerere mwenyewe.

Kuchagua siasa inayotoa mwelekeo wa utawala wake, utakuwa ni 'mwarobaini' wa kusaidia kuweka mambo yote wazi na kupunguza kuhujumiwa na warasimu. Wakati wa Nyerere mtu yoyote ambaye alikosoa utekelezaji wa jambo, alionekana hafai, anayebeza mamlaka ya Nyerere. Hata kama mtu huyo alionyesha mapungufu ya wale waliokuwa wakitohoa maamuzi ya Nyerere huku wakiimba 'Zidumu Fikra'.

Kuchagua uhurukweli kama mwongozo-mkuu wa mwelekeo wa taifa, kutakuwa na manufaa makubwa kwa watawala, warasimu na wananchi.
 
Back
Top Bottom