Tanzania Mama yangu

Dol

Member
Mar 24, 2021
58
115
Kuna watu kwa akili zao timamu wanafikili wanalidai sana taifa lao "Tanzania" kuliko jinsi taifa linavyowadai wao. Tanzania tangu enzi za ukoloni mpaka inajipatia uhuru wake kuna watu wamejitoa kwa jasho na damu mpaka kutufikisha hapa tulipo. Rejea harakati za kudai uhuru, azimio la Arusha, vita ya kagera, vijiji vya ujamaa, elimu ya kujitegemea, i can't mention them all because my time is limited.

Historia ni mwalimu mzuri sana lakini kizazi hichi hakijui thamani yake ndio maana imekuwa rahisi kusahau michango ambayo watu wengi waliitoa kwa ustawi wa taifa letu.

Nyerere alitufundisha mengi sana katika utumishi wake, pamajo na maandiko na vitabau vyake vizuri kujisomea. Unaweza kupasuka moyo ukisikia watu wanatapika kwamba wao wamefanya mengi kuliko watungulizi wao huu sio uungwana ni ujinga wa madaraka.

Nyerere alitufundisha kuwa cheo ni dhamama usikitumie kuonea watu lakini unaweza kuugua kisukari ukiona au kusikia vijana waliopewa madaraka jinsi wanavyofokea subordinates wao wakati sheria na taratibu zipo.

Ukisoma between the line utagundua kitu kuwa watu wanapotosha maana halisi ya uzalendo hususani kwenye kipindi cha Marehemu. Wenye macho tuliona mengi sana mpaka maprofesa waliotoka majararani. Hichi kinachotokea leo alikipanda mwenyewe kuponda, kukejeli na kuwananga watungulizi wake. Tumuache Mama yetu atuongoze vizuri kufikia malengo yetu.

Tuachane kabisa na utamaduni uliokuwepo ambapo watu walikuwa gizani na propaganda za wasakatonge walio eneza sifa kwa mtu mmoja kama amegundua dawa ya kifo. Aristotle aliwahi kusema " men cling to misfortunes to find the natural sweetness and happiness.
 
Tukipata katiba mpya tutazuia waganga njaa kuwa think tank ya taifa
Katiba mpya inahitajika Sana kipindi hiki sambamba na mageuzi ya elimu. Elimu yetu imeanguka sana fikilia jinsi watumishi wa umma wanavyo feel excuse kutimiza wajibu wao.

Fikikilia Nyerere amefanya mangapi mpake ameshinda vita ya kagera lakini alikuwa simple na alipenda kuitwa mwalimu.

Mwinyi na mkapa wamefanya mengi sana lakini hapakuwa na excuse, praising, wala chuki, as long as mzee wetu kikwete. Lakini mbegu aliyopanda JPM ni mbaya sana maisha yetu ni Bora kuliko vile alivyofikilia anafanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom