SoC03 Tanzania lini utanifanya nitabasamu?

Stories of Change - 2023 Competition

battle2

New Member
Aug 18, 2022
1
3
Tanzania nchi yangu nakupenda japo unanipa maumivu kila kukicha. Umejaliwa kila kitu cha kunifanya nitabasamu lakini tabasamu sipati. Nimekukosea nini? Niambie basi nielewe, kama ni samahani nikuombe. Vitu vingi umejaliwa vya kunifanya nijivunie uwepo wako lakini nabaki kulialia kila siku, matumaini yamepotea nakosa cha kujivunia. Au kwa vile hali yangu ni duni? Lakini mbona napambana kujikwamua ila wala hujali kunisaidia.

Kama ni mito mikubwa, maziwa makubwa, mabwawa na hata bahari unayo pia, iweje maji ya kunywa iwe shida mpaka nichote korongoni? Kulimojaa vyura na uchafu wa kila aina.

Nikiumwa tumbo, hospitali nayo ipo mbali. Basi nijikongoje kwenye zahanati ya kijiji, napo foleni ni kubwa, watu wamejazana wanasubiri matibabu. Loh! Kumbe mhudumu wa afya ni mmoja, nitatibiwa leo kweli? Tatizo ni lipi haswa? Mbona mtoto wa jirani kahitimu utabibu tokea mwaka juzi lakini bado yupo nyumbani hajaajiriwa anawasaidia wazazi wake kwenye kilimo.

Walau kwenye kilimo mmetukumbuka na ruzuku kwenye pembejeo japo mazao bado ni duni. Hatuna elimu wala ushauri kwenye kulima, Bwanashamba na bishamba hawaonekani. Hivi wapo kweli au ilikua kwa zama hizo tu. Nachoka zaidi nikiambiwa kilimo ni uti wa mgongo wa nchi, mbona kama kilimo kimetupwa mkono, tunalima kimazoea tu bila ushauri wowote.

Mashuleni nako nasikia waalimu wachache, madarasa hayatoshi vitabu navyo hakuna, wanafunzi watafaulu kweli? Mtaani wahitimu wa ualimu wamejazana hawana la kufanya, wanaambiwa wajiajiri kwani tatizo la ajira ni duniani kote. Wanaowaambia wajiajiri nao wanazeekea maofisini wawachie na wao basi wapate japo mitaji ya kujiajiri. Ila pia nabaki kujiuliza hivi huko duniani kwenye tatizo la ajira kuna upungufu wa watumishi kwenye sekta za umma? Nakosa jibu.

Ni pesa za kuwalipa zimekosekana, Ila mbona nasikia wewe ni tajiri? Una madini ya kila aina, mbuga za wanyama na vivutio vya utalii vya kila aina. Kwani hii pesa inayopatikana huko unaipeleka wapi? Maana nasikia una madeni kila kona na bado hukomi kukopa. Kama unaweka akiba tujuze basi walau tupate matumaini ya baadae.

Nilijua pesa hizo zitanisaidia ila ndio kwanza unaninyonya mpaka kidogo nilichonacho. Kwenye elimu kidogo umetupa ahueni japo mazingira ya shuleni magumu. Ila kwenye afya unanikamua haswa, umeme nako mpaka nimeshindwa kuunganisha nyumbani, maji siyaoni. Kwani unafanya biashara kwamba unahitaji faida? Mimi nakusaidia lakini sipati msaada kwako, nikisema nianzishe biashara japo ndogo unanishika shati nikugawie ninachopata kabla hata biashara haijasimama, unanikatisha tamaa kwakweli. Nakuchangia kwa kila ninachopata kwani unazipeleka wapi mbona sioni matumizi yake.

Ila niliambiwa waliopo kwenye ‘system’ wanazifaidi, hivi ni kweli? Maana wakipoteza mabilioni wanaambiwa walipe faini milioni, Inashangaza. Wakati juzi kijana wa kijiji cha pili kahukumiwa miaka 30 jela kwa kuiba kuku, kwakweli inawazisha na kuhuzunisha.

Wanaolalama wanaambiwa sio wazalendo, kwani uzalendo ni kuvumilia maumivu? Basi tuyafaidi wote matunda yako sio kuchagua wachache wa kuyafaidi. Tusipoyafaidi yako basi walau tuyafaidi yakwetu, na sio kuwafidisha nayo pia haohao wachache. Wakiwa na shida na sisi wanatunyenyekea wakituaminisha watatutatulia shida zetu tukiwatatulia zakwao. Tukiwasaidia wanajisahaulisha matatizo yetu na tukilalama tunaonekana sio wazalendo.

Masaa nayo yanasonga homa nayo inanizidia, hatimaye ni zamu yangu ya kufika kwa daktari. Namuelezea tatizo langu daktari bila kunipima ananiandikia dawa. Kumhoji anasema vifaa hakuna, hata hivyo dawa pia hakuna inabidi nikanunue mjini, sitafia njiani kweli? Kutokana na hizi barabara zisizopitika kwa magari? Yananijia mawazo mbona wakubwa wanatembelea magari ya kifahari na siye huku tunateseka, hivi wanayafahamu haya kweli? Huenda hawayafahamu kama wangeyafahamu basi wangeyashughulikia haya.

Kwa ghazabu narudi nyumbani naamua kutumia mitishamba, ila nisijekuambiwa naharibu mazingira kwakua nitakausha miti. Pia tunaambiwa tupunguze matumizi ya kuni na mkaa kwakua tunaharibu mazingira. Tutatumia nini? Gesi ipo juu ila ni wewe unamiliki ni kwanini sasa bei inatisha hivi? Kwa hali hii mazingira yatapona kweli?

Itabidi nimuhusie mwanangu ili walau apambane umchague aingie kwenye ‘system’ yako. Nasikia waliopo huko unawalipa pesa nyingi sana pia unawahudumia kila kitu, na hata kuwatoza ili wakuchangie hufanyi hivyo. Wanatumia za kwetu hata wasipofanya la maana, wamesahau hata kututetea wamebaki kutakandamiza.

Ila si unazeeka Tanzania, miaka 62 sio kidogo! Ila mbona unapambania mambo yaleyale! Inashangaza maji, umasikini, miundombinu (barabara), afya, elimu na ufisadi kila mwaka. Ni lipi umekamilisha? Nijuze basi walau nifarijike, nijiunge kutokomeza mengine pamoja. Basi pambania mojamoja kwanza huenda mengi yanakuchanganya. Mbona wengine mliokua sawa leo wapo mbali sana, wanashindana kwenye ulimwengu wa teknolojia, ni lini wewe utafika huko? Au sio malengo yako?

Tanzania nchi yangu nifanye nitabasamu, hata kama sina cha kujivunia basi nifanye nijivunie uwepo wako. Kwanini unatutesa wengi ili wafaidi wachache, wakati wanaweza kujibana ili walau na sisi tupate ahueni. Umoja wetu upo wapi? Wengine wanacheka, wengine wanalia. Anayecheka anamuona anayelia anadeka japo naye hataki kuvaa viatu vya wanaolia. Tanzania nchi yetu, tumechoka kulia, tufanye walau tutabasamu kidogo.
1669363812704-png.2427093
Raia wakituliza kiu (Chanzo cha picha: Jamiichek)
 
Wananchi wapewe elimu namna ya kusafisha maji machafu kuwa masafi na salama kwa kutumia mkaa
 
Usijari changamoto zote hizi zinaenda kuisha soon, chini ya raisi wetu mpendwa mama SAMIA , tuungane kwa pamoja kufanya kazi kwa bidii na kujituma, ili kuipunguzia mzigo serikali yetu

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom