Tanzania kuuza gesi katika soko la dunia

Tanzania kuuza gesi katika soko la dunia

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,952




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta Ewura Felix Ngamlagosi.

Tanzania ina gesi asilia ya kujitosheleza na ya ziada na hivyo inaangalia namna ya kuiuza gesi hiyo katika soko la dunia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta Ewura Felix Ngamlagosi jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa sekta ya gesi uliondaliwa na mamlaka hiyo.

Ngamlagosi amesema mazungumzo yanaendelea kwa sasa kati ya serikali na wadau mbalimbali kutafuta namna bora na wapi pa kuwekeza katika viwanda vya kusindika gesi na kuipeleka katika masoko ya dunia.
 
Akamdanganye yule mshamba mwenzie wa pale shinyanga sio sisi!
 
Ameona aongee ili asinuke mdomo. Hiyo gas tuliyoambiwa tumegundua mpaka mataifa ya nje yanatuonea wivu kila siku bei yake iko juu. Yaani ni upuuzi mtupu, huwa najiuliza kama sisi wenyewe hatuoni faida yake hayo mataifa ya nje yatatuoneaje wivu?
 
Nashauri Serikali ''Boresha Kwanza Soko la nyumbani Tengeneza miundombinu Rafiki kwa watanzania kwanza wapate nishati Hyo kwa bei nafuu ndio Muanze Kuangalia Soko La nje, Kumbuka kuna watanzaia Bado wanatumia, ''Koroboi" AKA taa za mafuta alafu Unataka Kuuza Gesi Nje, mmh Mtanzania kwanza Alfu Wengine Baaadae..
 
Kwani hilo soko la dunia limejegwa wapi!? Mkazi mmoja wa Mwanza alikuwa anasema eti 'Rock City Mall' ndilo soko la Afrika Mashariki!
 
Opposeeverything.com/ukuta
Mpaka sasa Tz bado tunateketeza misitu kwa mkaa, hio gas haifaa hata mqtumizi ya ndani ili angalau ipatikane na kwa bei nafuu ili kila mtu amudu. Bado tunakata miti, leo hio gas ikauzwe nje ya nchi??
Haitakuwa na maana, fanyeni kwanza ipatikane hapa nchini kwa wingi na kwa bei bafuu kisha ndio muwaze soko la nje.
 
Mpaka sasa Tz bado tunateketeza misitu kwa mkaa, hio gas haifaa hata mqtumizi ya ndani ili angalau ipatikane na kwa bei nafuu ili kila mtu amudu. Bado tunakata miti, leo hio gas ikauzwe nje ya nchi??
Haitakuwa na maana, fanyeni kwanza ipatikane hapa nchini kwa wingi na kwa bei bafuu kisha ndio muwaze soko la nje.
OK. Tutasubiri wananchi wote wawe na uwezo wa kutumia gas majumbani mwao ndipo tuwaze kuuza ili kukuza pato la taifa na kutoa huduma nyingine za kijamii
 
Mafisadi hayataki Taifa linufaike! Hiyo kauli imewakata maini kabisa! Yaani yanatamani hiyo gesi ingekua yao na familia zao!
 
Anaota huyu nn, gesi nchini haijatosha wala hakuna mikoani anaongea utumbo, viwanda vya gesi hakuna bado alafu anasema kuna gesi ya kutosha, upuuzi kabisa
 
Gesi ipi sorry, hii ya Mtwara msimbati si mkataba unasema yote inaenda China kufidia Mkopo wa kujengewa bomba la gesi? Au phase iii?
 
Magomeni hakuna anayejua tuna gesi!

Hivi hawa watu wanapatikana kwa vigezo gani, wana elimu gani !
Yaani tumasikini hadi mtu kama huyu anakuwa mkurugenzi!
 
Mafisadi hayataki Taifa linufaike! Hiyo kauli imewakata maini kabisa! Yaani yanatamani hiyo gesi ingekua yao na familia zao!


Taifa ni nani?Bibi yako kule kijijini anayenusurika kuuwawa kwa kudhaniwa ni mchawi kwa sababu ya kuwa na macho mekundu kutokana moshi unaosababishwa na matumizi ya jiko la kuni tangu alipokuwa binti mdogo amenufaikaje na hiyo gesi?Au yeye si sehemu ya Taifa hili?

Kama 95% ya watanzania hawajawahi kutumia hiyo gesi unayosema inalinufaisha Taifa,utasikilizaje ngonjera za serikali kuuza gesi nje ya nchi wakati wakati wananchi wenyewe hawaitumii kutokana na ghalama zake kuwa juu?Kama gesi ni maendeleo kwa Taifa,kwa nini hadi leo Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ghalama kubwa za Umeme wakati Taifa lina gesi ambayo inazalisha Umeme lakini Umeme umeendelea kuwa juu?

Hao mafisadi wasiopenda Maendeleo ya Taifa unaowasema hapa si kuna mahakama yao iliundwa,wakamateni muwahukumu wanyongwe,mbona hadi leo tunaambiwa mahakama hiyo ina kesi moja tu tena ya uvuvi haramu?Kamateni hao mafisadi wanaowazuia msiuze gesi nje ili walau majaji na watumishi wa mahakama ya mafisadi wawe na kazi za kufanya badala ya kulipwa mishahara ya bure huku mahakama ikikosa kesi za kusikiliza na kuishia kuwa na kakesi kamoja tu ka uvuvi haramu.
 
Back
Top Bottom