Tanzania Kusamehewa Madeni na Brazil!

Tanzania Kusamehewa Madeni na Brazil!

Mtu zkikukopesha halafu ukashindwa kulipa akaamua kukusamehe ni dharau sana ..n hasa mtu huyu akiwa mwanamke.....hii ni kwa mujibu wa kabila letu
 
Sio kweli kwamba hiyo ni katika kuimarisha uhusiano wake na nchi 7 za kiafrika bali ni katika kutengeneza competitive edge to be the partner to give priority in Gas Industry! Waache ujinga wao wa kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa; waseme tu "our aim is be good partners in business" so, tunafuta madeni yote ya nyuma na tunaanza upya! Wenye akili zao wataelewa tu.

Ni kweli kabisa mkuu. Meli lao (Wabrazil) liko hapa nchini likiendesha utafutaji wa mafuta na gesi. Pia walishaonyesha interest ya kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme wa hydro huko Selous katika bonde la mto Rufiji. Akili kumkichwa.
 
Kwanini watufutie madeni. Hawajui kuna watu wameweka fedha nyingi zisizo na kazi Uswisi!
 
Brazil imetangaza kuwa itafutilia mbali au kuwa na makubaliano mapya kuhusu madeni inayozidai nchi za Afrika ambayo yanakisiwa kuwa dola milioni 900.

130526043904_brazilian_president_rousseff_304x171_afp_nocredit.jpg

(Rais wa Brazil Dilma Rousseffalitoa matamshi yake katika mkutano wa AU nchini Ethiopia)

Miongoni mwa nchi 12 zilizo kwenye orodha ya mataifa yanayodaiwa ni pamoja na Congo-Brazzaville yenye uitajiri mkubwa wa mafuta na gesi, Tanzania ambayo hivi karibuni itaanza kuchimba gesi pamoja na Zambia

Wadadisi wanahisi kuwa hii ni njia mojawapo ya Brazil kutaka kukuza uhusiano wa kiuchumi kati yake ambayo ni ya saba kwa ukubwa kiuchumi na Bara la Afrika.
Taarifa rasmi zinaonyesha kuwa uhusiano wa Brazil na bara la Afrika umeongezeka mara tano katika mwongo mmoja uliopita.

Tangazo hili, lilitolewa wakati wa ziara ya tatu kwa miezi mitatu ya rais wa Brazil Dilma Rousseff,aliyehudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika nchini Ethiopia.

"takriban madeni yote huenda yakafutwa , '' alisema msemaji wa Rais Rousseff Thomas Traumann.
"ili kukuza uhusiano kati ya Afrika ni muhimu kwa sera ya kigeni ya Brazil."
Aliongeza kuwa nyingi ya madeni hayo yaliongezeka miaka ya sabini na kuwa kulikuwa na mazungumzo kuyahusu wakati huo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Brazil, alisema kuwa baadhi ya nchi huenda zikafaidika na makubaliano mazuri kuhusu namna ya kulipa madeni hayo huku muda wa kuyalipa ukiongezeka.
Congo-Brazzaville, inadaiwa dola milioni 352 ikifuatiwa na Tanzania inayodaiwa dola milioni 237 Zambia nayo ikidaiwa dola milioni 113.4.
Nchi zingine zitakazofaidika ni pamoja na Ivory Coast, Gabon, Guinea, Guinea Bissau, Mauritania, DRC, Sao Tome and Principe, Senegal na Sudan.
Brazil imekuwa ikiimarisha uhusiano wake wa kibiashara na Afrika, kitovu cha madini kama sehemu ya kile kinachojulikana kama ushirikiano wa kanda ya Afrika Kusini.
Kampuni nyingi za Brazil huekeza sana katika sekta ya mafuta na madini na zimekuwa zikifanya miradi mikubwa ya miundo mbinu barani humo.

source:Brazil kufuta madeni ya Afrika - BBC Swahili - Habari
 
habari njema sana kwetu ila ni aibu na fedhea kwa kimataifa.
 
nngu007 wewe ni kunguru,tena kunguru asie na mabawa..

Umeona Ulivyo KILAZA; ZEZETA.. Unatetea kitu usichokijua sababu unafaidika na serikali ya kifisadi Unaamua kutukana watu kuwa ni kunguru... ndio Maana ELIMU DUNI...

F.Y.I.... TANZANIA is among twelve African countries to benefit from the decision by Brazil to cancel or restructure almost 900 dollars worth of debt. Most of the debt was accumulated in the 1990s and had been renegotiated before. A spokesman for Brazil's Foreign Ministry told Efe news agency that the debt restructuring for some countries would consist of more favourable interest rates and longer repayment terms.
Tanzania owes Brazil a total of 237million dollars

*** PENDA NCHI YAKO; Jua Ni nani tunamkopa na ni kiasi gani; THAT's YOUR RIGHT... Tusiwe Mambumbumbu tunaamini Watu wasioweka hiyo MIKATABA in a BLUE PRINT WHITE PAPER; Sasa utakuwa unawafanyia kazi wadeni mpaka una Miaka 100??? --- we need to FIGHT for TRANSPARENCY in OUR GVT... sio uwe kama KUNGURU asie na MABAWA...
 
unaspin nini? sema tu nyerere alikopa hilo deni. acha kumislead watu, ---- we.
 
unaspin nini? sema tu nyerere alikopa hilo deni. acha kumislead watu, ---- we.

Unaona MLIVYO FUNDISHWA CHUKI? Wakati wa NYERERE BRAZIL haikuwa DEMOCRATIC ilikuwa inatawaliwa na Madikteta wa KIJESHI toka 1960 hadi 1985 wakati wa DEMOCRACY kuanzishwa baada ya kufa kwa USSSR

Kwahiyo Wanajeshi Makatili ndio waliokuwa wanaiongoza Brazil akina
Emilio Medici; Ernesto Geisel; João Figueiredo - ni wa Mwisho Mwaka 1985

Utataka utuambia NYERERE alikopa zaidi ya Jakaya Kikwete... it is a SHAME!!!

CHUKI ITAWARUDIA...
 
Inawezekana hizo pesa zikawa ni za ujenzi wa barabara,kwa kiwango cha lami toka Morogoro kwenda Dodoma,mradi uliofanywa na kampuni moja ya Brazil,kwenye miaka ya 80.

Kwa kuwa najua deni hilo serikali yetu ilishindwa ksbisa kulilipa.

Ni sawa kabisa, mkopo huo tulipewa ili uende kujenga hiyo barabara lakini kama unakumbuka wakti ule hasa baada ya vita tulikuwa na njaa kishenzi kwahio pesa ile ikatumika kwenye mambo mengine, si unakumbuka foleni kwenye maduka ya kaya na ugali wa Yanga?

Deni lililokopwa lilikuwa ni dola milioni 49 na tukashindwa kulilipa kabisa kiasi cha deni hilo kukua mpaka kufikia hizo dola milioni 240 kutokana na riba na adhabu kwa kushindwa kulipa.

Tanzania inabanwa kwelikweli na madeni na kusema ukweli nchi yetu ina madeni kila kona ingawa hata mzee Mkapa wakati wa uongozi wake aliwahi kusema amejaribu kulipa kiasi cha madeni hayo kwa nchi mbalimbali zinazotudai.
 
Back
Top Bottom