Tanzania Kusamehewa Madeni na Brazil!

Tanzania Kusamehewa Madeni na Brazil!

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,978
Ni la $237m/- katika juhudi za nchi hiyo kuimarisha uhusiano wake na nchi 12 za kiafrika ikiwemo Tanzania.

Source: http://m.bbc.co.uk/news/world-latin-america-22669331

Brazil has announced that it will cancel or restructure almost $900m (£600m) worth of debt with Africa.

Oil- and gas-rich Congo-Brazzaville, Tanzania and Zambia are among the 12 African countries to benefit.

The move is seen as an effort to boost economic ties between the world's seventh largest economy and the African continent.

Official data in Brazil show that its trade with Africa has increased fivefold in the past decade.

The debt announcement was made during the third visit in three months to Africa by Brazil's President Dilma Rousseff, who attended the African Union summit in Ethiopia.

'Strategic'
"Almost all (aid) is cancellation," Ms Rousseff's spokesman, Thomas Traumann, told reporters.

"To maintain a special relationship with Africa is strategic for Brazil's foreign policy."

He added that most of the debt was accumulated in the 1970s and had been renegotiated before.

A spokesman for Brazil's Foreign Ministry told Efe news agency that the debt restructuring for some countries would consist of more favourable interest rates and longer repayment terms.

Congo-Brazzaville owes the most to Brazil - $352m - followed by Tanzania ($237m) and Zambia ($113.4m).

The other countries to benefit are Ivory Coast, Gabon, Guinea, Guinea Bissau, Mauritania, Democratic Republic of Congo, Sao Tome and Principe, Senegal, and Sudan.

Brazil imetangaza kuwa itafutilia mbali au kuwa na makubaliano mapya kuhusu madeni inayozidai nchi za Afrika ambayo yanakisiwa kuwa dola milioni 900.

130526043904_brazilian_president_rousseff_304x171_afp_nocredit.jpg

(Rais wa Brazil Dilma Rousseffalitoa matamshi yake katika mkutano wa AU nchini Ethiopia)

Miongoni mwa nchi 12 zilizo kwenye orodha ya mataifa yanayodaiwa ni pamoja na Congo-Brazzaville yenye uitajiri mkubwa wa mafuta na gesi, Tanzania ambayo hivi karibuni itaanza kuchimba gesi pamoja na Zambia

Wadadisi wanahisi kuwa hii ni njia mojawapo ya Brazil kutaka kukuza uhusiano wa kiuchumi kati yake ambayo ni ya saba kwa ukubwa kiuchumi na Bara la Afrika.
Taarifa rasmi zinaonyesha kuwa uhusiano wa Brazil na bara la Afrika umeongezeka mara tano katika mwongo mmoja uliopita.

Tangazo hili, lilitolewa wakati wa ziara ya tatu kwa miezi mitatu ya rais wa Brazil Dilma Rousseff,aliyehudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika nchini Ethiopia.

"takriban madeni yote huenda yakafutwa , '' alisema msemaji wa Rais Rousseff Thomas Traumann.
"ili kukuza uhusiano kati ya Afrika ni muhimu kwa sera ya kigeni ya Brazil."
Aliongeza kuwa nyingi ya madeni hayo yaliongezeka miaka ya sabini na kuwa kulikuwa na mazungumzo kuyahusu wakati huo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Brazil, alisema kuwa baadhi ya nchi huenda zikafaidika na makubaliano mazuri kuhusu namna ya kulipa madeni hayo huku muda wa kuyalipa ukiongezeka.
Congo-Brazzaville, inadaiwa dola milioni 352 ikifuatiwa na Tanzania inayodaiwa dola milioni 237 Zambia nayo ikidaiwa dola milioni 113.4.
Nchi zingine zitakazofaidika ni pamoja na Ivory Coast, Gabon, Guinea, Guinea Bissau, Mauritania, DRC, Sao Tome and Principe, Senegal na Sudan.
Brazil imekuwa ikiimarisha uhusiano wake wa kibiashara na Afrika, kitovu cha madini kama sehemu ya kile kinachojulikana kama ushirikiano wa kanda ya Afrika Kusini.
Kampuni nyingi za Brazil huekeza sana katika sekta ya mafuta na madini na zimekuwa zikifanya miradi mikubwa ya miundo mbinu barani humo.

source:Brazil kufuta madeni ya Afrika - BBC Swahili - Habari
 
Ni la $237m/- katika juhudi za nchi hiyo kuimarisha uhusiano wake na nchi 12 za kiafrika ikiwemo Tanzania.

Source: BBC News - Brazil 'to write off' almost $900m of African debt
Sio kweli kwamba hiyo ni katika kuimarisha uhusiano wake na nchi 7 za kiafrika bali ni katika kutengeneza competitive edge to be the partner to give priority in Gas Industry! Waache ujinga wao wa kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa; waseme tu "our aim is be good partners in business" so, tunafuta madeni yote ya nyuma na tunaanza upya! Wenye akili zao wataelewa tu.
 
Kumbe tunadaiwa mpaka na Brazil?
Serikali zetu kiboko wewe....yaani walikata anga walikata anga, from Dar to Nairobi, Nairobi to London, London to Washington, Washington to Rio de Janeiro huku wakiwa wanahakikisha mkalimani wao wa lugha ya Kireno to English haiingii mitini! Njaa ikimkumba mwenye akili ndogo ni maafa si tu kwa ulimwengu bali katika mfumo mzima wa jua!
 
  • Thanks
Reactions: ilu
Huu ni wizi tu na watawala wetu,Petrobras ni kampuni ya kibrasil ambayo ipo kwenye mafuta na gesi hapa Tanzania, vituo vya mafuta vya Puma ni wabrazil hao hao wamenunua toka bp,ni business as usual na usanii na ghiliba za wizi wa Mali za taifa hili!!!
 
Kumbe tunadaiwa mpaka na Brazil?

Kuna umuhimu wa kuorodhesha madeni yote tunayodaiwa na nchi mbalimbali, yalikuwa ya nini, masharti yake yalikuwa yapi (kama yalikuwepo), yalisaidia nini, muda wa kulipa ulikuwa upi na namna ya kuyalipa! Kisha tu-deal na kuzuia madeni mapya, then tuanze upya!
 
  • Thanks
Reactions: ilu
Yani tunajua kukopa sisi aisee....mpaka raha....
LAKINI nadhani kukopa ni njia nzuri ya kufanya biashara...
hawa wazungu ukienda ukamwambia nina kuku nataka nikuuzie,anakataaa
Dawa unakopa kwake,halafu akija kukudai unamwambia nitakulipa KUKU....
Hapo ndio inatakiwa uwe mjanja wa kuhakikisha KUKU unaomlipa ni angalau thamani sawa na ulichokopa.....ukihakikisha hilo liko sawa......KOPA KOPA mpaka MAKOPE yaone WIVU
 
Kuna umuhimu wa kuorodhesha madeni yote tunayodaiwa na nchi mbalimbali, yalikuwa ya nini, masharti yake yalikuwa yapi (kama yalikuwepo), yalisaidia nini, muda wa kulipa ulikuwa upi na namna ya kuyalipa! Kisha tu-deal na kuzuia madeni mapya, then tuanze upya!

Wazo zuri sana hili la kupelekwa bungeni,kuitaka serikali ifanye hvyo!!!2kianzia madeni makubwa.
 
Kuna umuhimu wa kuorodhesha madeni yote tunayodaiwa na nchi mbalimbali, yalikuwa ya nini, masharti yake yalikuwa yapi (kama yalikuwepo), yalisaidia nini, muda wa kulipa ulikuwa upi na namna ya kuyalipa! Kisha tu-deal na kuzuia madeni mapya, then tuanze upya!

It is a good suggestion which is feasible only after a sane person takes the office of the PRESIDENT!! At the moment with Vasco Dagama still in office it cannot happen. Mpende au msipende ukweli ndio huo!
 
Rais wa Brazil amesamehe deni million 230 kutoka Tanzania duh Nilikuwa sijui hili hizi hela zilikopwa lini na zilitumika kufanya nini?

Naomba msaada.
 
Raid wa Brazil amesamehe deni million 230 kutoka tanzania duh Nilikuwa sijui hili hizi hela zilikopwa lini na zilitumika kufanya nini?

Naomba msaada.

Kwanza ni nina RAID wa Brazil???

Kama Unavyofahamu Serikali yetu ya AWAMU ya NNE inapenda MAENDELEO kwa MIKOPO - Toka BRAZIL
1. Wanajenga Mradi wa Mabasi ya kwenda KASI... Contractors pia ni Wabrazil
2. Kutafuta GAS Maeneo ya NCHI kavu kwa USHIRIKIANO na TPDC - PETROBAS ni Brazilian OIL and GAS company
3. Tumeanzisha UBALOZI BRASILIA, BRAZIL haujui Majengo kama tuliyalipia yote - tunavyopenda KUKOPA
4. Rais na kundi kubwa akiwemo MICHUZI walitembelea BRAZIL haujui ni MIKATABA gani tuli-sign kwa MIKOPO

*** Serkiali ya AWAMU ya NNE ni WAPENZI wa KUKOPA na TUNAPATA sababu --- Tukisema TUNA URANIUM kiasi GANi kila mtu anaweweseka na ilivyo na HIGH GRADE; Au GAS na hapo license tulizotoa kuchimba ni chache zaidi ya MOZAMBIQUE...
 
Raid wa Brazil amesamehe deni million 230 kutoka tanzania duh Nilikuwa sijui hili hizi hela zilikopwa lini na zilitumika kufanya nini?

Naomba msaada.

Samahani nilimaanisha rais wa brazil.Dah Ahsante sikujua hii serikali
 
Kwanza ni nina RAID wa Brazil???

Kama Unavyofahamu Serikali yetu ya AWAMU ya NNE inapenda MAENDELEO kwa MIKOPO - Toka BRAZIL
1. Wanajenga Mradi wa Mabasi ya kwenda KASI... Contractors pia ni Wabrazil
2. Kutafuta GAS Maeneo ya NCHI kavu kwa USHIRIKIANO na TPDC - PETROBAS ni Brazilian OIL and GAS company
3. Tumeanzisha UBALOZI BRASILIA, BRAZIL haujui Majengo kama tuliyalipia yote - tunavyopenda KUKOPA
4. Rais na kundi kubwa akiwemo MICHUZI walitembelea BRAZIL haujui ni MIKATABA gani tuli-sign kwa MIKOPO

*** Serkiali ya AWAMU ya NNE ni WAPENZI wa KUKOPA na TUNAPATA sababu --- Tukisema TUNA URANIUM kiasi GANi kila mtu anaweweseka na ilivyo na HIGH GRADE; Au GAS na hapo license tulizotoa kuchimba ni chache zaidi ya MOZAMBIQUE...

Yaani sasa mimeona jinsi serikali yetu onavyo
 
nngu007 wewe ni kunguru,tena kunguru asie na mabawa..
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana hizo pesa zikawa ni za ujenzi wa barabara,kwa kiwango cha lami toka Morogoro kwenda Dodoma,mradi uliofanywa na kampuni moja ya Brazil,kwenye miaka ya 80.

Kwa kuwa najua deni hilo serikali yetu ilishindwa ksbisa kulilipa.
 
Kwanza ni nina RAID wa Brazil???

Kama Unavyofahamu Serikali yetu ya AWAMU ya NNE inapenda MAENDELEO kwa MIKOPO - Toka BRAZIL
1. Wanajenga Mradi wa Mabasi ya kwenda KASI... Contractors pia ni Wabrazil
2. Kutafuta GAS Maeneo ya NCHI kavu kwa USHIRIKIANO na TPDC - PETROBAS ni Brazilian OIL and GAS company
3. Tumeanzisha UBALOZI BRASILIA, BRAZIL haujui Majengo kama tuliyalipia yote - tunavyopenda KUKOPA
4. Rais na kundi kubwa akiwemo MICHUZI walitembelea BRAZIL haujui ni MIKATABA gani tuli-sign kwa MIKOPO

*** Serkiali ya AWAMU ya NNE ni WAPENZI wa KUKOPA na TUNAPATA sababu --- Tukisema TUNA URANIUM kiasi GANi kila mtu anaweweseka na ilivyo na HIGH GRADE; Au GAS na hapo license tulizotoa kuchimba ni chache zaidi ya MOZAMBIQUE...
Hizo pesa tunazodaiwa na nchi ya Brazil,itakuwa ni pesa tulizokopeskwa na serikali ya Brazil,ili tujengee barabara kwa kiwango cha lami toka Morogoro kwenda Dodoma.

Kampuni iliyojenga barabara hiyo nishaikumbuka,ilikuwa inaitwa Ecisa,ambapo tulikuwa tukitamka Esiza.

Kambi yao kubwa ya ujenzi wa barabara hiyo,ilikuwa pale Dumila,ambapo hivi sasa kambi hiyo,imegeuzwa kuwa shule ya sekondari ya kutwa.
 
Back
Top Bottom