Tanzania kupata Bl 4.8 mara baada ya kukamilika kwa mradi wa Bomba la Mafuta toka Uganda.

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,556
3,838
Hayo yamesemwa na Waziri Muhongo akinukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo.

Inadaiwa kwamba, mara baada ya kukamilika kwa mradi huo Tanzania itakuwa inakusanya kiasi cha shilingi 24000 kwa kila pipa litakalopitishwa kwenye Bomba hilo ambazo ni sawa na Shilingi Bl 4.8 kwa pipa 200.000 zitakazopita kila siku.

Sambamba na hilo kunaajila kadhaa za vijana zitakazzopatika kutokana na uwepo wa Bomba hilo. Kama vile haitoshi mara baada ya mradi huo kukamilika yanatakiwa magari zaidi ya lakimoja kwaajili ya kusafirisha mapipa hayo toka Bandarini.

Kiukweli kama hali ndiyo hiyo basi naanza kugundua ni kwanini Wakenya wamerefusha midomo baada ya kuukosa mradi huo. Hakika mradi huo kama ukiendeshwa kiuadilifu basi ndani ya miaka kumi Tanzani itakuwa kama Ulaya.

Congratulations kwa Magufuli, Muhongo na Watanzania kwa ujumla kwa kupata Mradi huu.

BACK TANGANYIKA
 
Huu ni uongo,
mapipa ya kwenda wapi?
mafuta ni Ghafi na yatapakiw akwenye Meli na kwenda kwao.

Pia!
kama ni magarim, kwa nini tusijenge Reli tu.
 
Kweli mtanzania ni mtu wa mdomo mrefu. Si msubiri hata kazi ianze kabla hamjaanza kupiga kelele? Uvivu ni kitu kibaya sana. Unakaa chini unapanga mpango, unafanya kazi, unanunua magari na kujenga nyumba lakini bado ukiwa umekaa kitako kwenye jamvi! Waswahili walisema haja ya mja hunena, muungwana ni vitendo. Tujaribi kuwa waungwana.
 
Huu ni uongo,
mapipa ya kwenda wapi?
mafuta ni Ghafi na yatapakiw akwenye Meli na kwenda kwao.

Pia!
kama ni magarim, kwa nini tusijenge Reli tu.
Wee jamaa ni kilaza, kwani unadhani wanayamimina tu ktk bomba bila kujua ni mapipa mangapi? Ulitegemea uganda wasafirishe bure?
Wee bila shaka ni bavicha, kama sio ebu style up your brain!
 
Sambamba na hilo kunaajila kadhaa za vijana zitakazzopatika kutokana na uwepo wa Bomba hilo. Kama vile haitoshi mara baada ya mradi huo kukamilika yanatakiwa magari zaidi ya lakimoja kwaajili ya kusafirisha mapipa hayo toka Bandarini
Kama mafuta yanasafirishwa kwa bomba mapipa ya nini tena. uandishi huu ni aibu, kujua mafuta yanaujazo gani hakuhitaji mapipa tupu labda kama biashara hii inafanywa na chekechea.
 
Mimba ya wiki 2 watu mshanunua nguo kabisa za mtoto. Haya sasa subirini kukusanya mapato hewa kuanzia 2020
 
Back
Top Bottom