TANZANIA KUNUFAIKA MKONGO WA UMEME

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
View attachment 1025446

TANZANIA itanufaika kiuchumi kutokana na kuunganishwa katika mkongo wa umeme wa nchi tatu za Zambia, Tanzania na Kenya (ZTK) utakaosaidia kuzalisha umeme wa ziada na kuuzwa kwa nchi zingine zenye uhitaji baada ya kutosheleza mahitaji ya ndani ya nchi.

Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Alexander Kyaruzi amesema kuwa lengo la kuunganisha Tanzania ambayo kwa sasa ina gridi ya taifa ambayo haijaungwa na nchi yoyote ya jirani zake ni kuiwezesha kuwa miongoni mwa nchi za kusini mwa Afrika zenye uwezo wa kuzalisha umeme zaidi ya mahitaji.

Aliyasema hayo jana Babati mkoani Manyara katika ziara ya wajumbe wa bodi ya Tanesco pamoja na Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk James Nzagi
kukagua kazi zinazofanywa na wakandarasi wa mradi huo pamoja na kukagua vifaa vilivyohifadhiwa katika vituo vya Kalpa Taru, Nangwa na uchimbaji wa mashimo ya kusimika nguzo za umeme.


Alisema nchi yoyote yenye uhitaji wa umeme inaweza kuchukua kwenye nchi nyingine yenye umeme zaidi au ina umeme wa bei nafuu pia kuwa na uwezo wa kuuziana umeme kwa nchi zilizounganishwa katika mradi wa ZTK.

“Mtu wa Namibia anaweza kununua umeme kutoka Ethiopia na ikapita kwenye miundo mbinu yetu ya umeme ambayo itakuwa na tozo fulani kwa kupitisha
umeme huo lakini na sisi tukihitaji umeme wa ziada popote pale tunaweza kuupata kirahisi,” amesema Kyaruzi.


Pia alifafanua kuwa mradi wa kufufua umeme wa Stieglers Gorge ukikamilika utaweza kutoa megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye mkongo wa ZTK na kuwezesha pia kuuza umeme nchi jirani za Kaskazini, Mashariki na Kusini mwa Afrika zenye uhitaji wa umeme.

Bodi hiyo inasimamia Tanesco na utendaji kazi wake wote kati ya miradi Tanesco inaendesha sasa hivi ni mradi wa Tanzania Kenya Interconnector (ZTK) ambao utekelezaji wake utaanzia Singida, Babati, Arusha, Namanga Kenya chini ya wakandarasi watatu mmoja kutoka Singida hadi Babati, mwingine kutoka Babati hadi Arusha na wa mwisho ni kutoka Arusha hadi Namanga.

Mradi huo wa Zambia, Tanzania Kenya Interconnector (ZTK) unatarajiwa kukamilika Juni 2020, ikiunganisha Tanzania (ambayo kwa sasa ina gridi ya taifa ambayo haijaungwa na nchi yoyote) na jirani zake.

“Ukiangalia nchi za Afrika hususani Kusini mwa Afrika, gridi zao zimeungana mfano Gridi ya Angola imeunganishwa na Namibia, Afrika Kusini imeungana na Lesotho, Swaziland, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe na Botswana pia nchi zilizo Kaskazini mwa Tanzania, Kenya Uganda na Ethiopia na zenyewe zimeungana.

” Mratibu wa Mradi ujenzi wa njia za kusarisha umeme (ZTK), Peter Kigaja alibainisha kuwa kila mwananchi atalipwa dia kwa ardhi aliyoiachia kuweka miundo mbinu ya umeme katika maeneo yatakayopita mkongo huo na kukaguliwa na Mthamini wa Serikali.

Kipande cha mradi wa ZTK upande wa Tanzania kina kilomita 414 na kilomita 96 upande wa Kenya kutoka Babati na kazi hiyo itaendelea baadaye katika kukamilisha kipande cha kilomita 624 kutoka Iringa kwenda Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga ili kuunganisha na nchi ya Zambia. Utekelezaji wa miradi hiyo unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Africa (ADB) pamoja na shirika la maendeleo la Japan (JICA) kwa gharama ya dola za kimarekani 258.
 
Back
Top Bottom