Tanzania Kumbe haina Mkataba halali hata mmoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Kumbe haina Mkataba halali hata mmoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Untwa, Jul 15, 2011.

 1. Untwa

  Untwa Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjadala wa Kipimajoto ITV, Mchangiaji anasema kwa mujibu wa katiba iliyopo, kila mkataba wa Jamhuri ya Muungano lazima upitishwe na Bunge, Sasa hii mikataba ya siri inatoka wapi?
   
 2. J

  J_Calm Senior Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uo ndio ukweli na watu wanakula kupitia hapo na kuwatishia watanzania kuwa mkataba hauguswi ili wazidikupokea ama kulinda makubaliano yaliyofikiwa binafsi. Tukae mstari wa mbele ili tuokoe taifa.
   
 3. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  well, mengi yataibuka mikataba mingi ya nchi hii ni kwa jinsi mawaziri wanavyotaka, stupid.....
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Chadema plse akina Lissu mabere zito mnyika dada Reggia tuanzie hapa. sasa tunajua katiba ilivunjwa kwenye hii mikataba feki. tuchukue hatua kuivunja hii mikataba feki na waliohusika wote washtakiwe
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pumba tupu, kuna mmoja anaongea ooh wanyama wanapelekwa mini serengeti dubai eti kakasirika! mbona hajasema ya London Zoo, New York Zoo na ma zoo mengine yote yanayonunuwa wanyama hapa? kaona ya Dubai tu? mambo mengine yanatia kinyaa.

  Mikataba Feki? wasikilizeni mkaivunje kama haijawatokea puani, si mliona wa Dowans, wa IPTL sas nendeni kwenye mingine halafu mtajuwa. Hamjifunzi? Nyerere alijidai hivyo hivyo kutaifisha mali za wanyonge, alipojaribu kutaifisha za wajanja kina Tiny rawlands alijuta kuzaliwa, na ujanja wake wote, mwenyewe alirudisha na kuomba msamaha, "nisameheni sirudii tena" na alipoichukuwa alisema "nikigeuka nyuma ntageuka jiwe" kikowapi?

  Msisikie porojo za wale watu waliokuwa wanazipiga pale ITV wote wale ni uchwara na hawajui wakisemacho. Ya Dowans ni cha mtoto. Uingie na mtu mkataba kisha wekeza mabilioni yake halafu ujidai mkataba feki? weee, utakiona cha moto. Jaribuni, yale ya Dowans tuliwatahadharisha hamkusikia. Na sasa anzeni muone.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kweli akili ni nywele nadhani mwenzetu huna nywele. hivi unajiita mtu mzima kabisa kwa comments za kitoto namna hiii mweeee
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nimekupa mifano hai mitatu ambayo yote tulivunja mikataba na yote imetugeukia na inatutokea puani. Kuanzia wakati wa Nyerere na Tiny Rowlands kwa LONRHO, Mkapa kwa IPTL, Kikwete kwa Dowans.

  Sasa wewe lete hoja yako na nendeni mkaivunje mikataba mingine muone raha yake, au ngojeni mkichukuwa nchi muivunje mikataba yote muone raha yake.

  Na mwingine tumeona juzi juzi tu, majumba yale ya Oyster-bay yalivyobomolewa na sasa kiko wapi, yanatutokea puani, hayo yanaanza kujengwa na gharama zote za kuyajenga upya, muda wote yaliyosimama kujengwa, gharama za mali yote iliyoibiwa iliyopotea na mapato yote ya kodi yaliyopotea kuanzia yalipobomolewa na gharama zote za mahakama na mawakili Serikali ndio inalipa kwa fedha zangu na zako za kodi, kama unalipa kodi, kwa kuvunja mkataba. Nani alioshinda kesi? Au hujui?

  Umpe ruksa mtu wewe mwenyewe halafu umwambie navunja mkataba, vunja uone chako.

  Usilete pumba zako lete hoja zako au jibu hoja.
   
 8. k

  kajembe JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Pumbavu wewe!
   
 9. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,586
  Trophy Points: 280
  Hadi mama ya mikataba yote(articles of union) mashaka matupu.
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hao wanasheria wenu wa miaka hiyo ni ilaza kama wewe na fikra zako za ki CCM kama huna la kuchangia humu usituletee PUMBA!
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,590
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Wacha kupotosha soma Multinational Monitor, February 1980 uone mwanaume alivyokomaa na hata hao wakubwa wenyewe walikuwa wanajua Tanzanioa ni nini na nani , Nyerere hakua legelege kama viongozi wa leo walivyo
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uliza mkataba aliovunja nyerere na Lonrho wakili wake alikuwa nani? Mbona aligeuka nyuma?Hakuna wakili yeyote ataeshinda kwenye hii mikataba ya kibiashara, biashara si lelemama. Biashara haina siasa wala uzalendo. Leo mkijidai kuwasikiliza wanasiasa na porojo zao ndio wawe washauri wenu wa biashara basi mmepotea. Yatakuwa yaleyale ya nyerere. Leta hoja.
   
 13. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mikataba yetu mingi imejaa utata, haipo sawa coz rushwa imetawala!
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kukomaa peke yake haitoshi, huko kukomaa kwake kumeleta tija ipi? Si ndio hayo nnayosema mimi? Unakomaa kuvunja mikataba halafu inakugeukia na kukuumiza zaidi. Umepata faida gani?

  Kukomaa kwa nyerere na lonrho kumeleta faida gani? Mwishowe karudisha mali zao na gharama juu, kubwa sana tena. Na ndio tulichokifungia mikanda hicho. Msidanganywe kuwa tulifunga mikanda kwa vita ya Amin. Vita ya amin ililipiwa gharama zake na uingereza kama hamjui.
   
 15. Untwa

  Untwa Member

  #15
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kama tangu enzi za Mwalimu mikataba mibovu imewahi kuingiwa na kuigharimu nchi na mwalimu kwa kutambua hilo akasema 'mchukue mazuri na mabaya myaache', Kwa nini nchi inaendelea katika mikataba mibovu! ilhali madhara yake yanajulikana?
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna mikataba mibovu, tuna watu wana vichwa vibovu.

  Hivi wewe unakwenda kufunga mkataba na multibillion company na ka lawayer kako ka mtaa wa India unategemea nini?

  Kinachotakiwa ni kuwatumia watu waliopo huko huko kwa hao jamaa, sioni kwa nini hatuna washauri wa kuwaajiri waliobobea kutoka nje katika sehemu tulizokuwa weak?

  Mfano masuala ya umeme yametushinda hapo Tanesco, mimi nashaangaa Serikali kuingilia kazi za shirika ambalo limeshindwa badala kutafuta ufumbuzi wa kutatua matatizo yaliopo hapo Tanesco. Kama tatizo ni ununuzi, analetwa mtu aliobobea katika manunuzi kutoka nje ya Tanzania. Kama tatizo ni ku manage kitengo fulani amnaletwa aliebobea kutoka nje au simply monopoly inauliwa na unaweka wazi unaitangazia dunia kuwa sasa njooni muwekeze kwenye mume bila masharti, fuwa sambaza uza. Uone kama haijawa kama ya simu. Wakati wa Nyerere simu zilikuwa ghali ajabu ya mungu, tazama ilivyoondolewa monopoly, leo unaongea na dunia nzima kama upo Tanzania na bei wala huhisi.
   
 17. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  "bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi umepiga magoti" watu legelege waoga kama kina zomba hamstahili kuendelea kuishi !
   
 18. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Join Date : 27th November 2007
  Posts : 4,139
  Rep Power : 0

  Bwana kichefuchefu. Wewe umeangalia mkataba wako na waliokutuma kwenye JF. Huo ndio feki kuliko yote. Mr. 0 Rep Power since 2007 with 4139 posts!!!
   
 19. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hii style ya kuleta mgeni kila tunaposhindwa ni kichekesho!Kama vipi tuwaombe wamarekani(USA) watuazime rais Obama kwa muda wa miaka miwili tu mambo yawe msuwano.
   
 20. Untwa

  Untwa Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni uzalendo tu unaohitajika na siyo kila kitu anachoshindwa mtz mmoja basi ionekane wabongo wote hatuwezi kwa hiyo aletwe mwekezaji, baadaye tusipokuwa makini tutawekeza mpaka ikulu na familia zetu.
   
Loading...