Tanzania kuiuzia Umeme Afrika Kusini

Tanzania kuiuzia Umeme Afrika Kusini

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Tanzania itaiuzia Umeme Afrika Kusini kufuatia Nchi hiyo kukumbwa na msukosuko mkubwa wa nishati hiyo

Hayo yamebainishwa katika ziara ya Rais Samia nchini humo ambako mikataba mbalimbali ya Biashara imesainiwa

----
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema Afrika Kusini inafikiria kununua umeme kutoka nchini Tanzania ili kusaidia katika kutatua tatizo la nishati nchini humo.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano na Rais Samia Suluhu Hassan katika Majengo ya Muungano mjini Pretoria Alhamisi Machi 16, 2022 ikiwa ni sehemu ya ziara ya Kiserikali ya Rais Samia na kikao cha pili cha Tume ya Pamoja ya Afrika Kusini na Tanzania.

"Tulisema tulipotoa mpango wa utekelezaji wa nishati mwaka jana mwezi Julai ni kwamba moja ya mipango tunayoenda kuanza ni kupata nishati ya ziada kutoka kwa majirani zetu. [..] Tulikuwa tumenunua megawati 300 na sasa tulikuwa tunaenda kuongeza kiwango hicho hadi juu kidogo.

Nimekuwa nikizungumza na viongozi katika nchi mbalimbali, wanasema tuna ziada kidogo na tunaweza kukuuzia,” amesema Ramaphosa.
59%

Aidha, Rais Ramaphosa ameongeza kuwa ana imani kwamba mzozo wa nishati nchini Afrika Kusini hautazuia uwekezaji nchini humo.

Mkutano huo umeeleza azma ya Tanzania na Afrika Kusini katika kuimarisha uhusiano uliopo wa kisiasa na kiuchumi baina ya nchi hizo mbili pamoja na Tume ya Pamoja (BNC).

Swahili time.
 
Umbali kutokea Tanzania mpaka South Africa in 4,032.2 km (2,506.04 miles). Waya ya kusafirisha high-voltage kwa mile moja ni kati ya 1.7M USD - 5.3M USD, Tuchukue average lbd 2.3M USD, mkongo wa umeme unachukua kuanzia waya 3 mpaka 6, tuchukue average waya 4.

Cost ya waya pekeyake kutokea TZ mpaka SA ni ( 2,506.04 miles × 2.3M USD × 4) =
 
Tanzania itaiuzia Umeme Afrika Kusini kufuatia Nchi hiyo kukumbwa na msukosuko mkubwa wa nishati hiyo

Hayo yamebainishwa katika ziara ya Rais Samia nchini humo ambako mikataba mbalimbali ya Biashara imesainiwa

Source ITV Habari
Umeme huu huu tunaopimiwa kwa kijiko?? Mgawo kila siku??!! Hahahaha.....huu ni mzaha Wallah! Yale yale ya kuwaza kuuza chakula cha familia wakati hata watoto wako mwenyewe hawashibi!!!
 
Tanzania itaiuzia Umeme Afrika Kusini kufuatia Nchi hiyo kukumbwa na msukosuko mkubwa wa nishati hiyo

Hayo yamebainishwa katika ziara ya Rais Samia nchini humo ambako mikataba mbalimbali ya Biashara imesainiwa

Source ITV Habari
Atauza umeme kutoka wapi wakati wenyewe haututoshi? Labda atatoa zanzibar😂
 
😅😅😅😅😅😅😅😅 Heeeeee!

Ila wa south wanaiharibu nchi yao nzuri sana. Kweli watu weusi sisi ni noma!
 
Yaani maiti inataka kuchangia damu!?
JamiiForums-633895303.jpg
 
Umbali kutokea Tanzania mpaka South Africa in 4,032.2 km (2,506.04 miles). Waya ya kusafirisha high-voltage kwa mile moja ni kati ya 1.7M USD - 5.3M USD, Tuchukue average lbd 2.3M USD, mkongo wa umeme unachukua kuanzia waya 3 mpaka 6, tuchukue average waya 4.

Cost ya waya pekeyake kutokea TZ mpaka SA ni ( 2,506.04 miles × 2.3M USD × 4) =

Makubaliano ya itifaki ya pamoja ya SADC tayari iliainisha kila nchi mwanachama kujenga vituo vya kupokelea na kusafirisha umeme kwenye mipaka yake kutoka nchi moja kwenda nyingine na zoezi hilo lilishafanyika kwa baadhi ya nchi na nyingine zinaendelea, na hii itawezesha energy exchange baina ya nchi moja kwenda nyingine hivo hapo hakuna kitu cha ajabu kikubwa ni kusonga mbele tu
 
Back
Top Bottom