state agent
JF-Expert Member
- Jul 1, 2019
- 1,764
- 2,511
Ni baada ya kupeana ndege tausi then turudishiwa dhahabu hapo Jana
Mlipiga kelele sana kuuza ,serkali ikafunga masikia na kusema tutauza unga sio mahandi ila ndio dipromasia ina nguvu siku hizi
Tani million 1
Maendeleo hayana vyama
======
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa Serikali itaiuzia nchi ya Kenya mahindi tani milioni moja katika kipindi cha mwaka mmoja, baada ya msimu wa mvua kugoma nchini humo hali inayotishia kuwepo kwa upungufu wa chakula.
Ameyasema hayo leo Julai 25, katika kikao kilichokutanisha idara zilizo chini yake na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo wa Kenya, Hamad Boga pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu.
Amesema kuwa wamekubaliana kwa wiki ijayo watakutana na kufanya kikao kitakachozikutanisha idara zote za mapato na masuala ya viwango na ubora wa bidhaa kutoka nchi ya Kenya na Tanzania pamoja na sekta zote zinazohusika na mauzo ya chakula.
”Tumekubaliana na wenzetu kwamba mahitaji yao kwasasa ni Tani milioni moja, sasa hivi NFRA na Bodi ya mazao mchanganyiko wametuthibitishia kuwa wana uwezo wa kuhudumia hilo hitaji la tani milioni moja,”amesema Bashe
Aidha, hatua hiyo imekuja baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Kenya, Profesa Fred Segor, kusema mwaka huu wana changamoto ya hali ya hewa, kwa kuwa mvua haikunyesha ipasavyo.
Hata hivyo, Jana Julai 24, 2019, Rais John Magufuli katika mazungumzo yake na Rais Uhuru Kenyatta, alisema alipomtembelea nyumbani kwake Chato, alizungumzia hitaji la kununua mahindi kutoka Tanzania.
Huku wastaafu wananyimwa pension zao. Wafe njaa lakini chakula kiuziwe jirani! Serikali inawajali wanyonge wa nchi hii kweli?Ni baada ya kupeana ndege tausi then turudishiwa dhahabu hapo Jana
Mlipiga kelele sana kuuza ,serkali ikafunga masikia na kusema tutauza unga sio mahandi ila ndio dipromasia ina nguvu siku hizi
Tani million 1
Maendeleo hayana vyama
======
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa Serikali itaiuzia nchi ya Kenya mahindi tani milioni moja katika kipindi cha mwaka mmoja, baada ya msimu wa mvua kugoma nchini humo hali inayotishia kuwepo kwa upungufu wa chakula.
Ameyasema hayo leo Julai 25, katika kikao kilichokutanisha idara zilizo chini yake na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo wa Kenya, Hamad Boga pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu.
Amesema kuwa wamekubaliana kwa wiki ijayo watakutana na kufanya kikao kitakachozikutanisha idara zote za mapato na masuala ya viwango na ubora wa bidhaa kutoka nchi ya Kenya na Tanzania pamoja na sekta zote zinazohusika na mauzo ya chakula.
”Tumekubaliana na wenzetu kwamba mahitaji yao kwasasa ni Tani milioni moja, sasa hivi NFRA na Bodi ya mazao mchanganyiko wametuthibitishia kuwa wana uwezo wa kuhudumia hilo hitaji la tani milioni moja,”amesema Bashe
Aidha, hatua hiyo imekuja baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Kenya, Profesa Fred Segor, kusema mwaka huu wana changamoto ya hali ya hewa, kwa kuwa mvua haikunyesha ipasavyo.
Hata hivyo, Jana Julai 24, 2019, Rais John Magufuli katika mazungumzo yake na Rais Uhuru Kenyatta, alisema alipomtembelea nyumbani kwake Chato, alizungumzia hitaji la kununua mahindi kutoka Tanzania.
Sikuelewa vizuri sana kauli ya Bashe kuwa wakenya watanunua mahindi moja kwa moja toka kwa wakulima, no intemediaries, nkInchi yetu ya Tanzania inaweza kukuza uchumi wake kwa kasi sana kama itatilia mkazo mkubwa katika kulima cha zao la Mahindi.
Inchi yetu ya Tanzania inaweza kukuza uchumi wake kwa kasi sana kama itatilia mkazo mkubwa katika kulima cha zao la Mahindi.
Kama mahindi yatalilmwa kama zao la Biashara kikanuni na sh eria, na mavuno kuwa makubwa kiasi cha kuweza kuuza Afrika ya Mashariki yote hadi Sudani na Ethopia, kiasi cha pesa tutakachoingiza ni zaidi ya mazao yote kama pamba, korosho, chai n.k.
Tatizo kubwa tulilonalo ni mgando wa akili wa kuendelea kuliweka zao la mahindi kama zao la chakula na kwa hiyo kutolipa kipao mbele katika kuliendeleza.
Wakati wa uongozi wa hayati Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa, kila mkoa ulikuwa na ghala la kuhifadhia nafaka.
Maghala haya yaliuzwa karibu yote na hata baadhi ya vihenge vilivyojegwa Dar Es Saalam, Iringa na Arusha viliuzwa kwa watu Binafsi ambao wameyageuza maghala ya kuhifadhia mitumba ya nguo toka nje.
Vihenge navyo vinahifadhi ngano toka nje ya Inchi.
Tujiulize, ni kwa nini Kenya watuombe kununua Mahindi badala ya sisi kuwafuata na kuwataka kuja kununua mahindi yetu?
Sisi badala ya kulima zaidi na kuuza nje, tunapiga marufuku kusafirisha mahindi kwenda nje na kuwafanya wakulima kukosa soko la mazao yao au kupata bei ndogo.
Kilimo ni ajira kubwa sasa hivi Tanzania kwa hiyo zao la mahindi likiendelezwa watu wengi watapata ajira kwa kulima kwa wingi zao hili na kuuza Inchi za Nje.
Wastaafu wengi sasa hivi wanajishughulisha na Kilimo, lakini wanakata tama a kwa kukosa soko la mahindi au bei za mahindi kuwa za chini na kuwasababishia hasara.