Tanzania kuijibu Marekani, Uingereza

Tanzania kuijibu Marekani, Uingereza

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
24,150
Reaction score
56,463
Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema inalifanyia kazi tamko la pamoja la ubalozi wa Marekani na Uingereza linaloelezea wasiwasi wa kuzorota kwa haki za raia nchini.

Katika tamko hilo lililotoka leo Ijumaa Agosti 9, 2019 mabalozi hao wanaitaka Serikali kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kwa raia wake.

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Agustine Mahiga akizungumza na Mwananchi leo kuhusu tamko hilo amesema wameliona na wanalifanyia kazi.

Mwanadiplomasia huyo amesema wizara yake pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) watakutana kujadili tamko hilo na baada ya hapo Serikali itatoa msimamo.

“Baada ya kukaa kwa pamoja tutatoa taarifa ya Serikali kuhusu tamko hilo la pamoja,” amesema Balozi Mahiga aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Amesema anafahamu tamko hilo linatokana na tukio la hivi karibuni ambalo hakulitaja.
==========

My Take; Angalau Mahiga kajibu kidiplomasia angekuwa yule wangeambiwa Tanzania ni nchi huru wasituingilie.
 
Rais wa Rwanda alishawajibu vizuri sana hao jamaa kuhusu masuala ya haki za binadamu.
1. Kuwa Mwaafrika ndiye kinara wa haki hizo duniani.

2. Kuwa hao jamaa hawana moral authority ya kumfundisha Mwaafrika kuhusu haki hizo ambazo zinatawaliwa na mila na desturi.

3. Kuwa haki za binadamu za hao jamaa na ushoga, kutukana wakubwa zao na mambo mengine ambayo hayavumiliki kwa Mwaafrika. Mzungu anapaswa kujifunza kwetu katika masuala.ya haki za binadamu and not vice versa!

4. Kabendera kutumiwa na gazeti la Uingereza la Economist kuandika habari za kuleta machafuko kwa nchi yetu kwa malipo ya kampuni ya Uingereza ya Acasia, kamwe haliwezi kuvumiliwa na wala haliwezi kuwa kwenye haki za binadamu wa Kiafrika. Acasia wamekuwa wakimlipa Kabendera mabilioni ya pesa kwa shughuli hii baada ya kubanwa kwenye wizi wao wa makenikia. Lengo lao likiwa kuikomesha serikali ya Tanzania.

Huu ni uhaini unaopaswa kuzimwa kabla haujaleta madhara. Hichi ndicho serikali ilichofanya kwa kumkamata Kabendera na kumfikisha mahakamani. Pesa hizo za kigeni alizokuwa akilipwa Kabendera hazikulipiwa kodi ya serikali - alikuwa akilipwa kinyemela kama wanavyolipwa wanaotumikia vikundi vya kigaidi hususani Al Akaida. Hii kama siyo money laundering ni nini?

Suala la Kabendera liko mahakamani na hakuna mwenye haki ya kuingilia suala ambalo liko mahakamani, including hao mabalozi wa Uingereza na Marekani. It is a contept of court. Waache sheria zetu zichukue mkondo wake.Wasitake kuifanyia Tanzania kama walivyozifanyia nchi kama Libya.
 
Mkuu huyo ana stress ya kufa mtu. Alikuwa anamfuata Lowassa kila anapoenda sasa Lowassa amemkimbia njaa imekuwa kubwa sana. Pole Salary Slip !!
Pamoja na stress za mhusika nakukumbusha tu kwanba damu za Watanzania wenzenu jaribuni angalau ziwakinai sasa...
 
Back
Top Bottom