Tanzania kuacha kutoza VAT

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Kuanzia Januari mwakani, kodi ya ongezeko la thamani almaarufu VAT itaacha kutozwa kabisa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA.
Sosi: Magazetini, RFA.
 
Kiongozi inaonekana umefanya haraka kupost hii kitu.
VAT exemption kwa bidhaa zote au zile zinazalishwa Tanzania tu?

Kwa akili ya haraka wasipotoza VAT kwenye bidhaa zote serikali itapata wapi fedha?

Tia nyama kwenye post yako
 
vat exemption kwa bidhaa za kitanzania tu.wasiwasi wangu haya mapato yatatoka wapi?je kodi hii itahamishiwa kwenye bidhaa za nje au kwa wafanyakazi?nahisi kodi ya kichwa inarudi tena.
 
.....Nadhani hii ni kwa wageni tu ambao watakuwa wamenunua bidhaa mbali mbali nchini. Pale Airport kama wataweza kutimiza masharti yote ya kuweza kurudishiwa VAT waliyolipa wakati wakinunua bidhaa hizo, basi watarudishiwa. Mie uamuzi huu umenishangaza sana hasa ukitilia maanani hali mbaya ya kifedha ndani ya hii Serikali.
 
.....Nadhani hii ni kwa wageni tu ambao watakuwa wamenunua bidhaa mbali mbali nchini. Pale Airport kawa wataweza kutimiza masharti yote ya kuweza kurudishiwa VAT waliyolipa wakati wakinunua bidhaa hizo, basi watarudishiwa.

thanks mkuu
 
.....Nadhani hii ni kwa wageni tu ambao watakuwa wamenunua bidhaa mbali mbali nchini. Pale Airport kama wataweza kutimiza masharti yote ya kuweza kurudishiwa VAT waliyolipa wakati wakinunua bidhaa hizo, basi watarudishiwa.

Kitu kama hicho nimeona SA, ila hustle yake inakatisha tamaa, na bado hiyo pesa unayorudishia wanaitoza sijui kodi gani tena.

At the end of the day unalazimika kununua kitu hapo airport kama hutaki kusafiri na currency ya kigeni na kuja kuichange kwa hasara.

Ila kama umespend a lot, kidogo kuna kanafuu!
 
vat exemption kwa bidhaa za kitanzania tu.wasiwasi wangu haya mapato yatatoka wapi?je kodi hii itahamishiwa kwenye bidhaa za nje au kwa wafanyakazi?nahisi kodi ya kichwa inarudi tena.

Mafisadi nao kipato kitashuka
 
Kiongozi inaonekana umefanya haraka kupost hii kitu.
VAT exemption kwa bidhaa zote au zile zinazalishwa Tanzania tu?

Kwa akili ya haraka wasipotoza VAT kwenye bidhaa zote serikali itapata wapi fedha?

Tia nyama kwenye post yako

mi sielewi hayo makitu mwana.
Nimeandika kama nilivyosikia...
 
vat exemption kwa bidhaa za kitanzania tu.wasiwasi wangu haya mapato yatatoka wapi?je kodi hii itahamishiwa kwenye bidhaa za nje au kwa wafanyakazi?nahisi kodi ya kichwa inarudi tena.
Kwa kanuni za uchumi hii wanayofanya kufuta VAT kwa bidhaa za ndani ni moja ya njia za kuwapunguzia wananchi gharama za maisha. lakini wasi wasi wangu ni kuwa kutokana na udhaifu wa ukusanyaji wa mapato na kutokuwa waangalifu katika matumizi, kitakachofanyika hapa ni kusamehe upande mmoja na kuwaongezea mzigo wengine i.e wafanyakazi through PAYE. Hapo sidhani kama serikali itakuwa imetatua tatizo hili kwa sababu hao hao unaowapunguzia VAT kwenye bidhaa, ndio hao hao unawaongezea mzigo wa kodi. yaani ni sawa na kutoa kwa mkono wa kulia na kuchukua kwa mkono wa kushoto.
Na ninaamini kuwa uwezekano wa kuongeza PAYE ni mkubwa kwa sababu sijaona mikakati haya ya wizara ya fedha kupanua wigo wa kodi. Pia, tukumbuke kuwa Mkulo amefanya mabadiliko kwenye Finance Bill na kuanzia january, zile kodi korofi kwenye halmashauri kama vile kodi ya leseni, ambazo zilifutwa, zitaanza kutozwa tena. Sijui hiyo hatua ya kusamehe VAT italeta faida gani iwapo unaongeza gharama za biashara kupitia kodi nyingine! Sasa naamini kuwa Mkulo haiwezi wizara ya fedha
 
.....Nadhani hii ni kwa wageni tu ambao watakuwa wamenunua bidhaa mbali mbali nchini. Pale Airport kama wataweza kutimiza masharti yote ya kuweza kurudishiwa VAT waliyolipa wakati wakinunua bidhaa hizo, basi watarudishiwa. Mie uamuzi huu umenishangaza sana hasa ukitilia maanani hali mbaya ya kifedha ndani ya hii Serikali.

Na hii exemption ni kwa bidhaa zisizozidi thamani ya tshs 400,000/ za kitanzania.Hii ni nzuri sana kwa maendeleo ya viwanda vyetu kwani tayari hiyo ni market wazee. Viwanda vitazalisha kwa wingi kwa sababu ya ongezeko la soko serikali hapo itanufaika na kodi zingine kama corporate tax nk.
 
Wachangia mnatoa mawazo yenu kwa mtazamo chanya mkiamini kweli VAT haitatozwa kuanzia January 2012 naomba mnijulishe lini sheria ya ongezeko la thaman VAT 1997 ilifutwa na Bunge ili kodi hiyo isitozwe? Majiji kama Arusha kila leo ni matangazo ya kuhimiza wafanya biashara wanunue vingamuzi vya kukokotoa kodi nyie mnazungumzia VAT kufutwa? all who support this thread must in day dreaming
 
Kuanzia Januari mwakani, kodi ya ongezeko la thamani almaarufu VAT itaacha kutozwa kabisa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA.
Sosi: Magazetini, RFA.

TRA kuwarejeshea Vat kwa wageni
TRA kuwarejeshea Vat kwa wageni

James Magai
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekamilisha mchakato wa urejeshaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wageni wanaonunua bidhaa mbalimbali nchini kwa ajili ya matumizi, nje ya nchi.Mkurugenzi wa Fedha katika mamlaka hiyo, Saleh Mshoro, aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa utaratibu huo utaanza Januari mosi makani.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa Sheria ya VAT 1997 sura ya 148, kama ilivyorekebishwa mwaka 2011.
Mkurugenzi huyo alisema huko nyuma, raia wa kigeni walikuwa wanakatwa Vat kwa bidhaa walizozinunua nchini na kwenda kuzitumia katika nchi zao.

Alisema hata hivyo kwa mujibu wa marekebisho hayo, wageni hao sasa watakuwa wakirejeshewa fedha walizokatwa kulipia Vat wakati wakinunua bidhaa hizo.

Mshoro alisema ingawa utaratibu huo hautakuwa na faida ya moja kwa moja kwa Serikali lakini pia haikuwa halali kutoza tozo hilo hasa ikizingatiwa kuwa Vat inatokana na matumizi ya bidhaa husika.“Utaratibu huu umekuwa ukitumika katika sehemu mbalimbali duniani kutokana na ukweli kuwa Vat ni kodi inayotokana na matumizi ya bidhaa. Hata hivyo bidhaa zilizotozwa Vat kwa watu hao hazitumika humu nchini na badala yake zilikwenda nje ya nchi na kwa hiyo si vema kutoza Vat,” alisisitiza.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa fedha, wanaostahili kudai marejesho haya ni wasafiri ambao si raia wa Tanzania wanaosafiri kwenda nje ya nchi akiwa na bidhaa walizonunua Tanzania Bara kwa rejareja na kuilipia Vat.

Hata hivyo Mshoro alisema bidhaa ambazo zitastahili kurejeshewa Vat ni zile zenye thamani isiyokuwa chini ya Sh400,000 na kwamba utaratibu huo utaambatana na masharti.

Alitaja masharti hayo kuwa ni pamoja na marejesho hayo kufanyika katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JKNI) wa jijini Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).
Alisema marejesho hayo yatafanywa kupitia kwa wakala aliyeteuliwa kwa ushirikiano wa TRA na Benki ya Twiga Bancorp, ambayo itakuwa na ofisi katika viwanja hivyo.

Aliyataja masharti mengine kuwa ni muombaji kuwa risiti ambayo imetolewa na mashine ya kielektroniki (EFDs), ili kuthibitisha madai yake na kwamba risiti hiyo lazika ionyeshe maelezo ya bidhaa. “Madai kwa ajili ya marerjesho yanatakiwa yatolewe kabla ya miezi sita tangu risiti ilipotolewa na bidhaa husika zilizoponunuliwa, ziwe hazijatumika na kama zimewekwa kwenye makasha, lakiri iwe haijavunjwa,” alisema Mshoro.

“Lakini pia msafiri lazima awe na hati ya kusafiria, tiketi, na hati ya kuruhusiwa kupanda ndege (Board Pass). Nyaraka hizo pamoja na bidhaa husika zitahakikiwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato na mawakala,” alifafanua Mshoro.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani, Christine Shekidele alisema manufaa ya kutumia risiti za EFDs kuhakikisha kuwa kodi inayostahili kukusanywa inakusanywa na hivyo kuongeza mapato ya Serikali.
Hata hivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara waliojiandikisha katika mfumo wa risiti hizo kuwa waaminifu katika kutoa risiti hizo.
 
Katika mambo ambayo yanatakiwa kufanyiwa REFORMS kubwa ni mfumo wetun wa ukusanyaji kodi. Kodi inakusanywa kidogo na ni sisis wafanyakazi ndio walipa kodi wa nchi hii (labda kwa kuwa inakatwa juu kwa juu).
 
Back
Top Bottom