Tanzania kinara kupenda Utumwa

Tanzania kinara kupenda Utumwa

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
13,996
Reaction score
15,118
simba.jpg
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba

Ripoti mpya ya kimataifa kuhusu hali ya utumwa duniani imeitajaTanzania kuongoza Afrika Mashariki kwa kuwa na zaidi ya watu 350,000 wanaotumikishwa maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, jana alikiri kuwapo kwa tatizo hilo akisema: "Ni kweli kuwa wafanyakazi wa ndani wanatumikishwa hapa nchini ikilinganishwa na nchi nyingine."

Ripoti hiyo ijulikanayo kama ‘The Global Slavery Index 2014', iliyotolewa nchini Australia Novemba mwaka huu, inaonyesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya 14 barani Afrika na kuwa ya 33 duniani.

Imeitaja Uganda kuwa ndiyo inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa na watumwa 135,000, ikifuatiwa na Rwanda (83,600), Burundi (72,300) huku Kenya ikiwa na watumwa 64,900.

Utafiti huo uliofanyika katika nchi 167 duniani, unatafsiri utumwa kuwa ni hali ya mtu kumhifadhi mtu mwingine na kumnyima uhuru binafsi kwa nia ya kumnyonya kwa njia ya madaraka, faida au kumsafirisha.

"Mataifa mbalimbali yanatumia maneno tofauti kuuelezea utumwa mambo leo, ikiwa ni pamoja na kusafirisha binadamu, utumikishwaji, ndoa za lazima, kuuzwa kwa watoto. Maovu yote yanazungumzia jambo moja," inasema ripoti hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa hivi sasa kuna watumwa milioni 35.8 duniani kote, kati yao milioni 14 wapo India, milioni 3 wapo China na milioni 2 wanapatikana Pakistan. Akizungumzia ripoti hiyo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba alisema hali imefika ilipo sasa kutokana na kukosekana kwa sheria kali na vyama vyenye nguvu vya kutetea haki za wafanyakazi hao.

Waziri Simba alisema kwa sasa ni jambo la kawaida kumsikia mtu akijisifu kuwa amekaa na mfanyakazi kwa miaka mitatu bila kwenda likizo.

"Mtu anasema ‘nimekaa naye miaka mitatu msichana huyu ni mzuri' kwa hiyo nini? Anakaa kwako kwa sababu umeshindwa hela ya kumlipa akapange kama wafanyakazi wengine," alisema.

Aliongeza: "Msichana anakuwa wa kwanza kuamka asubuhi na wa mwisho kulala usiku, akupikie mchana, usiku na akufungulie mlango unaporudi. Ndiyo maana wasichana wanawadhuru watoto wanaokaa nao."

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na naibu wake, Dk Makongoro Mahanga hawakuweza kupatikana kuzungumzia ripoti hiyo baada ya simu zao kuita bila kupokelewa.

Kuhusu Afrika, ripoti inaonyesha kuwa Nigeria ndiyo inayoongoza kwa kuwa na watumwa 834,200, ikifuatiwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) (7,620, 900), Sudan (429, 000), Misri (393, 800) na Tanzania (350,000).

Nchi yenye watumwa wachache zaidi dunia ni Iceland ambayo inachini ya watu 100 wanaotumikishwa. Mauritus yenye watumwa 3,300 ndiyo iliyotajwa kuwa ya mwisho Afrika kwa kuwa na watu wachache.

Ripoti hiyo, pia imetaja nchi zinazoongoza kwa kuwa kuweka mikakati imara ya kupunguza idadi ya watu wanaotumikishwa. Nchi hizo zimetambuliwa kwa kupewa maksi kulingana na alama zilizopata. Netherland imetajwa kuwa na sera nzuri zaidi duniani baada ya kupata alama AA.

Nchi nyingine zilizofuatia na alama zao kwenye mabano ni Sweden (A), Marekani (BBB), Australia (BBB) na Switzeland (BBB).

Kwa upande wa Afrika, Nigeria ndiyo imetajwa kuwa na sera nzuri baada ya kupata alama B, ikifuatiwa na Zambia (CCC), Senegal (CCC), Uganda (CCC) na Ghana (CCC).

Vilevile Uganda imetajwa kuwa na mikakati bora ya kupunguza idadi ya watumwa Afrika Mashariki baada ya kupata alama CCC ikifuatiwa na Kenya (CC), Rwanda (CC), Burundi (CC) huku Tanzania ikishika ‘mkia' kwa kuibuka na alama C. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, alama C inamaanisha kuwa jitihada za Serikali kuondoa tatizo ni ndogo sana, huku kukiwa na idadi ndogo ya waathirika waliopata msaada.

Baadhi ya sera na vitendo vya Serikali vinarahisisha kuongezeka kwa watumwa.

Source:Mwananchi.co.tz
 
Kuna topic hapa ya wafanyakazi wa majumbani tuliiongelea sana hapa na kuitaka serikali iweke kiwango cha juu cha malipo lakini chini ya serikali sikivu kutoka kwa Mafisadi haikusikia na kusema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala.
 
Kama kuna nchi inayoongoza kwa kuwa na rekodi nyingi za ovyo ovyo basi tanzania inaongoza.Matokeo ya serikali ya ccm
 
Halafu WaTZ tumekuwa mbele mbele na kimbelembele kunyoshea vidole watu wengine !!! kumbe uchafu wote tunao humu..
 
Wachangiaji wote humu wa JF !! wenye damu za kibaguzi wametimua mbio....Nduki !! hawaonekani ktk. UZI huu !!!

muumbuko huo!!
 
Utumwa mamboleo upo na waziri wa jinsia na watoto pia aangalie na hao watoto wasioenda shule na kuwa vibaka au kuuza machupa tupu na kutumikishwa na watu na wasichana kupewa mimba ovyo baada ya kukosa malezi mazuri hayo pia uyashughulikie kwa kina.
 
Kila mtu ajifanyie kazi yanini kumtumikisha binadamu mwenzio kwa malipo ya 20,000 it's a slavery na hata waajiri wanaowalipa wafanyakazi zao sehemu za kazi na makampuni hayo tunayajua ukianza na IPP MEDIA ni utumwa pia kwa binadamu ..unawezaje ukamlipa mtu mwenye dip 250,000? kama huu sio utumwa nao tuuiteje
 
Tanzania imetajwa kuwa kinara wa utumwa miongoni mwa mataifa ya Afrika mashariki katika ripoti ijulikanayo kama The Global Slavery Index - Kielelezo cha utumwa duniani mwaka 2014, ripoti iliyotolewa nchini Australia mwezi Novemba.

12808_891915834187078_8802495429949270787_n.jpg

Source: Copy and past from fb ya dw
 
Hii habari ilitoka hata kwenye baadhi ya magazeti ya juzi.Ni aibu kwakweli.
 
Tanzania imetajwa kuwa kinara wa utumwa miongoni mwa mataifa ya Afrika mashariki katika ripoti ijulikanayo kama The Global Slavery Index - Kielelezo cha utumwa duniani mwaka 2014, ripoti iliyotolewa nchini Australia mwezi Novemba.

12808_891915834187078_8802495429949270787_n.jpg

Source: Copy and past from fb ya dw
Hii nchi ni nchi ya kipuuzi kabisa!tulishasema yote but waswahili wanasema oohoo wanatafuta riziki!...angalia jinsi wahindi wanavyofanya watz watumwa but serikali kimya tu....tanzania ina watumwa wengi sana.......hasa mijini
 
Ila najiuliza, mbona nikitembelea website ya ' the global slavery' Nigeria ndio inaongoza? ama mimi nashindwa kuinterprite?
 
Utumwa wameuainishaje?

Ninavyojua mimi nchi inayoongoza kwa utumwa Afrika ni Mauritania.
 
Makaura na Kiranga kaeni chini basi mtueleweshe!

Hii ripoti imelaumiwa katika kipindi kimoja nilikuwa nasikiliza BBC World Service, wamesema kwamba imeungwa ungwa tu bila data za kutosha na kuna nchi nyingine ambazo hawakuwa na data nazo wameziunganishia tu kwa kusema "nchi hii hatuna data lakini tunaiweka hapa kwa sababu hii ni kama ile".

Leaps of extrapolation.

Basically wameungaunga sana.

Na utumwa unaoelezwa sijaelewa.

Ma housegirl wanaolipwa mishahara midogo lakini walio huru kuondoka ni watumwa?

Kama ni watumwa Tanzania si ajabu kuongoza.

Lakini kama utumwa ni mtu kulazimishwa kuwa chini ya miliki ya mwingine, Tanzania haiwezi kuzishinda Sudan na Mauritania.
 
Last edited by a moderator:
tanzania tunaishi ishi tu......serikali yenyewe haina vision
watoto watumwa watazidi kuwepo...
 
Naanza kuisoma ripoti hapa, katika nchi 11 zilizokuwa ranked "the prevalent of slavery is highest in" Tanzania haimo.

Pia "in absolute terms, the countries with the highest number of slaves are" zimetajwa nchi 11, Tanzania haimo.

The former has Mauritania and Sudan (just as I predicted off the top of my head without reading the report), the latter has Nigeria.

Soma mwenyewe www.globalslaveryindex.com
 
Hii itakuwa inawagusa wengi maana kila mwanamke wa kibongo anahitaji kuwa na msichana wa kazi
 
Back
Top Bottom