Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,750
- 5,641
Tanzania tunakwama wapi???
1.Tanzania;
Una mgonjwa mahututi ndani, lakini unamuacha ili uwahi mazishi ya mtu alie kufa ambae hata sio ndugu yako!
2. Tanzania;
Mgeni akija nyumbani anakula vyakula vizuri kuliko familia yako, na anatumia vyombo vizuri kuliko familia yako.
3. Tanzania;
Ukiugua Ukaomba michango utibiwe hakuna anae jitokeza, ila ukifa wanatoa mpaka offer za maji, chakula, usafiri, na jeneza!
4.Tanzania;
Unamuomba mtu msaada wa sh 10,000 anakwambia sina ila anakwambia twende tukanywe bia anakununulia bia za 30,000.
5. Tanzania;
Watu wote mtaani wanajua mke wako au mme wako anachepuka, lakini hakuna wa kukwambia, wana ogopa kusutwa![emoji2957][emoji2957][emoji2957]
6. Tanzania;
Unavunjiwa nyumba usiku wezi wanaiba, hakuna jirani anae muona mwizi, lakini usiku ingiza mchepuko, asubuhi wote wanajua![emoji849][emoji849]
7. Tanzania;
Ukienda bar na mwanamke, wahudumu hawakuchangamkii na wanaweza hata kumpiga kikumbo usipokuwa makini.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
8. Tanzania;
Wenye vitambi wanaheshimiwa kuliko wasio navyo, ukienda kwenye harusi na kitambi hata kadi huulizwii, ngoja uende kibau mbau uone sura ya mtu wa getini![emoji23][emoji23][emoji23]
9.Tanzania;
Ukimkopesha mtu hela mnakuwa maadui, usipo mkopesha mnaendelea kuwa marafiki.
10.Tanzania;
Watu wanafuatilia mambo ya wasanii na kujua mpaka siri za ndani, lakini muulize mtu, asili ya ukoo wao, akutajie babu wa babu yake anaitwa nani hajui![emoji12][emoji12][emoji12]
11. Ukiwa na hela unaishi vizuri mtu anakuchukia tu bila sababu, na utaambiwa unaringa, unajisikia, kumbe tu umepambana umetusua![emoji57][emoji19][emoji57]
12. Tanzania;
Mtu yuko kwenye magroup sita, la primary, secondary, chuo, kazini, manchester fans etc, kote huko kila siku mtu kafiwa uchangie, anaoa uchangie, anaolewa uchangie, anaumwa uchangie, ...wewe nani uwe na hela zote hizo??
Maisha yataacha kuwa Magumu?? Punguza network isiyo ya lazima!
Watanzania tubadilike
Sponsored by unknown anonymous [emoji134]