Tanzania is viable for revolution politically. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania is viable for revolution politically.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njangula, Apr 22, 2012.

 1. N

  Njangula Senior Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dear JF members, ongoing circumstances in Tanzania provide a guarantee for mass revolution and the world will understand it just as they recognised a situation of Egypt, Tunisia and Libya. It's a revolution not coup detat. The mass will pioneer it not the army. People of lower classes suffers a lot from decays of top leaders. President is stubborn against mass cry. Anawalinda wahuni, anajilinda mwenyewe na jamaa yake. Waziri amedunishwa sana kwa kupingwa mawazo yake. It's high time to topdown him. 200 years ago Egptian nationalist Arab Pasha succeed to remove corrupt,bankrupty government from power,the same in Phillipines the corrupt Marcos was destroyed, kwa nini isiwe Tanzania? Rais anasema "ni upepo unapita" yupo sahihi kwani waTZ hupiga tu longo2 halafu wanasahau. Tuunde kamati ya Ukombozi ya Taifa (KAUTA). Tanzania will not be liberated by secret ballot. Ruling party once ascended, descending need sacrifice. Nawasilisha. SAUTI YA MTU ALIAYE NYIKANI.
   
 2. doup

  doup JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  umesomeka, inasikitisha na kuumiza
   
 3. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Naomba kukubaliana na wewe kwamba Tanzania pana tatizo, na kwamba tatizo kubwa tulilo nalo ni rushwa, rushwa ambayo ukiichambua sana inaweza ikawa na uhusiano na ufinyu wa uelewa wa kitu kinaitwa 'moral philosophy."

  Moral philosophy haiwezi kueleweka vizuri kwenye cabinet yenye darasa la saba ndani yake. Pamoja na udhaifu mkubwa wa cabinet yetu, naomba nawe sasa ukubaliane nami katika hili: Kwamba uchumi wa Tanzania ukiingizwa katika vurugu za Libya, Tunisia, Misri na kwingineko katika hayo mataifa yenye utajiri mkubwa wa mafuta, matokeo hayatakuwa sawa. Wananchi wengi watapoteza maisha yao SI kwa sababu ya magruneti, bali kwa sababu ya njaa kutokana na uzalishaji hata huo duni uliopo kusimama.

  Tafsiri yangu ya matukio ya siku za karibuni kule Arusha na kwingineko Tanzania ni kwamba watendaji wa serikali wametambua kwamba wananchi wamechoshwa na utawala wa CCM. Lakini pia CCM wenyewe wamekwisha jua kwamba wananchi walio wengi wamewachoka.

  Si busara kushabikia vurugu katika mazingira ambayo yapo tayari kwa mabadiliko ya amani. Nakusihi ukubaliane na hili. Tumia vigezo vya wana ccm kuhamia upinzani kwa uwazi, tumia vigezo vya polisi kukimbia vijana arusha, tumia vigezo vya
  mashushushu kuweka leaks za taarifa katika magazeti na hata JF kukubaliana na mimi kuwa mfumo wetu upo tayari
  kufanya mabadiliko kwa amani.

  Ombi langu kwako ni hili: Washauri Chadema kwa upande wa Bara na CUF kwa visiwani, waandae sasa Cabinet mbadala wakisubiri kuchukue serikali miaka mitatu ijayo. Huu muda uliobaki unatosha kuanza upembuzi yakinifu kujua nani atakuwa wapi katika cabinet mpya, nani wa CCM abaki wapi nani atoke--kwani si kila CCM ni mbaya! Kuna watu wazuri tu CCM. Na kama nilivyowahi kudokeza awali, kuwa na kipaji cha akili nyingi ndani ya CCM ni tatizo. Huwezi kukaa kule kwa sababu utazidiwa nguvu na vilaza waliojaa huko. Na kwa sababu hiyo kuna vipaji kibao vimefichwa kule. Ni wajibu wenu sasa nyie mliopo upinzani, katika kipindi hiki cha mpito, kuvitambua vipaji hivi ili kujua ni kwa namna gani mnaweza kuvitumia baada ya kupata cabinet mpya mwaka 2015. Si kila mwana CCM ni mbaya. Obama alifanya kitu ninachokisema hapa: Kufuatia ushindi wake, aliamuru chaguo la wapinzani Republican Party kwenye nafasi ya Usalama wa Taifa libaki na kutumiwa na Democrats: na hali imekwenda vizuri sana kwenye eneo hilo katika nchi ile.

  Si busara kushabikia vurugu katika mazingira ambayo yapo tayari kwa mabadiliko ya amani.
   
 4. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Piga chini hawa itisha uchaguz huru within 3months. 2015 mbali sana jaman taifa litakua limecollapse so we must act nw. Naunga mkono hoja.
   
Loading...