Watanzania lazima tukubali kuwa hatua ya wafadhili ni pigo kwa nchi yetu. ni lazima tuchague njia sahihi ya kutufikisha tunakokwenda.
kwa mtizamo wangu yapo mambo serikali yetu inaweza kufanya.
1. kutunishiana misuli na wafadhili hakutatusaidia bali kushuka chini na kutambua kuwa yapo mambo wanazungumza yanakuwa na mantiki. serikali ya awamu ya tano imeonyesha nia ya dhati katika kusimamia haki na yapo mambo yamefanyika huko nyuma hawawezi kubadilisha lakini wanachoweza kufanya ni kuwaonyesha wafadhili hawa kuwa tunasikitika kwa kukosa ufadhili wao na mabadiliko ambayo serikali hii imeyalenga hayawezi kuja kwa mara moja bali jamii itabadilika taratibu. hapa suluhisho ni serikali kuanzisha mchakato wa katiba mpya unaojumuisha wataalamu ni kuweka misingi ya taifa iliyo imara lakini ambayo haitaonyesha kupendezesha kundi fulani la siasa.
2. upo uwezekano kuwa mbali na matatizo yetu ya ndani lakini diplomasia yetu kimataifa inaweza kuwa inalega na ndio chimbuko la mtikisiko mkubwa. raisi anatakiwa kuangalia timu yake ya washauri pamoja na timu inayojihusisha na diplomasia ya kimataifa ili kuona kama kunahitajika overhauling.
3. kusitishwa kwa ufadhili ni pigo kubwa sana katika bajeti yetu. hapa hakuna mjadala ni lazima bajeti ya serikali ifumuliwe na kuweka vipaumbele vipya ili kulinda uchumi wetu. lazima tutambue kuwa misaada hii ilikuwa ni source kubwa ya foreign currency. tukijidai kukusanya kodi na kutekeleza bajeti tuliyokuwa nayo ni wazi tutakumbana na mporomoko mkubwa sana kwa shilingi yetu kushuka thamani.
je wewe kama mtanzania unadhani ni kitu gani kifanyike?