Tanzania inaonekana kituko katika EAC community

Tanzania inaonekana kituko katika EAC community

Watu wa aina yako mtadanganywa sana, actually ukweli ni kuwa wanaitamani sana TZ na hawana lolote ni habari za chuki tu.
Kenya kwa rushwa na ukiritimba ni kinara. Nyie kaeni kutegemea habari kama, ni njia ya kuwadhoofisha mjisikie dhaifu.

Waulize waliotembelea nchi hizi na kuona mambo yalivo, si kwenda Nairobi na kurudi.
Sikia fidivin! ni kweli kuwa wakenya wanaitamani sana Tanzania, na ni kweli kenya kuna rushwa na ukiritimba mkubwa lakini turudi kwenye content ya habari iliyoandikwa: hivi kwani ni uongo kuwa Rwanda inaongoza kwa kufanya vizuri? ni uongo kuwa Tanesco inaendeshwa ovyo sana? ni uongo kuwa mashirika ya umma yamefanywa apparati za ccm?
Haya yote yako wazi sasa ni kwanini tushambulie vyombo vya habari vya kikenya wakati kinachoandikwa ni kweli tupu? Wakati fulani mwaka 2005 moja ya vyombo vya habari vya kenya kilichora katuni ikionesha waandishi wa habari wa TZ wakimlamba viatu kikwete, waandishi wa TZ wakalalamika sana kudhalilishwa lakini si ni kweli kuwa waandishi walimpamba sana kikwete kiasi cha baadhi ya viongozi wa dini kusema ni chaguo la mungu? Mwisho kinachoongelewa ktk habari ile ni mafanikio ktk uchumi mkubwa (macro economy) na sio uchumi mdogo (micro economy) ni ukweli uliowazi kuwa kenya inafanya vizuri ktk uchumi mkubwa kuliko sie kwa hiyo usitumie reference za ugumu wa maisha ktk kibera, mathare na maeneo ya Garissa na Turkana kaskazini mwa kenya kama kigezo cha kuonesha kenya inafanya vibaya zaidi yetu.
 
Nyunyu,

I agree with you kuna tatizo KUBWA la uongozi, maana kwa kiwango kikubwa kutokuwajibika ni dalili tu ya ubovu wa system ambayo inashindwa kumuwajibisha asiyewajibika. System ni watu waliopo kwene top-layer ktk maamuzi. Nakubaliana na wewe kuwa watu waliotakiwa kuibadilisha hiyo system ya ulaji ni CCM, they are sole engineers of this corrupt system.
 
Back
Top Bottom