Tanzania inakwenda mrama!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania inakwenda mrama!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by luddo17, Mar 25, 2011.

 1. l

  luddo17 New Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi naogopa sana yale yanayotokea hivi sasa huko katika nchi za kiarabu, yasije yakatokea pia hapa Tanzania. Ndugu zangu, hali ni mbaya sana. Mamilioni ya watu wamejimwaga mitaani na kuzunguka majengo ya serkali ikiwa ni pamoja na kituo cha televisheni cha taifa.
  Swali la msingi la kujiuliza, kipi ni chanzo au chimbuko la hayo yanayotokea? Jibu ni UONGOZI. Wananchi wa nchi hizo, walikuwa watulivu kwa miaka mingi tu. Lakini sasa wananchi hao wamechoshwa na uvumilivu umewashinda. Wanashinikiza viongozi wao kuachia madarakani. Sio kwamba ni kwa sababu wamekuwa madarakani kwa muda mrefu, bali ni kutokana na utawala wao mbovu usiozingatia mahitaji muhimu ya wananchi wao. Wananchi wamezidi kuwa masikini na uchumi kuzidi kudorora, licha ya utajiri mkubwa ilizo nayo nchi hizo. Ukosefu wa ajira na huduma mbovu za kijamii, ni miongoni mwa mambo/sababu zilizopeleka kuibua hasira za wananchi wa mataifa hayo ambayo yalikuwa tulivu kwa kipindi cha miongo kadhaa.
  Hapo juu nimesema naogopa hayo ya nchi za kiarabu kutokea hapa kwetu, kwa vile shari si kitu chema. Lakini wasiwasi wangu mkubwa unajengwa na sababu zile zile zilizowafanya Waarabu wakose subira. Sababu hizo hizo ndizo naziona zinaanza kuwaingia watanzania ambao wengi wao sasa wamekata tamaa ya maisha, kufuatia kuandamwa na umaskini wa kutupwa; umaskini unaotokana na kupanda kwa gharama za maisha. Hivi sasa Mtanzania anaugulia maumivu makali ya kupanda kwa bei za mafuta, mgao mkali wa umeme unaoendelea, kupanda kwa gharama za umeme, maji na uchukuzi. Elimu na huduma mbovu za afya, ni miongoni mwa changamoto zinazozidi kumtesa mtanzania huyu ambaye mwaka huu anaazimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi yake! Migomo ya wasomi wa vyuo vikuu, matokeo mabovu ya mitihani ya kidato cha 4 na vurugu sehemu mbali mbali za nchi, ni ishara wazi kuwa watanzania wale waliokuwa ndani ya nchi iliyokuwa ikijulikana kama kisiwa cha amani, wanazidi kukata tamaa, kwa sababu wakijiuliza chanzo cha hayo ni serkali yao kutojali kutimiza na kutekeleza ahadi zake. Wanajiuliza iweje wawe maskini ndani ya nchi yenye utajiri wa hali ya juu! Kama si sera na mipango mibovu, nchi hii ingeweza kukapita ka-nchi kadogo kaitwako Uswisi ambako hakana hata simba mmoja, achilia mbali ardhi ya kutosha, misitu, maziwa na maliasili kadhaa kama zilizopo Tanzania. Tanzania tuna Tanzanite! Tuna mbuga za wanyama! Tuna Mlima Kilimanjaro! Tuna mito na maziwa makubwa! Tuna Ngorongoro crater! Tuna Almasi! Tuna dhahabu! Tuna gesi! Bwana wetu Yesu Kristo aliwaambia wafuasi wake wajifunze alama za nyakati! Viongozi wetu nanyi badilikeni! Hatupendi yatokee ya huko Arabuni!
   
Loading...