Francis fares Maro
JF-Expert Member
- Jun 20, 2021
- 1,227
- 1,341
Wasalaam
Kama vile nchi yetu na viongozi hatujui tunataka nini, tunaenda wapi na tuko wapi?
Huku COVID-19 na katazo la mikusanyiko, lakini viongozi ndio wa kwanza kufanya mikusanyiko (unajiuliza nini hiki!)
Huku Tozo za miamala ya simu kupandishwa, kule petrol imepandishwa juu, hapa kila ukiingia kwenye menu ya bank kupitia simu unakatwa!!!
Vyakula vitapanda bei maradufu, usafiri utapanda, vijana bado ajira za uhakika hakuna…
Viongozi kujiona wao ndio miungu watu, huyu anadai tutakaa kuzungumzia swala hili la Tozo, yule anatuambia kama huwezi nenda Burundi na huku tunasikia “tumeshapitisha hakuna njia nyingine ya kupata mapato”
Hofu ya Uwekezaji
Ukiangalia Kwa upana hakuna mwekezaji anaweza kuweka fedha yake kwenye nchi namna hii hatujui tunataka nini, tunaenda wapi na tufanyeje!! Kila mwenye mamlaka anachoona kinamfaa yeye ndio sahihi, kuhusu Sisi wananchi tutajua wenyewe.
Nimewaza mbali, hivi Kwa mwendo huu halafu tunasikia kuna watu wana kesi za ugaidi iwe kweli au uongo hivi kuna mtu atakuja kuweka fedha yake hapa?!