Tanzania inaelekea wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania inaelekea wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Exaud J. Makyao, Oct 10, 2009.

 1. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya kujiuliza ni wapi Tanzania inaelekea.
  Lakini sijui Tanzania inatoka wapi na sasa iko wapi.
  - Kiuchumi
  - Kijamii
  - kisiasa
  - Kiutamaduni, n.k.

  Ajuaye anipe mwanga tafadhali.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Zamani tulivaa buga na max
  Sasa tunavaa mini skirt na kata k"
  Baadaye tutatembea uchi!...lol!
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,483
  Trophy Points: 280
  Tulikuwa na Nyerere sasa tuna Kikwete
  Tulikuwa na Kawawa sasa tuna Pinda
  Tulikuwa na Karume sasa tuna Karume
  Tulikuwa na Kinjekitile sasa tuna Kingunge Ngombale Mwiru
   
 4. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pakajimi,
  Hii ni hatari.
  Nini kinatupeleka huko kutembea uchi?
  Mtazamo wako unatisha mkuu
   
 5. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Chrispin,
  Inafurahisha kweli kweli.
  Na baada ya Kikwete na Pinda ni nani?
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,483
  Trophy Points: 280
  Baada ya Kikwete anakuja Lowassa / Membe
  Baada ya Pinda anakuja Adam Malima
  Baada ya Karume anakuja Karume Mdogo au Abas Mwinyi.

  Weka kwenye kumbukumbu zako, utakuja kunibatiza Sheikh Yahya Hussein siku za usoni.
   
 7. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi sisemi neno mkuu.
  Utabiri wako unafurahisha na kushtua kidogo.
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  hakuna mwelekeo wowote yaani tupotupo tu.......
   
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,483
  Trophy Points: 280
  Usistuke mkuu, we furahi tu. Ndio Sihasa za Tanzania hizo.
   
 10. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ili kutoshtuka kunahitajika nguvu ya ziada kuamini.
  Kama itakuwa hivyo, itabidi watu tujiulize sawa na ile thread yako kwamba KUNA UMUHIMU WA KUPIGA KURA TENA?
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,483
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nakuambia ndugu yangu. Kama mfumo mzima wa tume ya uchaguzi na taratibu za uchaguzi kwa ujumla havitabadilishwa. Hao niliokutajia watakuwa viongozi wetu tutake tusitake. Kwa mantiki hiyo basi, kama itabakia hivihivi, siku wakati nyie mtakuwa mmepanga mafoleni kupoteza muda wenu kupiga kura, mi ntakuwa kaunta najilambia serengeti yangu baridi na kitimoto cha moto
   
 12. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nchi imepoteza mwelekeo, kwa sasa tunakwenda tusikokujua. Gari liko katika mwendo na mara dereva kalala usingizi ama hajui kuendesha unafikiri gari litaenda vipi?. Tulikotoka tulikuwa na dira (enzi za Nyerere) lakini kwa sasa bora liende, na nchi haina mwenyewe, fanya utakacho na utakapo hakuna wa kukufanya kitu chochote.
  Serikali inatishiwa na wezi, umeona wapi katika dunia hii?. Ukiwakamata wezi nchi itayumba. Hii nimeiona na kusikia Tanzania tu.
   
 13. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  1. Kiuchumi tupo kwenye soko huria as per IMF/WB guidelines tunafuata watakavyo tuko enzi za Mkapa hadi enzi za Kikwete
  2. Kijamii-Tuko kwenye globalization...tumekubaliana tuka enzi za Mwinyi kwamba sisi siyo kisiwa, mkapa akafuata nyayo akampe kijiti hichohicho kikwete same direction..kijamii tunaangalia globe inafanya nini tunafanya ..mfano America Idols..(in US) in TZ bongo search etc.
  3. Kisiasa..sera yetu ni kushinda uchaguzi kwa kishindo ili kukomesha wapinzani wapiga kelele kina Slaa, Lipumba etc bila kujali dhamana za kisiasa
  4. Kiutamaduni- tunafuata america/uk a.k.a western style ukiwa against utakuwa mshamba, hujasoma (backward all bard names),
  Kwa ufupi ni hayo, You either join them or wait and see!
   
 14. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii imekaaje mkuu?
  Lazima watoa hoja watakujibu bila shaka.
   
 15. 1

  1954 JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,282
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Tanzania inaelekea wapi? Hili ni swali zuri la kujiuliza kwa wale wote wanaoitakia mema nchi hii. Sijasoma makala, kama ipo, kuhusu swali hili kwamba serikali inaelekea wapi.

  Pamoja na hayo nitoe mchango wangu kidogo. JIBU la jumla kwa swali hilo na kwa kuzingatia hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi iliyopo nchini kwa sasa ni kwamba TANZANIA INAELEKEA KUZIMU.

  Tanzania ya sasa siyo ile ya miaka ya 1960 ambapo wananchi walikuwa na matumaini makubwa ya maisha bora ya baadaye baada ya ukoloni. Wala tanzania hii siyo ya miaka ya 1970 au 1980. Tanzania ya sasa ni ya wananchi waliokata tamaa; wavivu; wapiga majungu; na walafi wa kupindukia.

  Mtu (aliyeko kwa nafasi ya ulaji) anajilimbikizia bilioni 20 lakini shule zetu ziwe na primary aju sekondari au hata vyuoni hakuna vifaa vya kutosha. Rushwa imetawala kila mahali. Huna pesa sasa na unaumwa ni lazima utakufa tu. Huwezi kutibiwa Muhimbili au hospitali yoyote ile ya serikali na siku hizi hata za binafsi bila kutoa rushwa.
  Watanzania ni wavivu, inherently wavivu, siyo wachapa kazi wakiwa hapa Tanzania. Makampuni ya nje yakija hayapendi kuajiri watanzania kwa kuwa ni wavivu na wapiga majungu wakuu. Kwenye maeneo ya kazi vyama vya wafanyakazi (Trade unions) kazi yao ni kutetea wavivu na majungu. Trade unions zinajifanya zinatetea haki lakini kimsingi zinatetea uozo uliopo nchini mwetu kwenye maeneo ya kazi.

  Dar es salaam ni jiji chafu kupindukia lisilo na nidhamu kwa upande wa wakazi wake. Kila mtu ni mjanja. Dereva wa gari anaweza akasimama katikati ya barabara na kuanza kupiga soga na wengine na wala asijue kuwa kwa kufanya hivyo anasababisha foleni na adha kwa wengine. Na hata akisababisha foleni atafanywa nini?

  hakuna anayewajibika tanzania kila mtu ni mjanja. Tuna mawazo bado ya kinyama kwa kutostarabika. Tanzania ilivyo sasa inahitaji dikteta au utawala wa sheria za kijeshi ili kutuwaajibisha. Demokrasia ya vyama vingi vya siasa ni ujinga mtupu. Kila muda ni siasa siasa siaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaasa tu.

  Wanasiasa wanawazia uchaguzi tu. Mtu ameitumbukiza nchi hii kwenye matatizo lakini bado ana mawazo ya urais mwaka 2015 au hata 2010. Vyombo vya habari ndiyo usiseme, waandishi wa habari au tuseme wahariri wana misimamo yao au mtu wao. Fulani anaweza kuwa fisadi kwa gazeti au redio fulani lakini huyo huyo anaweza kuwa mtu safi kwa gazeti au chombo kingine cha habari.

  Magazeti yanaanzishwa kwa kuwaandama watu wengine na kuwasafisha watu wengine. Waandishi wa habari hawawezi tena kuwakomboa watanzania kwani nao ni mafisadi. Yaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani tuko matatizoni. Tunaelekea kuzimu. Nothing is working in this country. Magazeti yamekaa kuandika umbea tu. No serious analysis on serious issues. Every thing is taken lightly.

  Rwanda inatupita kimaendeleo na sisi tumekaa tu. Burundi nayo itakwenda kwenye maendeleo sisi tunakazania kuimba wimbo usio na tija kwamba eti Tanzania ni nchi ya amani. Iko wapi hiyo amani na mshikamano au umoja wa kitaifa kama sio utani wa karne?
   
 16. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu 1954,
  Haya mwazo yako yamejaa falsafa.
  Naamini kila ayasomaye, atasema neno.
  TZ INAELEKEA KUZIMU?
  Hii inatisha.
   
Loading...